Dereva Adam Idd: Leseni ikichukuliwa, ukienda kwa RTO unaombwa utoe Shilingi 500,000 ili leseni yako isifungiwe

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wakati madereva kutoka Stendi ya Magufuli wakitoa kero zao mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, wameeleza malalamiko yao kuhusu askari kuwakamata mara kwa mara bila kufuata taratibu za kisheria, pamoja na kuchukuliwa leseni zao.

Moja ya dereva Adam Idd ameeleza kama ifuatavyo

  • Mfumo wa Pointi za Leseni: "Wao wanaanzisha sheria alafu wanatuhukumu sisi bila sheria kupitishwa na serikali. Kwa mfano sheria za pointi wameweka pointi 15... ukitoka hapa mpaka Kigoma kwa siku tatu leseni itakuwa imeisha."
  • Makosa ya Overtaking na Mistari: "Mistari unapokuwa unaovertake kama dereva unaweza ukaovertake mahali mstari unaruhusu lakini kidogo ukakanyaga mstari ambao hauruhusu... askari anakukamata anakuchukua leseni anakwambia hii leseni nenda kwa RTO..."
  • Shinikizo la Rushwa na RTO: "...ukienda kwa RTO... anakuambia hapa bila 500 bila laki ile mimi nakufungia miezi sita... Posho yangu ya kutoka daa kwenda Kigoma 6000 sasa anataka laki inabidi nikauze shamba langu nimletee laki ili leseni yangu asiifunge."

"...ukienda kwa RTO RTO sasa anakuambia wewe unasemaje sasa kwa sababu wewe hutakiwi kufungiwa leseni unabidi uanze kumbembeleza yule RTO bwana RTO unanisaidiaje anakuambia hapa bila 500 bila laki ile Mimi nakufungia miezi sita."

​
 
Kuna basi Nilikuwa Nimepanda yaani dereva alifanya makosa matatu na mawili yanafanana kabisa
Alikuwa ana overtake kwenye kona na mbele haoni kitu huku kuna mistari kabisa isiyomruhusu ku overtake na alirudia kosa la hivyo mara mbili

Sasa mtu kama huyo amebeba watu zaidi ya 50 si hatari?
Akikutana na lorry atakwepaje?
Madereva wengine wana matatizo na sheria hawazifuati kabisa
Na ndio sababu wanasababisha Rushwa kila wakati
 
nadhani ukikiuka sheria mara kadhaa,
ni muhimu sana kufungiwa leseni jumla jumla,
ili kuepusha ajali za barabarani za mara kwa mara kutokana na uzembe wa madereva kama hawa :NoGodNo:
 
Kuna basi Nilikuwa Nimepanda yaani dereva alifanya makosa matatu na mawili yanafanana kabisa
Alikuwa ana overtake kwenye kona na mbele haoni kitu huku kuna mistari kabisa isiyomruhusu ku overtake na alirudia kosa la hivyo mara mbili

Sasa mtu kama huyo amebeba watu zaidi ya 50 si hatari?
Akikutana na lorry atakwepaje?
Madereva wengine wana matatizo na sheria hawazifuati kabisa
Na ndio sababu wanasababisha Rushwa kila wakati
Hii ni sahihi kabisa mkuu
 
hivi ni kwa nini mnawapa podium low iq stupid people kama hao? kwa hali ya kawaida haupaswi kuwa na points kwenye leseni yako kama ukifwata sheria za br ambazo ni lazima uzifwate.
hivyo kama ktk dar-kgm unamaliza points basi tafuta kazi nyingine na haukupaswa kuwa dereva to begin with, siyo lazima, kila mtu awe dereva, kuna watu wengi ambao wanaweza kuendesha gari ktk dar-kgm kwa 0 point kwenye leseni na hao ndiyo wanaopaswa kutumia br zetu ...

Unashangaa hawa kupewa podium? Hushangai samuya kuwa rais?
 
Kuna basi Nilikuwa Nimepanda yaani dereva alifanya makosa matatu na mawili yanafanana kabisa
Alikuwa ana overtake kwenye kona na mbele haoni kitu huku kuna mistari kabisa isiyomruhusu ku overtake na alirudia kosa la hivyo mara mbili

Sasa mtu kama huyo amebeba watu zaidi ya 50 si hatari?
Akikutana na lorry atakwepaje?
Madereva wengine wana matatizo na sheria hawazifuati kabisa
Na ndio sababu wanasababisha Rushwa kila wakati
Sawa hilo la point limeeleweka
Sema rushwa rushwa rushwa kwa matrafic ila tunajuwa ni maagizo wanatumwa

Ova
 
Kwa kuwa wamelifanya kama ni moja ya ajira na wanaotoa ni wabaya zaidi

Shida inakuja kama wanatumwa nao kukusanya kwa ajili ya wakubwa ndio mbaya zaidi

Rushwa kuisha ni ndoto za mchana na pia ajali na makosa hayatakwisha
Mtu anaendesha chombo hata kubadili kioo cha mbele hawezi
Jua likiwaka mbele haoni ila alivyo mpumbavu anaona ni sawa tu
Au moshi unatoka utafikiri mashine ya unga
Kuna haja gani ya kuwa na gari kama hata kubadili kitu mtu hawezi
Na hapo ndio anapewa makosa zaidi ya matatu na anatoa hongo anapita
Huko mbele anauwa kwa kosa aliloachiwa na traffic
 
Wakati madereva kutoka Stendi ya Magufuli wakitoa kero zao mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, wameeleza malalamiko yao kuhusu askari kuwakamata mara kwa mara bila kufuata taratibu za kisheria, pamoja na kuchukuliwa leseni zao.

Moja ya dereva Adam Idd ameeleza kama ifuatavyo

  • Mfumo wa Pointi za Leseni: "Wao wanaanzisha sheria alafu wanatuhukumu sisi bila sheria kupitishwa na serikali. Kwa mfano sheria za pointi wameweka pointi 15... ukitoka hapa mpaka Kigoma kwa siku tatu leseni itakuwa imeisha."
  • Makosa ya Overtaking na Mistari: "Mistari unapokuwa unaovertake kama dereva unaweza ukaovertake mahali mstari unaruhusu lakini kidogo ukakanyaga mstari ambao hauruhusu... askari anakukamata anakuchukua leseni anakwambia hii leseni nenda kwa RTO..."
  • Shinikizo la Rushwa na RTO: "...ukienda kwa RTO... anakuambia hapa bila 500 bila laki ile mimi nakufungia miezi sita... Posho yangu ya kutoka daa kwenda Kigoma 6000 sasa anataka laki inabidi nikauze shamba langu nimletee laki ili leseni yangu asiifunge."

"...ukienda kwa RTO RTO sasa anakuambia wewe unasemaje sasa kwa sababu wewe hutakiwi kufungiwa leseni unabidi uanze kumbembeleza yule RTO bwana RTO unanisaidiaje anakuambia hapa bila 500 bila laki ile Mimi nakufungia miezi sita."

Ukiacha uuaji, polisi pia wamebobea kwenye ujambazi, rushwa na kusigina sheria.
 
Kuna basi Nilikuwa Nimepanda yaani dereva alifanya makosa matatu na mawili yanafanana kabisa
Alikuwa ana overtake kwenye kona na mbele haoni kitu huku kuna mistari kabisa isiyomruhusu ku overtake na alirudia kosa la hivyo mara mbili

Sasa mtu kama huyo amebeba watu zaidi ya 50 si hatari?
Akikutana na lorry atakwepaje?
Madereva wengine wana matatizo na sheria hawazifuati kabisa
Na ndio sababu wanasababisha Rushwa kila wakati
Si unawaona hapo kwenu kwa babu walivyo makini.
 
Huku kuna heshima na nidhamu
Kuna camera zaidi 4m
Kila ukipita big brother is watching 👀
Licence yangu haina point kwa miaka 27 sasa
Najichunga sana maana ukifanya kosa na insurance inapanda
Utanyooka tu na rushwa hakuna labda akusamehe tu uende
 
Wakati madereva kutoka Stendi ya Magufuli wakitoa kero zao mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, wameeleza malalamiko yao kuhusu askari kuwakamata mara kwa mara bila kufuata taratibu za kisheria, pamoja na kuchukuliwa leseni zao.

Moja ya dereva Adam Idd ameeleza kama ifuatavyo

  • Mfumo wa Pointi za Leseni: "Wao wanaanzisha sheria alafu wanatuhukumu sisi bila sheria kupitishwa na serikali. Kwa mfano sheria za pointi wameweka pointi 15... ukitoka hapa mpaka Kigoma kwa siku tatu leseni itakuwa imeisha."
  • Makosa ya Overtaking na Mistari: "Mistari unapokuwa unaovertake kama dereva unaweza ukaovertake mahali mstari unaruhusu lakini kidogo ukakanyaga mstari ambao hauruhusu... askari anakukamata anakuchukua leseni anakwambia hii leseni nenda kwa RTO..."
  • Shinikizo la Rushwa na RTO: "...ukienda kwa RTO... anakuambia hapa bila 500 bila laki ile mimi nakufungia miezi sita... Posho yangu ya kutoka daa kwenda Kigoma 6000 sasa anataka laki inabidi nikauze shamba langu nimletee laki ili leseni yangu asiifunge."

"...ukienda kwa RTO RTO sasa anakuambia wewe unasemaje sasa kwa sababu wewe hutakiwi kufungiwa leseni unabidi uanze kumbembeleza yule RTO bwana RTO unanisaidiaje anakuambia hapa bila 500 bila laki ile Mimi nakufungia miezi sita."

Zifungwe kamera ili wahukumiwe kwa haki badala ya macho ya askari wengine wana makengeza
 
Kwani we huku denga unawaona traffic police wa barabarani wanalundikana
Kila eneo?????
Kama nchi fulani

Ova
Hamna huo upuzi. Ila bongo madereva bana. Kwaanzia magari hadi bodaboda. Unakuta gari nyi hata indicators hazina na hawajali.
 
Back
Top Bottom