Dereva wa Basi la Saratoga apigwa na Askari wa JWTZ

Dereva wa Basi la Saratoga apigwa na Askari wa JWTZ

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Dereva wa basi la Saratoga linalofanya safari kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, Yasini Shabani (45), ameshambuliwa kwa kupigwa maeneo mbalimbali ya mwilini na Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), anayejulikana kwa jina la Emmanuel Peleka baada ya basi hilo kulipita gari la JWTZ katika eneo la Picha ya Ndege Kibaha mkoani Pwani.

Sihalalishi alichofanyiwa dreva Basi

Ila Madreva mabasi sometimes wanakera Sana, wanajifanya wana haraka sn kuliko watumiaji wengn wote wa barabara.

Sometimes Wanachomekea kwa fujo na overtaking zao za kipuuzi sn zisizochukua tahadhali za usalama barabarani.

Ukikaa kizembe kwny usukani, ukawakadiria kwa macho, unastuka mtu huyu Hapa, wanachezesha Basi ghafla, unamkwepa unahama Njia, wanakusababishia ajali afu wao wanalala zao mbele na matusi juu wanatukana.

Sent using JamiiForums mobile app
 
Morogoro road imekua ya kiduanzi Sana,mahari makubwa ya mizigo no mengi,yanasababisha jam ,yanaharibika njiani ovyo,kusababisha ajali,yanatembea mwendo wa kinyonga,Apo inasababisha fujo nyingi Barabarani,watu wanashidwa kuwahi inavyotakiwa,sehemu za ku overtake hakuna ,au ni chache .fujo tupu
 
Mkuu wa Majeshi angetoa tamko mbele ya waandishi kuwa ni marufuku mwanajeshi kumpiga raia

Hivi kwanini huwa wanajiona wakivaa gwanda basi hilo gwanda ndio linapiga?
Mbona Enzi zetu tulikuwa tunaheshimu amri zote?

Utakuta ni ushamba umewajaa maana mtoto wa mjini hawezi kufanya ujinga huu
 
Dereva wa basi la Saratoga linalofanya safari kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, Yasini Shabani (45), ameshambuliwa kwa kupigwa maeneo mbalimbali ya mwilini na Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), anayejulikana kwa jina la Emmanuel Peleka baada ya basi hilo kulipita gari la JWTZ katika eneo la Picha ya Ndege Kibaha mkoani Pwani.

Acha apigwe tu hakuna namna. Siku mkiacha kuogopa manguo yao mtaishi kwa kujiamini.

Kuna mwamba last year aliwakalisha chini askari 3 kwa upuuzi wao, walikosea wakamkadiria vibaya wakaingia cha kike
 
Back
Top Bottom