Dereva wa Basi la Saratoga apigwa na Askari wa JWTZ

Dereva wa Basi la Saratoga apigwa na Askari wa JWTZ

Watu humu mnaongea kwa mihemko iko hivi ni sawa kabisa mwanajeshi kutopiga raia lakini hawa watu wa mabus alooo wanakera sio siri, kwanza wanahisi ukiwa na chombo kama pikipiki ww ni boda boda n ahuna leseni yaani wanakua na maneno mabaya sana na muda mwingine dharau hizo wanapeleka mpka kwa wenye magari ilimradi yeye anajiona yupo kwenye bus ni kubwa ww mwenye gari ndogo huna haki. Wanakera nimeshashihudia mtu naataka kuingi akulia kaka kagikati ya chaki kawasha na indicator lakini jamaa wa bus anapiga honi kali kanakwamba huyu anaeingia kushoto apishe bus ipite ndio yeye atafute utaratibu w akuingia naakoenda. Wanakosa sama ustaarabu kazingua ndio maana kala kichapo ni nadra kukuta mjeda anapiga raia nahisi toka 2020 mpka leo ndio tukio la kwanza nalisikia
 
Kiutaratibu vyombo vya ulinzi na usalama(JWTZ,PT, UT na TISS) vimeanzishwa kwa sheria na kanuni. Kupitia sheria na kanun hizo ndo tunapata majukumu na ukomo wa kila chombo. Ukomo wa chombo kimoja ktk utekelezaji wa kimajukumu ndo mwanzo wa chombo kingine, japo huwa wanafanya Joint Task Force ktk kutimiliza jukumu flani mfano OPS Kimbunga, OPS Kibiti na zingine nyingi.

TPDF wanazo Defence Force Regulations ktk maswala ya pesa (Volume I) na maswala ya maadili(Volume II), sheria hizi ndo uti wa mgogo ktk usimamiz na uendeshaji wa jeshi.

Jeshini kuna watu wawili, Maafisa na askari. Hawa wote hupitia course za awali za kijeshi kabla ya kula kiapo cha Utii na Ulinzi. Maisha ya askari na maafisa wawapo mafunzoni na vikosini hupaswa kuwa ya nidham na utii. Pale inapotokea askari au afisa amekengeuka taratibu za kumuwajibisha hufuatwa.

Jeshini uongoz huanzia ngaz ya section mpaka ngaz ya juu kabisa. Ngaz ya sec wapo sec commander na 2IC wake. Ngaz ya Platoo yupo Pl commander na 2IC wake hvyhvyo ktk brigade. Ktk ngaz hzo zote za kiuongoz VOLUME I & II husimamiwa na kufuatwa kwa msaada wa Military Police.

Askar walio wengi ni darasa la saba, form four na six. Mbaya zaid hawa ndo man-power majeshin. Wao hufunzwa kutii amri ya mkuu wake na kutumia nguvu. Hawa hawafundishwi hz sheria za maadili na maswala ya pesa. Ila kwa maafisa pale TMA bila ya shaka hufunzwa sheria hizi kwakuwa wao huandaliwa kuwa viongoz majeshin.

Hvyo basi, kiwango cha matukio ya mafisa wa jeshi kumpiga raiya au kugomea chombo kingine cha ulinzi na usalama ni ktk viwango vidogo sn ukilinganisha na matukio ya askari. Hivyo, TPDF yabid kuwapa askari wake mafunzo ya sheria na kanuni hz, ili kuepuka kulipaka Jeshi letu matope ya kujichukulia sheria mkonon kw askari mmojammoja.
 
Hawa wapumbavu wanajikuta kama wao wako juu ya Sheria hata kama alifanya kosa ndio wampige? Yani wao hua wanajiona wamekua polisi wamekua mahakama na wamekua mahakimu nikupiga piga watu hovyo ilimradi tuu kisa mwanajeshi, ndio maana maeneo Fulani hivi kigoma walikua wanarogwa tuu washenzi Sana hao
 
Sjyo sawa kumpiga wangempeleka police Kisha police wamfikishe mahakamani
 
Dereva wa basi la Saratoga linalofanya safari kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma, Yasini Shabani (45), ameshambuliwa kwa kupigwa maeneo mbalimbali ya mwilini na Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), anayejulikana kwa jina la Emmanuel Peleka baada ya basi hilo kulipita gari la JWTZ katika eneo la Picha ya Ndege Kibaha mkoani Pwani.


Pole zake aliepigwa kuna shida sehemu lazima tusikie upande wa pili
 
Huyo Koplo wa Jeshi hana akili, anatakiwa afanye kazi aliyoajiriwa jeshini na sio kufanyakazi za Usalama Barabarani.

Kama kuna makosa yalifanywa na Dereva wa basi alitakiwa atoe taarifa kwenye kitengo cha Usalama Barabarani.

Huyo mwanajeshi akamatwe apelekwe mahakamani Sheria ichukue mkondo wake
Hakika
 
Kwa fujo za madereva wa ma bus, wapigwe tuu, huwa wakiwa kwenye bus wanajiona nao ni wakubwa kama hayo ma bus, wanadharau na roho mbaya,

Wapuuzi wengine ni madereva wa magari ya migodini wanapakia mchanga, upo site yako anakufata huko huko na hapunguzi mwendo wewe ndio utafute vichana vya kuingia, ingekua wanamingo na wajeda wangepigwa kila siku
 
Back
Top Bottom