Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
nilishawahi kupita kwenye depression kubwa sana, najua maana ya maumivu ya moyo, hadi yeyote unayekutana naye anakuuliza mbona una stress? lakini baada ya kugeuza macho yangu nikamtazama Yesu Kristo, nilipata amani ya ajabu isiyo na kipimo. nikaamini kumbe Isaya alipotabiri kwamba Yesu atakuwa mfalme wa amani, wayahudi walidhani atakuwa mfalme wa kuishi ikulu, kumbe anao uwezo kukupatia amani moyoni, amani ipitayo akili zote.Sasa siwezi hata ongea nikisema neno nalia.
pamoja na depression ukimpa Yesu maisha yake anaweza kukupatia furaha na amani ya ajabu hadi ukasahau. pesa haziwezi kukupatia amani kama hiyo, wapenzi au cheo au chochote hakiwezi, ila yeye anakupa amani na furaha bure bila gharama. ni amani ambayo mtu hata kama hana pesa moyoni amejaa furaha na amani, inapita akili zote.
ISAYA 9:6 INASEMA; Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa Jina lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
Yesu Kristo ni Mfalme wa amani, ukimpa maisha yako, atakupa amani ipitayo akili zote, depression itafutika, stress na vyote vitafutika.