Ila hii ya askari kujificha kichakani imekaa kinafiki sanaDereva wa gari kubwa amelalamikia vikali hatua ya askari wa usalama barabarani kuwakata pointi kwenye leseni zao kutokana na ubovu wa magari ambayo ni ya kampuni. Amesema kuwa adhabu hiyo inawanyima fursa ya kuendelea kufanya kazi na kuhudumia familia zao pale pointi hizo zinapomalizika, huku sekta hiyo ikiwa ndiyo chanzo chao kikuu cha kipato.
Mbali na mfumo huo wa pointi, dereva huyo amekosoa tabia ya askari wa usalama barabarani kujificha vichakani wakiwa na tochi za kupima mwendo badala ya kutoa elimu au kuboresha usalama.
Pia ameainisha ubovu uliokithiri wa barabara katika njia kuu kipande cha kutoka Igawa hadi Tunduma, akisisitiza kuwa mashimo na miundombinu mibovu ndivyo vyanzo vikuu vya ajali badala ya makosa ya madereva pekee.
Amesisitiza kuwekeza kwenye miundombinu bora ya barabara pamoja na mifumo ya kisasa ya kuongoza magari ili kupunguza migongano na chuki isiyo ya lazima kati ya madereva na askari barabarani.
Ha ha ha mtu baada ya kutii sheria analialia. Ila la ubovu wa gari ni mtego kwa madereva. Kabla ya point faini ya ubovu wa gari ambao dereva alitoa ripoti kampuni ndio inalipa. Huu utaratibu wa point ina maana dereva agome kuendesha na kampuni itampa dereva mwingine.watanzagiza bhana, siyo kazi ya trafiki kukufundisha sheria na alama za barabarani, ukipata leseni maana yake umefanya mafunzo ya udereva na kufuzu na ndiyo maana ukapata leseni, trafiki kazi yake ni kukagua na kuhakikisha madereva wanafwata sheria za barabarani na siyo kukufundisha tena huo muda hawana na wala siyo kazi yao kama unataka kujua khs sheria za br. rudi shule ya udereva kujifunza upya, khs trafiki kujificha na kamera hili nalo la linashangaza kulalamikiwa, kwani una wasi wasi gani kama akijificha na kamera kama unafwata sheria za bara barani? unapaswa ufwate sheria hata kama ni saa tisa usiku na hakuna mtu kama ni eneo la 50 km/h inapaswa kuwa hivyo.
ni nadra sana trafiki polisi akaonea dereva tanzagiza, madereva wengi wana makosa na hata hawakupaswa kuwa na leseni ...
Unajua dawa yake? Ukifika sehemu kuna kibao cha 50kph tembea 50kph, ukifika eneo haliruhusu kuovateki usiovateki. Hapa hata ajifiche uvungu wa kitanda hakupati.Ila hii ya askari kujificha kichakani imekaa kinafiki sana
π πUnajua dawa yake? Ukifika sehemu kuna kibao cha 50kph tembea 50kph, ukifika eneo haliruhusu kuovateki usiovateki. Hapa hata ajifiche uvungu wa kitanda hakupati.
Ila kuna siku niko road nimejiachia mara ghafla naona nguo nyeupe mbele halafu eneo la 50kphndefuuu ika idi nipunguze mwendo namfikia menye nguo nyeupe kumbe shehe ubwanwa!
ππππUnajua dawa yake? Ukifika sehemu kuna kibao cha 50kph tembea 50kph, ukifika eneo haliruhusu kuovateki usiovateki. Hapa hata ajifiche uvungu wa kitanda hakupati.
Ila kuna siku niko road nimejiachia mara ghafla naona nguo nyeupe mbele halafu eneo la 50kph ndefuuu ikabidi nipunguze mwendo namfikia menye nguo nyeupe kumbe shehe ubwabwa!
Na ndio maana tukikutana na msala, Bora utoe tu elfu 5 yaishe. Unakua umesave 25k na points.Hili suala la point ni kwa kila dereva saizi watu wa gari binafsi wanaona hawahusiki wanajua ni madereva maroli,basi,bajaji na bodaboda. Hii unaweza kukatwa na gari yako binafsi na leseni ikafungiwa hapo huwezi kuendesha gari yako
Sisi wafuata sheria tunasema wacha wanyooshwe tu maana vichaa wamekuwa wengi barabarani. Na askari wamejizatiti hadi usiku wapo wanawasubiri.Hili suala la point ni kwa kila dereva saizi watu wa gari binafsi wanaona hawahusiki wanajua ni madereva maroli,basi,bajaji na bodaboda. Hii unaweza kukatwa na gari yako binafsi na leseni ikafungiwa hapo huwezi kuendesha gari yako
Ha ha ha mtu baada ya kutii sheria analialia. Ila la ubovu wa gari ni mtego kwa madereva. Kabla ya point faini ya ubovu wa gari ambao dereva alitoa ripoti kampuni ndio inalipa. Huu utaratibu wa point ina maana dereva agome kuendesha na kampuni itampa dereva mwingine.
Leseni zote zina point 15. Ukifanya kosa ukaandikiwa zinapungua endapo zitaisha zote 15. Utafungiwa leseni na daraja litashuka na unatakiwa uende chuo kisha utafunguliwa baada ya miezi 6. Ukikosea mara ya 2 unafunguliwa baada ya miezi 12.Nawezaje kujua kama leseni yangu imepewa hizo point za offences?
Nawezaje kujua kwamba leseni yengu imekatwa point?Leseni zote zina point 15. Ukifanya kosa ukaandikiwa zinapungua endapo zitaisha zote 15. Utafungiwa leseni na daraja litashuka na unatakiwa uende chuo kisha utafunguliwa baada ya miezi 6. Ukikosea mara ya 2 unafunguliwa baada ya miezi 12.