Depression inanimaliza, sina muda mrefu wa kuishi

Mkuu unaweza shangaa ila bado nasoma .. ningekuwa nimemaliza miaka mingi sana ila hii hali ilinichelewesha. Wenzagu karibia wote tayar wameajiriwa na wana maisha yao. Naamini na mimi siku moja nitamaliza pia
 
Mkuu mimi ni mwanafunzi wa kada ya afya.. bado napambana na kitabu.. ila nakushukuru kwa ushauri wako mzuri .. chanzo nimekieleza tayar kwenye nyuzi hii hii
 
Ahsante sana ndugu yangu, kiukwel hata wazazi hawajawahi kunielewa kuhusu hali yangu.. wakati mwingine hata jamii inaona nafanya makusudi.. nashukuru sana kwa ushauri huu mkuu
 
Pole sana naona watu wanawahi kutoa ushauri bila kujua mtoa mada ana depression ya nn kitu gani kinamtatiza kikijulikana ndyo aelekezwe afanye nn pole sana
 
Pole kwa changamoto, tenga muda wa kufanya mazoezi ya mwili yale ya kungfu huku ukifanya meditation at the same time yanasaidia sana ku control emotion zako.

Pia itambue sababu inayokupelekea kuwa hivyo kisha ikatae kwa kubadilisha lifestyle yako mkuu, nakuombea kila lenye heri.
 
Kama unajua huna siku nyingi za kuishi na unajua shida ni depression basi R.I.P. Ninachojua mtu anayejua chanzo cha tatizo pia utatuzi anao pia Kwaheri. Wacha kudekadeka JF, jisimamie mwenyewe kwani maisha yako ni wajibu wako, wala siyo wajibu wa wazazi wako, ndugu zako, marafiki zako au JF members. 😑😑😑😑
 
 

Attachments

  • VID-20241230-WA0132.mp4
    8.6 MB
Wee unajua depression ilivyo au kwakua unaiskia tu redioni na Tv ndo unaona anadeka!?.

Ukiwa na depression akili haifanyi kazi, huwezi kufikiria sawa sawa, unaona kama huna haki ya kuishi tena, Dunia Yako imesimama, unakuwa na mawazo hasi,, angalau yeye ameweza kujishkilia akasema shida yake ambapo ni hatua katika uponaji wake, wengi hujabeba moyoni maoni Yao na wanajikuta wanafanya maamuzi yasiyo sawa ( kujiua). Kama huna msaada chanya wa kimawazo katika shida za wengine ni busara kukaa kimya.

Mtu ana depression nawewe unamuongezea mawazo hasi
 
Hapa ndo ninapopataka. Kama akili haifikirii sawa sawa, amejuaje ana depression Hadi akaja kuandika JF?! Hebu tuache utani ya kutafuta kiki kwenye mitandao
 
Mkuu pole sana kwa hayo maradhi yako ya mawazo, uoga ulipitiliza, panic attack Nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako upate kupona uguwa pole.
 
Hapa ndo ninapopataka. Kama akili haifikirii sawa sawa, amejuaje ana depression Hadi akaja kuandika JF?! Hebu tuache utani ya kutafuta kiki kwenye mitandao
Kwani umeskia depression ni ukichaa!?. Ukiwa na huzuni unajuaje kuwa unahuzuni!?.
 
Nini kinakusababishia msongo wa mawazo na uoga uliopitiliza? Tafuta chanzo (root cause). Mfano ni kukosa kazi, ni kukosa mke/mpenzi, kufiwa na ndugu/wazazi au nini? Lazima kuna chanzo ambacho unakijua.

Ulikisha jua chanzo ndo tunaweza kukusaidia.

Njia moja wapo ya kukusaidia ni kukutanisha na watu ambao wamepitia mapito yako na wakakaa sawa baadae. Hawa watakupa matumaini.

Binadamu tunaishi kwa matumaini. Kila mtu unaye muona barabarani akiwa happy si kwamba hana shida ila ana matumaini. Ukipoteza matumaini ndo hali kama yako inajitokeza.

Je ni nini kimekupotezea matumaini ya maisha?
 
natamani sana tungekaa pamoja japo tupoge story mbili tatu,....mwaka 2011 nilienda mahali kwa ajili ya kujiua,........lakini leo siwezi kujiua na sitojiua, japo naamini maisha ni upuuzi at all, ila ni vyema kuyaishi in a simple way,...kaza buti ndugu yangu kuna wengi bado tunakuhitaji,....
 
Tafuta CHUMVI YA MAWE kilo 2 hivi ukiipata chota viganja viwili nuizia shida zako kisha itupie kwenye maji ndoo ya lita 10

Koroga hakikisha imeyeyuka yote

kisha OGA hayo maji bila SABUNI

Fanya hilo ZOEZI kutwa mara 3 kwa wiki nzima bila kukoma

Asubuhi, mchana na USIKU SAA SITA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…