Dereva wa basi namba T331 BMM achunguzwe haraka kabla hajaua watu!

Kenge mmoja, mbele kuna Lorry, na kulia kuna Lorry linakuja, una-overtake vipi kama sio bangi zinawasumbua
 
Tunaomba namba za dereva wa Semi tumchangie tafadhari ntashukuru sana sana ana stahiki pongezi kubwa sana
 
Kama alishtakiwa kwa wana usalama muda huo huo, abiria wake ndio wangetoa ushahidi kama wangekuwa tayari kutoa ushirikiano.
Tatizo lingine ni rushwa, kwahiyo hata hiyo faini sina hakika sana hata kama alipigwa
 
Kwa kweli alifanya Jambo Baya Sana na hiyo adhabu unayofikiria alipata ni ndogo. Tatizo ushahidi toshelevu hakuna kama picha mnyato WA tukio nk , labda kama abiria waliokuwa kwenye Hilo basi watajitokeza
 
Kuna shida kubwa sana kwenye mabasi hivi sasa, last week tumenusurika kusambaratishwa kwenye bus kona za mlima wa Dumila baada baada ya mabasi matatu kuovertake malori kadhaa kwa mpigo huku yule wa mbele akijichomekachomeka wakati wale wawili wa nyuma yake hawaoni kinachotokea mbele.

Nadhani ipo haja magari yote yafungwe camera ili footprint zinazopatikana zitumike kufilter madereva wa hovyo
 
Tatizo lingine ni rushwa, kwahiyo hata hiyo faini sina hakika sana hata kama alipigwa
Wengine wanachofanya ni kulipa fine mapema asubuhi ili huko mbele wasisumbuliwe, nadhani ni kutokana na utaratibu wa kulipa fine once
 
Panda ndege
 
Baadhi ya wamiliki wa kampuni za mabasi wanapendezwa na mwendokasi kasi.

Tena wanatafuta madereva wenye mwendokasi.

Na wananunua makosa yote ya njiani [emoji108]

Inasikitisha sana.[emoji848]

Sijui itokeapo ajali hawajui kwenye dhambi ya kuua nao watakuwa na mgao wao?!
 
Unaogopa kufa angali Kuna mabikra 77 wanakusubiri huko. Ww hupendi kwenda mbinguni kwa baba!?

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…