Dereva Bajaji ana Maisha Mazuri Kuliko Watumishi wa Umma

Dereva Bajaji ana Maisha Mazuri Kuliko Watumishi wa Umma

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
Watumishi wa Umma ni kundi la watu Maskini wanaojitahidi sana kuficha Hali Yao Kwa kupasi nguo..

Dereva Bajaji anaepeleka hesabu ya 20,000 Kwa boss wake ana maisha Mazuri kushinda Watumishi karibia robo tatu wa Umma.

Dereva Bajaji akikosa sana Kwa siku baada ya kutoa ya boss ni anabakiwa na 30,000-40,000 take home ambayo ni sio chini ya 1,000,000 on average hapo hana gharama za usafiri Kwa familia yake au kwenye mishe zake maana atatumia hiyo hiyo bajaji ya boss..

Ni Watumishi wangapi wa Umma wanapata milioni Moja Kwa mwezi hata wakiwa na hizo posho? Binafsi ni mtumishi wa Umma naongea ambacho Nina uhakika nacho.Hata Mimi mwenyewe hiyo take home ya milioni Moja naiona kwenye basic tuu sio take home,Laiti ningekuwa nafanya kazi sehemu ambayo Haina posho ningeadhirika,huu ndio ukweli.

Sasa chukulia Watumishi wengi wa Umma pamoja na Mishahara midogo Kuna wanapata posho ila unakuta posho zenyewe hazifiki hata Laki 5 Kwa mwezi,huyu atachaje kuwa na maisha magumu sawa na bodaboda?

Kwa dereva Bajaji yeye alifanya kazi miaka 2 tuu ananunua Bajaj yake lakini Watumishi wako kazini miaka na miaka kujenga tuu Hadi Mkopo na nyumba inaishia njiani.

Mwisho Serikali iache kudhalilisha Watumishi, iwaongezee Mishahara Ili wapate hadhi inavyostahili badala ya kudharaulika Kila siku na ndio sababu ya wake zao wengi kugongwa hovyo na madereva Bajaji na Bodaboda maana wao Wana uhakika wa supply ya pesa na ule usafiri unawapa hadhi kushinda Mtumishi.
 
Hata mfugaji ni bora kuliko mtumishi
Hata Bodaboda ni bora kuliko mtumishi
Hata wale maajenti wa mabasi wa pale msamvu

Ila saasa haiwezekani wote tukawa madereva wa bajaji kwani mabosi wa hizo bajaji watakosekana ambapo wengi ni haohao watumishi wa serikali! Huu ni mgawanyo tu wa majukumu na ndio unafanya Dunia inazunguka
 
Ongezeko la mshahara halisaidii kila wakati, maana kiasi chochote kikishaongezwa kinadokolewa Tena kwenye Makato na kubaki ROBO.

Cha muhimu, serikali ilipe HAKI za mtumishi.

Siyo kipesa hicho hicho anacholipwa ndio anakitumia kufanya kazi za serikali Tena.

- Mtumishi apewe nyumba ( Kama HAKUNA nyumba, serikali ilipe pango )

- Mtumishi apewe pesa ya nauli ya LIKIZO, Kama ilivyo kwenye sheria.

- Mtumishi alipwe gharama za Usafiri, stationery, na mawasiliano kwa kazi za serikali.

- Mtumishi alipwe overtime payments kwa kazi zote atakazofanya weekend, sikukuu na baada ya saa za kazi.

Kikokotoo Cha KUSTAAFU kiwe kimoja kwa watu wote ikiwemo TABAKA la kisiasa.
 
Yaani dereva Bajaj ni bora kuliko mtumishi wa umma?!?
Tena Bajaj ambayo sio yake ?!?
Hizi dharau zimezidi sana
Narudia tena
1. Bima ya afya
2. Uhakika wa mshahara kila mwezi
3. Mikopo
4. Mafao baada ya kustaafu

Huyo dereva Bajaji au Bodaboda
Wewe unachoona ni hela za haraka haraka ambazo wanazishika ila kwa faida za muda mrefu hazizidi watumishi.

Acheni dharura basi.
 
Yaani dereva Bajaj tena ni bora kuliko mtumishi wa umma?!?
Tena Bajaj ambayo sio yake ?!?
Hizi dharau zimezidi sana
Narudia tena
1. Bima ya afya
2. Uhakika wa mshahara kila mwezi
3. Mikopo
4. Mafao baada ya kustaafu

Huyo dereva Bajaji au Bodaboda
Wewe unachoona ni hela za haraka haraka ambazo wanazishika ila kwa faida za muda mrefu hazizidi watumishi.

Acheni dharura basi.

Dereva wa bajaj ni bora sana.

Mafao, sijui mafaa, ngoja hata nisiseme, wanaishia ku repair nyumba, kujenga, au Kuanza kufuga kuku ambayo yote hufa maana hawana uzoefuwa biashara...

Kutokana na kuwa na uhakika wa Dereva wa bajaj wa:


Bima
Mshahara
Mikopo,

Atajibiidisha na kuwa na akiba na:

-Atajenga.
  • Atafungua biashara mke asimamie.
  • Atakuwa na Bima...

Bado ana uhuru fulani wa kufanya mambo yake.....
 
Back
Top Bottom