Tangu 2019 mpaka sasa nasumbuka na msongo mkali wa mawazo, uoga ulipitiliza, panic attack, yaani nimekuwa kama mfu anaetembea, nilienda hospitali ya Mount Meru Arusha wakaniambia ni psychosis, wakanipa Haloperidol na Benzylhexol nikaanza kutumia ila zilinisaidia kwa wiki chache baada ya hapo hali ikawa mbaya zaidi ya mwanzo na nikawa nikitumia kichwa kinakuwa chepesi kupita kiasi kama nimelewa.
Nikaamua kuacha zile dawa kwa sasa naona sina muda mrefu wa kuishi, imechoka sana
Pole sana!
Pili, hongera sana kwa kuamua kushirikisha wengine haya unayoyapitia, ni mwanzo mzuri wa kutatua na kulimaliza tatizo hilo amini hivyo.
Depression ipo na inawatesa wengi. Matibabu yake kamili ni kubaini chanzo chake (kisababishi) na si kutumia dawa tu. Pia mbali na dawa kuna matibabu maalumu ambayo hutolewa na wataalamu wa psychology inaitwa psychotherapy.
Kutibu depression huchukua muda mrefu kidogo, wala siyo wiki au wiki mbili. Unahitaji kuhudhuria clinic au sessions kila mwezi nk
Kwa hiyo pamoja na msaada na ushauri ambao wenzangu wamekupa nami nikushauri pia:
-uweze kubaini chanzo (kisababishi) cha tatizo hili kwako kwani itasaidia sana kujua aina ya ushauri, msaada au tiba ambayo itakufanya uwe sawa.
-usikate tamaa: Kuna vingi unaweza kufanya hata kama kuna mahali pengine ulifeli au ulifanya vibaya.
-epuka kukaa pekeeako/kujitenga-shirikiana vizuri na wote wanaoonesha utayari wa kukusaidia
-rudi kwa madaktari wale waliokuandikia hizo dawa ili uwape mrejesho wa hali yako baada ya kuzitumia hizo dawa
Mwisho, hongera sana kwa kuomba msaada na kushirikisha changamoto hizi unazopitia kwa jamii, naamini kwa msaada na ushauri wa jamii hii utakuwa sawa mkuu.
You're a hero, you're a winner!
Kila la kheri.