zwangandaba
JF-Expert Member
- Jan 31, 2023
- 750
- 1,427
Motivation speaker hamna tofauti na mafarisayo.Watumishi wa Umma ni kundi la watu Maskini wanaojitahidi sana kuficha Hali Yao Kwa kupasi nguo..
Dereva Bajaji anaepeleka hesabu ya 20,000 Kwa boss wake ana maisha Mazuri kushinda Watumishi karibia robo tatu wa Umma.
Dereva Bajaji akikosa sana Kwa siku baada ya kutoa ya boss ni anabakiwa na 30,000-40,000 take home ambayo ni sio chini ya 1,000,000 on average hapo hana gharama za usafiri Kwa familia yake au kwenye mishe zake maana atatumia hiyo hiyo bajaji ya boss..
Ni Watumishi wangapi wa Umma wanapata milioni Moja Kwa mwezi hata wakiwa na hizo posho? Binafsi ni mtumishi wa Umma naongea ambacho Nina uhakika nacho.Hata Mimi mwenyewe hiyo take home ya milioni Moja naiona kwenye basic tuu sio take home,Laiti ningekuwa nafanya kazi sehemu ambayo Haina posho ningeadhirika,huu ndio ukweli.
Sasa chukukia Watumishi wengi wa Umma pamoja na Mishahara midogo Kuna wanapata posho ila unakuta posho zenyewe hazifiki hata Laki 5 Kwa mwezi,huyu atachaje kuwa na maisha magumu sawa na bodaboda?
Kwa dereva Bajaji yeye alifanya kazi miaka 2 tuu ananunua Bajaj yake lakini Watumishi wako kazini miaka na miaka kujenga tuu Hadi Mkopo na nyumba xinaishia njiani.
Mwisho Serikali iache kudhalilisha Watumishi,iwaongezee Mishahara Ili wapate hadhi inavyostahili badala ya kudharaulika Kila siku na ndio sababu ya wake zao wengi kugongwa hovyo na madereva Bajaji na Bodaboda maana wao Wana uhakika wa supply ya pesa na ule usafiri unawapa hadhi kushinda Mtumishi.
Mnaongea nadharia sana kuliko uhalisia.
Hii mijadala ya kazi fulanikuwa bora kuliko kazi nyingune ni utoto tu. Hakuna hitimisho lenye ukweli ndani yake.
Katika hii dunia kuna kazi za kila aina na kila kazi ina kipato chake kulingana na mazingira