Dereva wa gari kubwa amelalamikia vikali hatua ya askari wa usalama barabarani kuwakata pointi kwenye leseni zao kutokana na ubovu wa magari ambayo ni ya kampuni. Amesema kuwa adhabu hiyo inawanyima fursa ya kuendelea kufanya kazi na kuhudumia familia zao pale pointi hizo zinapomalizika, huku sekta hiyo ikiwa ndiyo chanzo chao kikuu cha kipato.
Mbali na mfumo huo wa pointi, dereva huyo amekosoa tabia ya askari wa usalama barabarani kujificha vichakani wakiwa na tochi za kupima mwendo badala ya kutoa elimu au kuboresha usalama.
Pia ameainisha ubovu uliokithiri wa barabara katika njia kuu kipande cha kutoka Igawa hadi Tunduma, akisisitiza kuwa mashimo na miundombinu mibovu ndivyo vyanzo vikuu vya ajali badala ya makosa ya madereva pekee.
Amesisitiza kuwekeza kwenye miundombinu bora ya barabara pamoja na mifumo ya kisasa ya kuongoza magari ili kupunguza migongano na chuki isiyo ya lazima kati ya madereva na askari barabarani.
Pia soma:
~Dereva alalamika Askari wa barabarani kuwakatia Point kwenye leseni
~Mfumo wa Pointi Leseni: Usawa Wapi?
~Serikali isirudi nyuma: Mfumo wa kukata pointi kwenye leseni usisistishwe, migomo isitumike kuchezea maisha ya abiria barabarani
~Makosa ya barabarani na point zake zitakazowekwa kwenye leseni. Kila leseni itakuwa na jumla ya pointi 15