Depression inanimaliza, sina muda mrefu wa kuishi

Depression inanimaliza, sina muda mrefu wa kuishi

Tangu 2019 umejishikilia mpaka leo hii ni hatua kubwa.

Kwenda hospitali ilikua step nzuri, kuamua kushare hapa ni step nzuri nyingine.

Umejitahidi kwa uwezo wako wote tafadhali ruhusu mtu mwingine akusaidie kubeba huu mzigo.

Kwenye huu uzi nimeona MD nimeona mtu yupo tayari kugharamia kuwaona wataalamu. Hawa ndiyo watu wameamua kusaidia kuubeba huu mzigo.

Please give them the chance.
Ningekuwa nimejiondoa muda mrefu sana mkuu. Nilifanya suicidal attempt tatu lakin nashukuru Mungu aliyeniokoa katika zote izo mkuu
 
Pole sana ndugu yetu, hii hali uisikie tu kwa wenzako, naamini hapa utaipata msaada na usipuuzie kabisa.
Katika pita pita zako za maisha lazima kuna mambo umeyapitia na ndio chanzo, Kuna kushindwa kwa baadhi ya mambo na unashindwa kukubaliana na hiyo hali.
Kwanza kubaliana na kila badiliko au anguko la vitu ambavyo hukutarajia kukutokea, kumbuka hata unaowataminia au unachokitamani kiwe kilishawahi kupitia magumu.
Jichanganye na watu wennye maono na fanya Ibadan sana kwa imani yako.
Mwisho ukiweza badilisha mazingira, hama mji ukutane na watu wapya.
 
Tangu 2019 mpaka sasa nasumbuka na msongo mkali wa mawazo, uoga ulipitiliza, panic attack, yaani nimekuwa kama mfu anaetembea, nilienda hospitali ya Mount Meru Arusha wakaniambia ni psychosis, wakanipa Haloperidol na Benzylhexol nikaanza kutumia ila zilinisaidia kwa wiki chache baada ya hapo hali ikawa mbaya zaidi ya mwanzo na nikawa nikitumia kichwa kinakuwa chepesi kupita kiasi kama nimelewa.

Nikaamua kuacha zile dawa kwa sasa naona sina muda mrefu wa kuishi, imechoka sana

Haujasema shida yako! Tatizo lako ni nini? Linalosababisha hayo mawazo na stress?
 
Kwanza Unafaida Gani kwenye Jamii inakuzunguka na Taifa Kwa ujumla, tuanzie hapa, yaani wewe ni Mwalimu, Daktari, Nesi, Askali, Mkulima, Mfanyabishara, je una familia? Tuambie fani yako na inatumikaje kunufaisha Jamii. Bila hivyo kama wewe ni reject, yaani kibaka, mvuta bange, mla rushwa, jambazi, muuza unga au mla sembe, tukutakie punziko la mapema. Si vyema kutoa ushauri Kwa mtu alijikataaa mwenyewe.
 
Tangu 2019 mpaka sasa nasumbuka na msongo mkali wa mawazo, uoga ulipitiliza, panic attack, yaani nimekuwa kama mfu anaetembea, nilienda hospitali ya Mount Meru Arusha wakaniambia ni psychosis, wakanipa Haloperidol na Benzylhexol nikaanza kutumia ila zilinisaidia kwa wiki chache baada ya hapo hali ikawa mbaya zaidi ya mwanzo na nikawa nikitumia kichwa kinakuwa chepesi kupita kiasi kama nimelewa.

Nikaamua kuacha zile dawa kwa sasa naona sina muda mrefu wa kuishi, imechoka sana
Join kwenye gym yoyote iliyo karibu na ww itabadilisha uwezo wako wa kufikiria

Jikamue asubuhi na jioni

Huna kazi nenda gym
Umeachwa nenda gym
Unatatizo financially nenda gym

Akili imara huanza na mwili imara dawa sio solution la tatizo lako mindset na perspective ndio shida kwako switch the bend
 
Mkuu natamani sana baada ya Ujumbe huu uliouandika nenda kahudhurie Msiba mmoja tu na uage sura ya mwisho. Itakusaidia kujua Mwanadamu akishalala haamki tena. Tuwapiganie wenzetu wakiwa hai kabla hawajapoteza hamu ya kuishi. Haikupunguzii chochote kumtamkia mema huyu Jamaa.
 
Wakuu habarini, samahanini sikuweza kuwa online kwani nilikuwa na maumivu mwili mzima, akili ilikuwa haifanyi kazi. Leo nimepitia jumbe zote, kiukweli nimefarijika sana, sijawah pata faraja mliyonionyesha wana JF , kiukweli nawashukuru sana kwa ushauri wenu. Nimeona jumbe za ushauri nyingi ambazo zimeniinua na kunifanya nijione mwenye thaman. Wengi wameniuliza chanzo ni nini. Naomba leo niongee historia yangu mpaka leo hii.

Nimezaliwa mwaka 1997 nna umri wa miaka 27, nilizaliwa kama mtoto wa pili. Nikiwa mdogo sikumbuki ni miaka mingapi nilimwagikiwa na maji ya moto nikaungua mikononi na miguuni kwa kiasi kikubwa. Hivo makovu yakawa yamebakia hata nilipopona. Unaweza jiuliza hayo makovu yanahusiana nini.

Nitaeleza:

Nilipofika umri wa kuanza shule nikiwa darasa la tatu wenzangu walikuwa wananiogopa kutokana na makovu yalivokuwa makubwa mwilini.. hivo hata kunitenga kwenye dawati, nakumbuka nilikuwa navaa soksi ndefu na muda wote sweta lilikuwa halitoki mwilini. Niliendelea ivyo ikafika kipind mpka namaliza shule ya msingi naingia sekondari hali ya kutengwa ndio ikazid zaid, watu walikuwa wananisema wazi wazi. Nakumbuka siku ya juma tatu na alhamis tulikuwa hatuvai masweta siku nzima ivo wengi waliona hiyo shida, hata ukipishana kauli na mtu anatumia ule udhaifu kukutukana.

Katika familia yetu tumezaliwa watoto watatu, baba yangu na mama yangu walitengana kwa kipindi kirefu sana, tokea nikiwa mdogo nimekuwa nikishuhudia ugomvi mkubwa . Vikao vya ndugu wakitaka mama yangu aondoke kwani ndugu walikuwa hawamtaki na sababu sikuweza kuielewa, nilishuhudia mama angu akitukanwa na ndugu wa upande wa baba, alinyang'anywa duka la nguo ambalo ndio lililokuwa likitupa mahitaji ya kila siku na kutusomesha, nakumbuka mzee wangu alienda kuoa mke mwingine, wakati huo nikiwa darasa la sita, huku tukawa na maisha magumu mno. Kumbe pia mzee alikopa deni kubwa sana benki ivo tukauziwa ile nyumba na benki ya nmb, kibaya zaid baada ya kutimuliwa kuna msamalia mwema alikuwa jirani yetu akatupa nyumba ilikuwa haijamaliziwa ili tuishi kwa muda wakati tunajipanga, kiukwel tuliishi maisha magumu sana, hata ela ya mboga ilikuwa ngumu kupata, mama akawa anaenda kufanya vibarua ndo tupate sare.

Nakumbuka mzee alilowea huko mda mrefu sana ila siku moja alirud na akaomba msamaha Tulimpokea na alikiri nakumbuka kipind icho nilikuwa kidato cha sita, baada ya hapo mzee alipata kibarua kwenye kampuni na mama akafungua biashara ya nguo za shule kiukwel maisha yalibadilika tena tukajikuta tunajenga nyumba yetu nzuri. Na furaha ikarejea kwenye familia lakini wanasema siku zote mbuzi wa maskini hazai na hapo ndipo mikasa mingine ikaja kwa kasi.

Nakumbuka nilikuwa nimemaliza kidato cha sita, nimerudi nyumbani. Mwezi wa kumi mwaka 2019 nilianza chuo katika kozi ya clinical medicine ngazi ya diploma, nakumbuka niliingia chuoni nikiwa sijalipa ada na kilikuwa chuo cha private walinipa muda kabla ya mtihani wa semester ya kwanza niwe nimelipa . Nakumbuka nilirud nyumbani kufuatilia suala la ada nikiwa nyumbani walikuja askari kanzu, hawakuwa na sare walipiga hodi nikawafungulia walipofika tu waliuliza tumemkuta baba yako. Niliwajibu ndio nikidhani ni wageni tu.. nakumbuka mzee alipotoka tu walimchukua wakamfunga pingu wakaondoka nae, kumbe kwenye kampuni aliyokuwa anafanyia yeye na wenzake wameiba pesa ndefu. Na ilitakiwa kulipwa basi mimi na mama tulipambana kutafuta hela hata kwa kukopa ili kumtolea mzee dhamana ila ikashindikana. Na tukapewa siku chache bila ivo mali zote za mzee zinataifishwa.

Tulipambana sana aise hatukufanikiwa na nakumbuka mimi ndo nilikuwa mtoto pekee wa kiume, hivo ilibidi niache chuo nianze kupambana . Nyumba iliuzwa kwa mara nyingine tukarudi maisha ya kupanga, mzee ilimchukuw miez kadhaa ndio akaja kuachiwa na kazi akafutwa, kiukweli nilimchukia mzee, niliona bora hata asingerud kile kipind ametitelekeza maana tulirud kuishi maisha magumu zaid ya yale ya mwanzo.. kila kona mama angu alikuwa na madeni, ndugu walikuwa wakituona kama najiandaa nikawasalimie maeneo wanauofanyia kaz unaona kabisa wanakuangalia kwa jicho kali la hasira, nilianza kupambana kuuza sabuni. Nilikuwa natembeza sabuni mitaani.. ili angalau familia yetu tupate chochote kitu.

Kipindi chote hicho kodi tulikuwa hatulipi kwa wakat ivo mwenye nyumba alikuwa anakuja kututukana na kututishia kutufukuza. Kiukweli mzee nae aliugua sana sana, aliugua presha ambayo ilibaki kidogo tumpoteze, nakumbuka tulikopa ela nyingi mama akampeleka ikondo ndipo akapata naafuu.. maana aliumwa karibia mwaka mzima, kiukwel baada ya hapo niliaamua kurud chuo . Japo bado tulikuwa kwenye nyumba ya kupanga ila mama yangu alikuwa analia kila siku ananitaka nirud chuo akidai atafanya kila liwezekanalo tulipe ada kidogo kidogo .

Nilirud tena nikaanza upya, baada ya kumaliza mwaka wa kwanza walikuja watu wa nacte na kusema hiki chuo hakijasajiliwa na kikafungiwa, pale nilihisi nakufa, niliona mimi sio mwenye bahati kwenye hii dunia, nilirud nyumbani nikiwa naumwa maana nilipata mshtuko mkubwa, nilipofika nyumbani nilikuta maisha ni magumu mno tunadaiwa kodi ya miez sita na kumbe ile ela ya kod waliona wasilipe wawe wananiongezea kwenye ada, kiukwel na hiyo ilikuwa mwaka 2019 na hapo ndio tatizo hili lilipoanza, kwanza niliuza simu niliyokuwa nayo nikaaga nyumbani ili nikaende kwa ndugu yangu nikajifunze gereji angalau niwe na fani. Kufika huko nikaona siku zinaenda na bado kiasi sijapata cha kulipia. Nikajikuta nimejiunga kwenye makundi ya ulevi. Nikawa nakunywa pombe sana , na sio mimi niliyekuwa nanunua ni vile unaenda na washkaji angalau nikinywa nasahau shida kwa muda, kumbe ndo nikawa naongeza tatizo. Nilichakaa mno.

Bahati nzuri dada yangu alipata ajira serikalini ivo akakopa ela benk akawanunulia wazaz nyumba ya kuishi . Na pia akaniomba nirudi chuo atanisomesha, lakin nikawa najishangaa nikawa sina morali ya kusoma tena, yan nikawa ni kama mfu nnayetembea, nilikuwa naupenda sana udaktar ila nikawa nimepoteza ile energy ya kutaka kusoma , nikawa mtu wa kujifungia ndani.

Dada yangu aliniita akakaa na mimi kwa masaa mengi kunishauri nirudi kusoma, nikakubali ila ile mood ikawa haipo kabisa, nakumbuka alinipambania nikapata chuo cha serikali cha afya nikaanza tena mwaka wa kwanza . Lakin nilikuwa mtu mwenye hofu sana .. yan nilikuwa siwez kumuangalia mtu usoni.. nilikuwa nikitembea nasikia sauti nyingi kichwani zinaniambia mimi siwez, wakati wangu wa kuishi duniani umeisha, mimi sifai, mimi nachukiwa na ndugu wote, na kweli nikiangalia ilikuwa nikienda kusalimia kwa ndugu wananiogopa sana. Mpaka nikahisi ninatisha. Nilikuwa nasoma kwa shida sana kwan akili yangu kuna muda ilikuwa haifanyi kazi.

Nilipomaliza mwaka wa kwanza nilihairisha masomo niliandika barua ndipo nikaenda hospital pale mount meru Arusha na ndipo nilipoambiwa nina hii shida. Na nilipewa dawa hizo lakini sikutumia muda mrefu sana. Kwan zilikuwa zinanipa side effect nying sana.

Mwaka huu 2024 mwezi wa 10 nilirud chuoni kuendelea na mwaka wa pili baada ya kuahirisha miaka miwili, lakini nimerud akili yangu haifanyi kazi, nikiwa darasani nakuwa sipo huru . Ninaosoma nao ni wadogo sana kiumri na pia mimi nina mwili mkubwa sana, na wananiogopa, kuna muda najilaumu nashindwa kusoma, nakosa usingiz, nakosa hamu ya kula, muda huu ninaoandika nimelala na sina nguvu. Nawaza nitamaliza chuo kweli kwan akili yangu haifanyi kazi.. nasoma sielewi. Nina miaka 27 kwa sasa.

Msaada ninaouomba, ninaomba mnisaidie je ni dawa gani nitumie ambayo itamaliza hii hali maana sioni future yangu mbele yaan hadi mdogo angu anaenifuata ameshanipita kielimu.. naona sisogei ni kama maisha yangu yamewekewa mipaka.

Msaada mwingine naomba nipate rafiki ambae atakuwa mshauri wangu na pia atakuwa mentor wangu katika maisha .

Kuna wakati natamani nipelekwe hospital ya taifa ya mirembe, kwani naona ntakutana na watu wa jamii yangu maana huku duniani sieleweki, naitwa kila majina, kuna muda nakutana na watu wananicheka.

Pia hiyo ni summary tu ya maisha niliyoyapitia siwez kuandika yote maana ni mengi sana.

Mwisho nawaahidi sitowaza jambo la kujitoa uhai japo mawazo hayo yanakuja ila napambana nayo sana.

Nawashukuru sana sana madaktari na washauri kwa kunishauri .. wote mliochukua nafasi ya kunishauri kiukweli nimefarijika sana sana.

Mimi sio mjuzi sana wa kutumia jamii forum ila nashukuruni sana wanafamilia, nimefarijika sana😭
Hongera sana Mkuu kwa kutokata Tamaa na kurejesha hamu ya kuishi! Vijana wenzio tunakuahidi kusimama nawe urejeshe kila kilocholiwa na Nzige katika Maisha yako. Mungu akujalie usimame tena na kutimiza Ndoto yako katika sekta ya Afya. Hakika utakuwa Mtaalamu Bora wa Afya kwa kuwa umepitia Maisha hayo. Naomba kufahamu uko Mkoa gani kila inapotokea nakuja Mkoa huo nifike kukutembelea walau kushare nawe kidogo Mungu anachotubariki kwenye utafutaji.
 
Ulitakiwa upate na folic acid na wangekuongezea muda wa kulala kwa amytriptiline. Hapo pia, ungepata na sehem ya kupoa na kusocialize na watu wazuri wanaofariji na kukufanya kua active hasa kiuchumi na kijamii kwenye michezo, burudani, mipira.

Unafanya kazi gani?
 
Tangu 2019 mpaka sasa nasumbuka na msongo mkali wa mawazo, uoga ulipitiliza, panic attack, yaani nimekuwa kama mfu anaetembea, nilienda hospitali ya Mount Meru Arusha wakaniambia ni psychosis, wakanipa Haloperidol na Benzylhexol nikaanza kutumia ila zilinisaidia kwa wiki chache baada ya hapo hali ikawa mbaya zaidi ya mwanzo na nikawa nikitumia kichwa kinakuwa chepesi kupita kiasi kama nimelewa.

Nikaamua kuacha zile dawa kwa sasa naona sina muda mrefu wa kuishi, imechoka sana
Una kazi au shughuli ya kukuingizia kipato. Depression sio ugojwa ni dalili za tatizo au matatizo yaliyo shindikana kutatuliwa. Kutibu dalili bila kujuwa chanzo cha tatizo hakuwezi kuponya tatizo. Swali la kujiuliza nini chanza cha depression. Mfano chanzo kinaweza kuwa kutoridhika hali yako ya maisha . Hali ya maisha mara nyingi inahusisha vitu vingi ikiwemo aina ya kazi, biashara, au shughuli inayo kuwezesha kupata kipato. Pia inahusisha mahusiano ya familia na jamii inayo kuzunguka. Hivyo ni baadhi ya maeneo ambayo unahitaji kushughulikia kabla ya kutumia dawa.
 
Pole sana Mkuu, Mungu asikuache na usiache pia kufatilia Kuna member wawili hapo mwanzo wapo tayari kukusaidia.
 
Hongera sana Mkuu kwa kutokata Tamaa na kurejesha hamu ya kuishi! Vijana wenzio tunakuahidi kusimama nawe urejeshe kila kilocholiwa na Nzige katika Maisha yako. Mungu akujalie usimame tena na kutimiza Ndoto yako katika sekta ya Afya. Hakika utakuwa Mtaalamu Bora wa Afya kwa kuwa umepitia Maisha hayo. Naomba kufahamu uko Mkoa gani kila inapotokea nakuja Mkoa huo nifike kukutembelea walau kushare nawe kidogo Mungu anachotubariki kwenye utafutaji.
Ahsante sana mkuu.. kiukwel nimefarijika sana kuona kuna watu wanaoelewa hali hii.. binafsi nipo mkoa wa Rukwa nasoma chuo huku. Pia nitakutumia mawasiliano yangu inbox tuzidi kufahamiana mkuu
 
Back
Top Bottom