Deontay Wilder vs Tyson Fury -2

Deontay Wilder vs Tyson Fury -2

Leo hawa mabondia kutoka UK na US wametifuana nimesoma kwenye mtandao Tyson Fury kutoka UK amemshinda Deontay Wilder kwa TKO raundi ya saba. Wale walofanikiwa kuuona live huu mpambano watupe tathmini kidogo hali ilivyokuwa, manake wengi walikuwa wanatupa karata kwa Deontay Wilder .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo hawa mabondia kutoka UK na US wametifuana nimesoma kwenye mtandao Tyson Fury kutoka UK amemshinda Deontay Wilder kwa TKO raundi ya saba. Wale walofanikiwa kuuona live huu mpambano watupe tathmini kidogo hali ilivyokuwa, manake wengi walikuwa wanatupa karata kwa Deontay Wilder.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wilder kapigwa kama mbuzi! Nimesikitika sana mtu mweusi kupigwa na mzungu!
 
Toka enzi za kina tyson sijawahi kuona tena ngumi za maana.

Nilikua nasikia watu wakiwazungumzia hawa wapiganaji nikasema ngoja labda nitafurahia kuangalia ngumi miaka mingi sijaangalia.

Nimeangalia nikajilaumu kupoteza muda wangu, hakuna ngumi kabisa, ni kuruka ruka na kukimbia kimbia tuu.

Sijui tena kwenye kizazi changu kama atakuja kutokea mtu kama Iron, Evander, Lenox, nk.
 
Mkuu Tyson,evander,lewis na wengine walikua Konyo nimeangalia mechi zao dah noma sana hasa tyson amenivutia sana huyo mtu.
Toka enzi za kina tyson sijawahi kuona tena ngumi za maana.

Nilikua nasikia watu wakiwazungumzia hawa wapiganaji nikasema ngoja labda nitafurahia kuangalia ngumi miaka mingi sijaangalia.

Nimeangalia nikajilaumu kupoteza muda wangu, hakuna ngumi kabisa, ni kuruka ruka na kukimbia kimbia tuu.

Sijui tena kwenye kizazi changu kama atakuja kutokea mtu kama Iron, Evander, Lenox, nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngumi kali na za ushindani zimehamia kwenye uzito wa kati,kuna vijana wapo vizuri sana ukicheki mapambano yao unaenjoy.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huku heavy weight hakuna kitu kabisa.

Nimeangalia pambano la hao jama, kisha nikarudi kuangalia la kwanza nimeamini hakuna mpiganaji wa heavy weight wa maana zama hizi. Kuna yule anaitwa AJ ndio hakuna kitu kabisa.

Uingereza wapigaji ni Lenox na Haye tu, ila hawa kina AJ, Dereck Chisora, Fury, sijui nani hakuna kitu.

Zama zangu ngumi zimeishia kwa kina Vitali Klitchiko.
 
Ukisemacho ni kweli mtupu mkuu!

Ukionacho ndio nikionacho.
Mkuu tena wana style ya kumtegemea refa. Yani refa anafanya kazi kubwa kama naye ni mmojawapo wa wapiganaji. Nikitazama video za kina Foreman wanapigana mpaka unajiuliza kazi ya refa nini sasa kama si kutangaza mshindi. Hawa kina Joshua na Furry wanakumbatiana sana, nimesikitika kuona eti hii ni big match ya mwaka tena iliyokuwa ya mahasimu wa muda mrefu.
 
Huku heavy weight hakuna kitu kabisa.

Nimeangalia pambano la hao jama, kisha nikarudi kuangalia la kwanza nimeamini hakuna mpiganaji wa heavy weight wa maana zama hizi. Kuna yule anaitwa AJ ndio hakuna kitu kabisa.

Uingereza wapigaji ni Lenox na Haye tu, ila hawa kina AJ, Dereck Chisora, Fury, sijui nani hakuna kitu.

Zama zangu ngumi zimeishia kwa kina Vitali Klitchiko.
Sasa huyo Klitschko alipigwa na AJ kama mtoto
 
Back
Top Bottom