Dereva Arusha: Unafanya kazi ya Kanisa mshahara ni Haleluya

Dereva Arusha: Unafanya kazi ya Kanisa mshahara ni Haleluya

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966

Wakazi wa Jiji la Arusha wamejikuta wakipata adha kubwa ya usafiri baada ya baadhi ya madereva wa daladala kugoma kuingiza magari yao barabarani wakipinga kile walichodai kuwa ni manyanyaso kutoka Land Transport Regulatory Authority (LATRA). Mgomo huo ulioshuhudiwa leo Jumatatu Mei 25, 2026 umeathiri njia mbalimbali ikiwemo kutoka katikati ya jiji kupitia Mrombo hadi Intel kuelekea Mapambazuko, pamoja na njia za Kilombero, Uswahilini, Dampo hadi Mapambazuko na Barabara ya Tengeru.

Baadhi ya madereva wakizungumza eneo la Soko la Mrombo wamedai kuwa maofisa wa LATRA wamekuwa wakiwatoza faini kubwa zinazofikia kati ya Sh250,000 hadi Sh350,000 kwa madai ya kuzidisha nauli iliyopangwa na mamlaka hiyo. Kutokana na hali hiyo, wananchi wengi walilazimika kutafuta usafiri mbadala ambapo magari ya Guta yaliongeza nauli hadi Sh1,000 huku bajaji na bodaboda zikitoza kati ya Sh2,000 hadi Sh3,000 kutoka Mrombo kuelekea katikati ya jiji. Wananchi wameiomba serikali pamoja na LATRA kutafuta suluhisho la haraka ili kurejesha huduma ya usafiri na kuondoa usumbufu unaoendelea jijini humo.
 
Back
Top Bottom