Depression inanimaliza, sina muda mrefu wa kuishi

Wee unajua depression ilivyo au kwakua unaiskia tu redioni na Tv ndo unaona anadeka!?.

Ukiwa na depression akili haifanyi kazi, huwezi kufikiria sawa sawa, unaona kama huna haki ya kuishi tena, Dunia Yako imesimama, unakuwa na mawazo hasi,, angalau yeye ameweza kujishkilia akasema shida yake ambapo ni hatua katika uponaji wake, wengi hujabeba moyoni maoni Yao na wanajikuta wanafanya maamuzi yasiyo sawa ( kujiua). Kama huna msaada chanya wa kimawazo katika shida za wengine ni busara kukaa kimya.

Mtu ana depression nawewe unamuongezea mawazo hasi
Kuna watu ni wapumbavu sana mkuu
Wanakera mno
 
Tafuta wataalam ukae nao wakuweke sawa, changamoto tumeumbiwa binadamu
Jambo la kwanza kujua ulimwenguni ni kuwa "changamoto timeumbiwa wanadamu"
Hata ukilimaliza hilo litakuja jingine zito yani maisha yako hivyo ! Pia lolote linalokutokea halijaanza leo lishawatokea watu sana.
Akianzia hapo kidogo itasaidia
 
Mkuu unaweza shangaa ila bado nasoma .. ningekuwa nimemaliza miaka mingi sana ila hii hali ilinichelewesha. Wenzagu karibia wote tayar wameajiriwa na wana maisha yao. Naamini na mimi siku moja nitamaliza pia
Sasa una miaka 27 tu unaangalia maisha ya wenzio. Mm 27 natimiza mwezi wa 3 mwakani na hapa nilipo sina kazi wala geto, hata sufuria sina na nina background ya kusota sana kitaa. Lakini naona ni kawaida tu, kila kitu ni rizki shehe. Kuna vitu vingine unavipenda lakini sio rizki yako, fanya kilichopo kwa nafas yako, usilokuwa na uwezo nalo liache liende
 
Hujanielewa mkuu
 
Jambo la kwanza kujua ulimwenguni ni kuwa "changamoto timeumbiwa wanadamu"
Hata ukilimaliza hilo litakuja jingine zito yani maisha yako hivyo ! Pia lolote linalokutokea halijaanza leo lishawatokea watu sana.
Akianzia hapo kidogo itasaidia
Ahsante sana mkuu.. nimekuelewa sana point yako . Ubarikiwe
 
natamani sana tungekaa pamoja japo tupoge story mbili tatu,....mwaka 2011 nilienda mahali kwa ajili ya kujiua,........lakini leo siwezi kujiua na sitojiua, japo naamini maisha ni upuuzi at all, ila ni vyema kuyaishi in a simple way,...kaza buti ndugu yangu kuna wengi bado tunakuhitaji,....
Mkuu natamani sana kuongea na wewe, naamini experience is a good teacher, nafarijika kuona unaelewa ubawa wa changamoto hii. Ubarikiwe mkuu
 
Kosa kubwa dada yako wa serikalini anafanya ni kukulazimisha Kurudi kusoma. Ilitakiwa akuulize kitu ambacho unaona wewe unaweza kufanya kwa sasa na kikakomboa kiuchumi
 
Mkuu natamani sana kuongea na wewe, naamini experience is a good teacher, nafarijika kuona unaelewa ubawa wa changamoto hii. Ubarikiwe mkuu
naamini yatapita tu ndugu yangu,..... kikubwa angalia wale uwapendao, then angalau ishi kwa ajili yao,......we need you
 
Mapito uliyopitia ni makubwa ila ukilinganisha na mapito niliyopitia mimi yako hayo ni kama 10% tu au pungufu.

Tatizo lako lilianza na too much expectations then matokeo yakaja tofauti lakini pia kutotimiza ndoto zako za kimaisha.

Dawa ya hili tatizo unalo wewe mwenyewe, tafakari Kisha kubali matokeo.
 
Wakuu habarini, samahanini sikuweza kuwa online kwani nilikuwa na maumivu mwili mzima, akili ilikuwa haifanyi kazi. Leo nimepitia jumbe zote, kiukweli nimefarijika sana, sijawah pata faraja mliyonionyesha wana JF , kiukweli nawashukuru sana kwa ushauri wenu. Nimeona jumbe za ushauri nyingi ambazo zimeniinua na kunifanya nijione mwenye thaman. Wengi wameniuliza chanzo ni nini. Naomba leo niongee historia yangu mpaka leo hii.

Nimezaliwa mwaka 1997 nna umri wa miaka 27, nilizaliwa kama mtoto wa pili. Nikiwa mdogo sikumbuki ni miaka mingapi nilimwagikiwa na maji ya moto nikaungua mikononi na miguuni kwa kiasi kikubwa. Hivo makovu yakawa yamebakia hata nilipopona. Unaweza jiuliza hayo makovu yanahusiana nini.

Nitaeleza:

Nilipofika umri wa kuanza shule nikiwa darasa la tatu wenzangu walikuwa wananiogopa kutokana na makovu yalivokuwa makubwa mwilini.. hivo hata kunitenga kwenye dawati, nakumbuka nilikuwa navaa soksi ndefu na muda wote sweta lilikuwa halitoki mwilini. Niliendelea ivyo ikafika kipind mpka namaliza shule ya msingi naingia sekondari hali ya kutengwa ndio ikazid zaid, watu walikuwa wananisema wazi wazi. Nakumbuka siku ya juma tatu na alhamis tulikuwa hatuvai masweta siku nzima ivo wengi waliona hiyo shida, hata ukipishana kauli na mtu anatumia ule udhaifu kukutukana.

Katika familia yetu tumezaliwa watoto watatu, baba yangu na mama yangu walitengana kwa kipindi kirefu sana, tokea nikiwa mdogo nimekuwa nikishuhudia ugomvi mkubwa . Vikao vya ndugu wakitaka mama yangu aondoke kwani ndugu walikuwa hawamtaki na sababu sikuweza kuielewa, nilishuhudia mama angu akitukanwa na ndugu wa upande wa baba, alinyang'anywa duka la nguo ambalo ndio lililokuwa likitupa mahitaji ya kila siku na kutusomesha, nakumbuka mzee wangu alienda kuoa mke mwingine, wakati huo nikiwa darasa la sita, huku tukawa na maisha magumu mno. Kumbe pia mzee alikopa deni kubwa sana benki ivo tukauziwa ile nyumba na benki ya nmb, kibaya zaid baada ya kutimuliwa kuna msamalia mwema alikuwa jirani yetu akatupa nyumba ilikuwa haijamaliziwa ili tuishi kwa muda wakati tunajipanga, kiukwel tuliishi maisha magumu sana, hata ela ya mboga ilikuwa ngumu kupata, mama akawa anaenda kufanya vibarua ndo tupate sare.

Nakumbuka mzee alilowea huko mda mrefu sana ila siku moja alirud na akaomba msamaha Tulimpokea na alikiri nakumbuka kipind icho nilikuwa kidato cha sita, baada ya hapo mzee alipata kibarua kwenye kampuni na mama akafungua biashara ya nguo za shule kiukwel maisha yalibadilika tena tukajikuta tunajenga nyumba yetu nzuri. Na furaha ikarejea kwenye familia lakini wanasema siku zote mbuzi wa maskini hazai na hapo ndipo mikasa mingine ikaja kwa kasi.

Nakumbuka nilikuwa nimemaliza kidato cha sita, nimerudi nyumbani. Mwezi wa kumi mwaka 2019 nilianza chuo katika kozi ya clinical medicine ngazi ya diploma, nakumbuka niliingia chuoni nikiwa sijalipa ada na kilikuwa chuo cha private walinipa muda kabla ya mtihani wa semester ya kwanza niwe nimelipa . Nakumbuka nilirud nyumbani kufuatilia suala la ada nikiwa nyumbani walikuja askari kanzu, hawakuwa na sare walipiga hodi nikawafungulia walipofika tu waliuliza tumemkuta baba yako. Niliwajibu ndio nikidhani ni wageni tu.. nakumbuka mzee alipotoka tu walimchukua wakamfunga pingu wakaondoka nae, kumbe kwenye kampuni aliyokuwa anafanyia yeye na wenzake wameiba pesa ndefu. Na ilitakiwa kulipwa basi mimi na mama tulipambana kutafuta hela hata kwa kukopa ili kumtolea mzee dhamana ila ikashindikana. Na tukapewa siku chache bila ivo mali zote za mzee zinataifishwa.

Tulipambana sana aise hatukufanikiwa na nakumbuka mimi ndo nilikuwa mtoto pekee wa kiume, hivo ilibidi niache chuo nianze kupambana . Nyumba iliuzwa kwa mara nyingine tukarudi maisha ya kupanga, mzee ilimchukuw miez kadhaa ndio akaja kuachiwa na kazi akafutwa, kiukweli nilimchukia mzee, niliona bora hata asingerud kile kipind ametitelekeza maana tulirud kuishi maisha magumu zaid ya yale ya mwanzo.. kila kona mama angu alikuwa na madeni, ndugu walikuwa wakituona kama najiandaa nikawasalimie maeneo wanauofanyia kaz unaona kabisa wanakuangalia kwa jicho kali la hasira, nilianza kupambana kuuza sabuni. Nilikuwa natembeza sabuni mitaani.. ili angalau familia yetu tupate chochote kitu.

Kipindi chote hicho kodi tulikuwa hatulipi kwa wakat ivo mwenye nyumba alikuwa anakuja kututukana na kututishia kutufukuza. Kiukweli mzee nae aliugua sana sana, aliugua presha ambayo ilibaki kidogo tumpoteze, nakumbuka tulikopa ela nyingi mama akampeleka ikondo ndipo akapata naafuu.. maana aliumwa karibia mwaka mzima, kiukwel baada ya hapo niliaamua kurud chuo . Japo bado tulikuwa kwenye nyumba ya kupanga ila mama yangu alikuwa analia kila siku ananitaka nirud chuo akidai atafanya kila liwezekanalo tulipe ada kidogo kidogo .

Nilirud tena nikaanza upya, baada ya kumaliza mwaka wa kwanza walikuja watu wa nacte na kusema hiki chuo hakijasajiliwa na kikafungiwa, pale nilihisi nakufa, niliona mimi sio mwenye bahati kwenye hii dunia, nilirud nyumbani nikiwa naumwa maana nilipata mshtuko mkubwa, nilipofika nyumbani nilikuta maisha ni magumu mno tunadaiwa kodi ya miez sita na kumbe ile ela ya kod waliona wasilipe wawe wananiongezea kwenye ada, kiukwel na hiyo ilikuwa mwaka 2019 na hapo ndio tatizo hili lilipoanza, kwanza niliuza simu niliyokuwa nayo nikaaga nyumbani ili nikaende kwa ndugu yangu nikajifunze gereji angalau niwe na fani. Kufika huko nikaona siku zinaenda na bado kiasi sijapata cha kulipia. Nikajikuta nimejiunga kwenye makundi ya ulevi. Nikawa nakunywa pombe sana , na sio mimi niliyekuwa nanunua ni vile unaenda na washkaji angalau nikinywa nasahau shida kwa muda, kumbe ndo nikawa naongeza tatizo. Nilichakaa mno.

Bahati nzuri dada yangu alipata ajira serikalini ivo akakopa ela benk akawanunulia wazaz nyumba ya kuishi . Na pia akaniomba nirudi chuo atanisomesha, lakin nikawa najishangaa nikawa sina morali ya kusoma tena, yan nikawa ni kama mfu nnayetembea, nilikuwa naupenda sana udaktar ila nikawa nimepoteza ile energy ya kutaka kusoma , nikawa mtu wa kujifungia ndani.

Dada yangu aliniita akakaa na mimi kwa masaa mengi kunishauri nirudi kusoma, nikakubali ila ile mood ikawa haipo kabisa, nakumbuka alinipambania nikapata chuo cha serikali cha afya nikaanza tena mwaka wa kwanza . Lakin nilikuwa mtu mwenye hofu sana .. yan nilikuwa siwez kumuangalia mtu usoni.. nilikuwa nikitembea nasikia sauti nyingi kichwani zinaniambia mimi siwez, wakati wangu wa kuishi duniani umeisha, mimi sifai, mimi nachukiwa na ndugu wote, na kweli nikiangalia ilikuwa nikienda kusalimia kwa ndugu wananiogopa sana. Mpaka nikahisi ninatisha. Nilikuwa nasoma kwa shida sana kwan akili yangu kuna muda ilikuwa haifanyi kazi.

Nilipomaliza mwaka wa kwanza nilihairisha masomo niliandika barua ndipo nikaenda hospital pale mount meru Arusha na ndipo nilipoambiwa nina hii shida. Na nilipewa dawa hizo lakini sikutumia muda mrefu sana. Kwan zilikuwa zinanipa side effect nying sana.

Mwaka huu 2024 mwezi wa 10 nilirud chuoni kuendelea na mwaka wa pili baada ya kuahirisha miaka miwili, lakini nimerud akili yangu haifanyi kazi, nikiwa darasani nakuwa sipo huru . Ninaosoma nao ni wadogo sana kiumri na pia mimi nina mwili mkubwa sana, na wananiogopa, kuna muda najilaumu nashindwa kusoma, nakosa usingiz, nakosa hamu ya kula, muda huu ninaoandika nimelala na sina nguvu. Nawaza nitamaliza chuo kweli kwan akili yangu haifanyi kazi.. nasoma sielewi. Nina miaka 27 kwa sasa.

Msaada ninaouomba, ninaomba mnisaidie je ni dawa gani nitumie ambayo itamaliza hii hali maana sioni future yangu mbele yaan hadi mdogo angu anaenifuata ameshanipita kielimu.. naona sisogei ni kama maisha yangu yamewekewa mipaka.

Msaada mwingine naomba nipate rafiki ambae atakuwa mshauri wangu na pia atakuwa mentor wangu katika maisha .

Kuna wakati natamani nipelekwe hospital ya taifa ya mirembe, kwani naona ntakutana na watu wa jamii yangu maana huku duniani sieleweki, naitwa kila majina, kuna muda nakutana na watu wananicheka.

Pia hiyo ni summary tu ya maisha niliyoyapitia siwez kuandika yote maana ni mengi sana.

Mwisho nawaahidi sitowaza jambo la kujitoa uhai japo mawazo hayo yanakuja ila napambana nayo sana.

Nawashukuru sana sana madaktari na washauri kwa kunishauri .. wote mliochukua nafasi ya kunishauri kiukweli nimefarijika sana sana.

Mimi sio mjuzi sana wa kutumia jamii forum ila nashukuruni sana wanafamilia, nimefarijika sana😭
Pole sana kwa mapito unayopitia,ila ipo sababu ya wewe kuwa hai mpaka sasa.
 
Tangu 2019 mpaka sasa nasumbuka na msongo mkali wa mawazo, uoga ulipitiliza, panic attack, yaani nimekuwa kama mfu anaetembea, nilienda hospitali ya Mount Meru Arusha wakaniambia ni psychosis, wakanipa Haloperidol na Benzylhexol nikaanza kutumia ila zilinisaidia kwa wiki chache baada ya hapo hali ikawa mbaya zaidi ya mwanzo na nikawa nikitumia kichwa kinakuwa chepesi kupita kiasi kama nimelewa.

Nikaamua kuacha zile dawa kwa sasa naona sina muda mrefu wa kuishi, imechoka sana
Nenda kanisan af jichetue chezaa sanaa ..mda wa kusalii fumba macho Sali Kwa bidii ukitoka utanambia ...
 
Tujitahidi kuwaambia wengine namna ya Kutumia ni nzuri sana
Nakazia .. interact chochote kizur share na wenzio ..Kwa mfano umepata fedha extra jitahid kutumia na wenzako... Hii ni njia ya kutengeneza furaha na aman ya ndanii
 
MUNGU AKUTIE NGUVU AKUPE AMAN AKUPE KUJIAMINI, AKUPE KUKUBALIKA, KUDHAMINIKA , TTUNAPOINGIA MWAKA 2025 UKAWE WA TOFAUTI KWAKO

KAMA HAUSALI JITAHIDI UANZE KUSALI ITAKUSAIDIA NIMEPITA KWENYE HALI HIYO NAELEWA NINI MAANA YA MSONGO WA MAWAZO LKN NASHUKURU MUNGU NIKO NAPAMBANA HAKUNA LINALOSHINDIKANA KWA MUNGU ANZA KUSALI
 
Tangu 2019 mpaka sasa nasumbuka na msongo mkali wa mawazo, uoga ulipitiliza, panic attack, yaani nimekuwa kama mfu anaetembea, nilienda hospitali ya Mount Meru Arusha wakaniambia ni psychosis, wakanipa Haloperidol na Benzylhexol nikaanza kutumia ila zilinisaidia kwa wiki chache baada ya hapo hali ikawa mbaya zaidi ya mwanzo na nikawa nikitumia kichwa kinakuwa chepesi kupita kiasi kama nimelewa.

Nikaamua kuacha zile dawa kwa sasa naona sina muda mrefu wa kuishi, imechoka sana
Njoo kwa Yesu utapona Bwana Yesu anasema njoni kwangu ninyi nyote na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha mkaribishe Yesu aje aishi ndani yako hiyo hali utaiona tena
 
Back
Top Bottom