Dereva Adam Idd: Leseni ikichukuliwa, ukienda kwa RTO unaombwa utoe Shilingi 500,000 ili leseni yako isifungiwe

Dereva Adam Idd: Leseni ikichukuliwa, ukienda kwa RTO unaombwa utoe Shilingi 500,000 ili leseni yako isifungiwe

Hamna huo upuzi. Ila bongo madereva bana. Kwaanzia magari hadi bodaboda. Unakuta gari nyi hata indicators hazina na hawajali.
Mfumo tu wa ovyo wameulea wenyewe,rushwa rushwa
Sema uzuri mabasi mengi na malori yanamilikiwa na vigogo, wanasiasa hili sakata watajuwa wenywe watamalizana nalo vp

Ova
 
hivi ni kwa nini mnawapa podium low iq stupid people kama hao? kwa hali ya kawaida haupaswi kuwa na points kwenye leseni yako kama ukifwata sheria za br ambazo ni lazima uzifwate.
hivyo kama ktk dar-kgm unamaliza points basi tafuta kazi nyingine na haukupaswa kuwa dereva to begin with, siyo lazima, kila mtu awe dereva, kuna watu wengi ambao wanaweza kuendesha gari ktk dar-kgm kwa 0 point kwenye leseni na hao ndiyo wanaopaswa kutumia br zetu ...
Kwa uzoefu wangu madereva ni Ile class ya mwisho mwisho kabisa kwenye vipimo vyote vya IQ

Wana uelewa mdogo Sana ingawa kwakweli wanabeba dhamana kubwa sana ya usafirishaji
 
wamewageuza vitega uchumi
Tena hata makosa ya kubandika mtandaoni ndio balaa, Askari ukimnyim Rushwa Tu anakukomoa vile unaondosha Gari Tu yeye anajaza kwenye mfumo makosa Mawili au matatu kadiri anavyojisikia.

Wewe huna habari unakuja kumbiwa a month later Una deni la makos barabarani na yamesha double penalty😂😂

Ubaya wa hii Kitu huna pakukaa rufaa wala pakulalamika unatakiwa Tu ulipe.

Hii imeweka mazingir madereva wa vyombo wanaogopa sana kila Askari anataka 5000 au 10000 na inabidi utie Tu kwa uchungu
 
Kwa uzoefu wangu madereva ni Ile class ya mwisho mwisho kabisa kwenye vipimo vyote vya IQ

Wana uelewa mdogo Sana ingawa kwakweli wanabeba dhamana kubwa sana ya usafirishaji
Kuna kipindi makampuni (Pepsi) waliajiri madereva wenye degree au advanced diploma ya marketing, ajira ilikuwa ni nafasi ya marketing manager ila sharti uwe na leseni ya udereva. Wasomi wakaingia barabarani kusambaza vinywaji wakiwa mameneja na udereva juu.
 
Hii nzuri
 
Tena hata makosa ya kubandika mtandaoni ndio balaa, Askari ukimnyim Rushwa Tu anakukomoa vile unaondosha Gari Tu yeye anajaza kwenye mfumo makosa Mawili au matatu kadiri anavyojisikia.

Wewe huna habari unakuja kumbiwa a month later Una deni la makos barabarani na yamesha double penalty😂😂

Ubaya wa hii Kitu huna pakukaa rufaa wala pakulalamika unatakiwa Tu ulipe.

Hii imeweka mazingir madereva wa vyombo wanaogopa sana kila Askari anataka 5000 au 10000 na inabidi utie Tu kwa uchungu
Hii ni mbaya sana aise.
 
Asa kwanini wasiombe serikali iwaongezee mishahara kuliko kuzalilika hivi
 
Wakati madereva kutoka Stendi ya Magufuli wakitoa kero zao mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, wameeleza malalamiko yao kuhusu askari kuwakamata mara kwa mara bila kufuata taratibu za kisheria, pamoja na kuchukuliwa leseni zao.

Moja ya dereva Adam Idd ameeleza kama ifuatavyo

  • Mfumo wa Pointi za Leseni: "Wao wanaanzisha sheria alafu wanatuhukumu sisi bila sheria kupitishwa na serikali. Kwa mfano sheria za pointi wameweka pointi 15... ukitoka hapa mpaka Kigoma kwa siku tatu leseni itakuwa imeisha."
  • Makosa ya Overtaking na Mistari: "Mistari unapokuwa unaovertake kama dereva unaweza ukaovertake mahali mstari unaruhusu lakini kidogo ukakanyaga mstari ambao hauruhusu... askari anakukamata anakuchukua leseni anakwambia hii leseni nenda kwa RTO..."
  • Shinikizo la Rushwa na RTO: "...ukienda kwa RTO... anakuambia hapa bila 500 bila laki ile mimi nakufungia miezi sita... Posho yangu ya kutoka daa kwenda Kigoma 6000 sasa anataka laki inabidi nikauze shamba langu nimletee laki ili leseni yangu asiifunge."

"...ukienda kwa RTO RTO sasa anakuambia wewe unasemaje sasa kwa sababu wewe hutakiwi kufungiwa leseni unabidi uanze kumbembeleza yule RTO bwana RTO unanisaidiaje anakuambia hapa bila 500 bila laki ile Mimi nakufungia miezi sita."

huyu hapa, acheni kuleta vipande vipande

View: https://www.youtube.com/watch?v=kN1M3NB3Azo
 
Back
Top Bottom