Dereva Bajaji ana Maisha Mazuri Kuliko Watumishi wa Umma

Uongo wa wanasiasa na kudanganya waendesha bodaboda. Kiukweli ni hatari nguvu kazi kuendesha bodaboda. Kuna madhara mengi mno kwao na kwa nchi
 
Itakuwa unauza bajaji Sasa unatafuta mteja ambae kimsingi awe mtumishi
Biashara ya bajaji ni ngumu na njaa sana Bora hiyo 8500000 uwekeze kwenye vifaa vya simu au vipodozi na sio bajaji
Huu ni uongo 100% wewe ni kati ya watu wengi wenye roho mbaya mwenye kukatisha watu tamaa sana
 
Ana masihara sana, unakuta kijiwe kina bajaji 50+ wanapakia Kwa foleni kupata 20 tu ni mtiti.
Na hiyo foleni mchana inaganda inatoka kimatonematone unawapakia hawashuki hadi mwisho unafika na 3000 ukirudi unapata 2000 mafuta umetumia ya 3000 hujakutana na trfiki aseme TU nakuandikia 10000 nasema hivi Bora ufungue
1.duka la chakula
2.duka la urembo
3.vifaa vya simu
4.jiko uuze na soft drinks
5.Mashine uanze kufyatua tofali hata uanze na Chache.
Ila sio bajaji
 
Leo siku ya waendesha Bajaji… taratibu tutafikia kwa waendesha Daladala
 
Ungekuwa na akili ungekopa ukanunua bajaji ukaendelea kibarua chako ukaacha kulalama
 
Huu ni uongo 100% wewe ni kati ya watu wengi wenye roho mbaya mwenye kukatisha watu tamaa sana
Mi ni kati ya watu wachache wenye msaada,nimefanya biashara ya bajaji sana goms mbezi goms Kongo goms mnazi mmoja Kisha nikaamia mnazi mmoja ferry na kuendelea naijua hii biashara kuliko unavyodhani ni umiza kichwa na haikuwi ila inashuka.
2015 kurudi nyuma yes ilikuwa biashara halisi ila kwa Sasa ni biashara mfu
Kuweka 9000000 kwenye bajaji ni risk wekeza vifaa vya simu bidhaa za urembo jiko au vifaa vya ujenzi hasa tofali kama uko mahali pazuri
 
Sasa kwani kwenye Wilaya kunakuwa na maofisa wangapi? kama sio mmja?
 
Nyie ndio mnafanya watoto wakatae shule wakiamini udereva bajaji una pesa matokeo yake wanaacha shule wanaenda kwenye udereva bajaji at the end familia umaskini hauishi kwa kupenda vitu vya short cut, mnaamza shikana uchawi kwenye familia kumbe mmejiroga wenyewe kwa tamaa tamaa mama hizi

Kuna familia umaskini umekithiri kwa sabaabu tu zamani biashara ya udereva tax ulikuwa unalipa so baba mpaka watoto wote walikimbilia kwenye udereva tax hawakutaka shule matokeo yake Sasa boda boda zikaja bajaji zikaja tax zikakosa deal kijana kawa mkubwa ujuzii wake ni udereva tu at the end ndio hawa unaowana kwenye bajaji nk , wanatamani waendeshe. Magari ya serikali ila sifa hawana so familia zinaishi maisha. Ya kuunga unga tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…