Kiutaratibu vyombo vya ulinzi na usalama(JWTZ,PT, UT na TISS) vimeanzishwa kwa sheria na kanuni. Kupitia sheria na kanun hizo ndo tunapata majukumu na ukomo wa kila chombo. Ukomo wa chombo kimoja ktk utekelezaji wa kimajukumu ndo mwanzo wa chombo kingine, japo huwa wanafanya Joint Task Force ktk kutimiliza jukumu flani mfano OPS Kimbunga, OPS Kibiti na zingine nyingi.
TPDF wanazo Defence Force Regulations ktk maswala ya pesa (Volume I) na maswala ya maadili(Volume II), sheria hizi ndo uti wa mgogo ktk usimamiz na uendeshaji wa jeshi.
Jeshini kuna watu wawili, Maafisa na askari. Hawa wote hupitia course za awali za kijeshi kabla ya kula kiapo cha Utii na Ulinzi. Maisha ya askari na maafisa wawapo mafunzoni na vikosini hupaswa kuwa ya nidham na utii. Pale inapotokea askari au afisa amekengeuka taratibu za kumuwajibisha hufuatwa.
Jeshini uongoz huanzia ngaz ya section mpaka ngaz ya juu kabisa. Ngaz ya sec wapo sec commander na 2IC wake. Ngaz ya Platoo yupo Pl commander na 2IC wake hvyhvyo ktk brigade. Ktk ngaz hzo zote za kiuongoz VOLUME I & II husimamiwa na kufuatwa kwa msaada wa Military Police.
Askar walio wengi ni darasa la saba, form four na six. Mbaya zaid hawa ndo man-power majeshin. Wao hufunzwa kutii amri ya mkuu wake na kutumia nguvu. Hawa hawafundishwi hz sheria za maadili na maswala ya pesa. Ila kwa maafisa pale TMA bila ya shaka hufunzwa sheria hizi kwakuwa wao huandaliwa kuwa viongoz majeshin.
Hvyo basi, kiwango cha matukio ya mafisa wa jeshi kumpiga raiya au kugomea chombo kingine cha ulinzi na usalama ni ktk viwango vidogo sn ukilinganisha na matukio ya askari. Hivyo, TPDF yabid kuwapa askari wake mafunzo ya sheria na kanuni hz, ili kuepuka kulipaka Jeshi letu matope ya kujichukulia sheria mkonon kw askari mmojammoja.