Dereva wa basi namba T331 BMM achunguzwe haraka kabla hajaua watu!

Dereva wa basi namba T331 BMM achunguzwe haraka kabla hajaua watu!

Shida bas za kibongo konda ana nguvu(ya maamuzi) kushida abiria, na abiria hawana ushirikiano
Ni kweli, na abiria ndo wengi. Kuna wanyama wanaitwa nyumbu huwa ni wengi ila sasa.
 
Hapo ndipo nchi hii inafeli,yaani watawala wameshajua upumbavu wa watanzania ndio mtaji wao, wenzetu sasa wanaanza kutumia demerits systems, yaani kila mwaka dereva anapewa 12pts, za kutumia mwaka mzima, zikiisha kabla driving license yake automatically inajifunga,kwa kosa hapo juu, huyu dereva wa bus la abiria angepoteza pts zote, na mwisho madereva hawa wa public transport ni lazima pia wawe na PDP ili waendeshe magari haya
PDP ni nini Mkuu
 
Kiukweli nasafiri muda mwingi,ila mabasi yote ni tatizo,overtake, speed,na ushindani barabarani ni tatizo.
 
Pole sn mkuu,hizi ajali zinaepukika tu wakinyooshwa vizuri hawa madereva[emoji22]
 
Ni Basi la kampuni gani? Wazani Kuna MTU ambaye anafuatilia namba ya gari hasa Basi?
 
Ni Basi la kampuni gani? Wazani Kuna MTU ambaye anafuatilia namba ya gari hasa Basi?
Kama alivyosema mdau, hakuna ushahidi..., sasa linapokuja suala la kutaja kampuni inaweza isiwe haki kwa kampuni, dereva achunguzwe yeye kama yeye
 
Sijui ni stress za mapenzi au bangi zinawakataa maana ukiuliza wanakokimbilia hata wenyewe hawajui.kuna basi Moja limetupita juzi Kwa Fujo zote kidogo litutupe mtaroni,ila mbele kidogo tukalikuta limepaki pembeni mwa road abiria wanachimba dawa,Nashangaa mbio zote zile kumbe alikuwa anawahisha watu wakojoe?Au
 
mkuu ulikua ulikua ulikua maeneo gani? izo basi za majinja special ni basi za ovyo sana izo basi ilishawahi kusababisha ajali pale mafinga changalawe kisa ku ovatake kingese ivo ivo
 
Utakuwa ulijaa kwenye barabara na kigari chako used cha Japan na kileseni chako cha kuhonga kuletewa nyumbani bila kupitia mafunzo serious ya udereva na kufaulu mitihani yote ya theory na vitendo

Madereva wa mabasi ya safari ndefu wakikuona hujielewi wana namna ya ku overtake ambayo kama wewe leseni uliletewa nyumbani lazima uende porini huko wanajua namna ya kukusukumiza huko kama u awabania ku overtake

Anakuchomekea kichwa kama anataka kukugonga mbele kwenye usukani ulipo halafu huyo anachomoa mbio akikuacha wewe unasererekea huko na Kigali chako mtumba cha wajapani

Ukiendesha na vigari vyenu vya mikopo au mitumbab hakikisha unaancha nafasi kubwa gari kubwa kama mabasi ya overtake kwa raha zao sio unakomaa tu kimwendo chenyewe kidogo na barabara unazuia basi ku overtake lazima akufanyizie na hutasagau alichokufanyizia

Siku ingine usirudie huo ujinga mwenye nguvu mpishe .Basi ukiona kinakuja wangu wangu achia nafasi lipite usikomae tu na hicho kimtumba chako
 
Mabasi ya jioni kanda kaskazini yanakimbia
Vibaya sana!

Tahadhari ichukuliwe mapema jamani.
 
Back
Top Bottom