Depression inaniua

Depression inaniua

Sasa siwezi hata ongea nikisema neno nalia.
nilishawahi kupita kwenye depression kubwa sana, najua maana ya maumivu ya moyo, hadi yeyote unayekutana naye anakuuliza mbona una stress? lakini baada ya kugeuza macho yangu nikamtazama Yesu Kristo, nilipata amani ya ajabu isiyo na kipimo. nikaamini kumbe Isaya alipotabiri kwamba Yesu atakuwa mfalme wa amani, wayahudi walidhani atakuwa mfalme wa kuishi ikulu, kumbe anao uwezo kukupatia amani moyoni, amani ipitayo akili zote.

pamoja na depression ukimpa Yesu maisha yake anaweza kukupatia furaha na amani ya ajabu hadi ukasahau. pesa haziwezi kukupatia amani kama hiyo, wapenzi au cheo au chochote hakiwezi, ila yeye anakupa amani na furaha bure bila gharama. ni amani ambayo mtu hata kama hana pesa moyoni amejaa furaha na amani, inapita akili zote.

ISAYA 9:6 INASEMA; Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa Jina lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.

Yesu Kristo ni Mfalme wa amani, ukimpa maisha yako, atakupa amani ipitayo akili zote, depression itafutika, stress na vyote vitafutika.
 
"The bravest thing I ever did was continuing my Life when I wanted to die.

Depression ipo asiwaambie mtu ila nakuomba bibie kama una kazi na uko mbali na familia please chukua likizo nenda nyumbani kapumzike na usiliongelee kabisa tatizo bali jichanganye nao na taratibu utaona imepungua kwa kiasi kikubwa

Huu ugonjwa unakufanya haya usioge na kubadili nguo na pia unawaza hata kujitoa uhai ila ukipambana yataisha

Jaribu kupuuza hicho chanzo cha matatizo haya hata kama ni mpenzi wako muone kama kafa
 
Sasa siwezi hata ongea nikisema neno nalia.
Duniani sio sehemu salama kwa watu walegevu walegevu…utalia sana…
Fanya maamuzi acha kulia inaku pambana na changamoto hiyo ,washirikishe watu usitake wakuonee huruma bali wakusaidie kulitatua tatizo lako!

Acha kulia kwani kulia kwako hakutoondoa tatizo!
 
Back
Top Bottom