BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Alikuwa na kitu kama kisu!!! Kwa maneno mengine si kisu kwani polisiccm wameshindwa kuthibitisha. Hao polisiccm aliowajeruhi watatu aliowajeruhi alitumia nini kuwajeruhi? Je, polisiccm watatu walishindwa kutumia nguvu kumdhibiti huyo dreva hadi wamuue!? Huyo aliyemuua ana kesi ya kujibu na afukuzwe kazi mara moja.
Jana usiku kwenye taarifa ya habari saa mbili jashi la polisi lilieleza jinsi tukio lilivyokuwa, polisi wanadai dereva alikuwa na kitu kama kisu! Inamaana hata baada ya kumuua hawakuweza kutambua kama ni kisu au la! Pili wananasema mtuhumiwa akiwa na zilaha yake hiyo alitaka kumnyang'anya silaha askari na askari husika alifanikiwa kumpiga risasi mtuhumiwa, mwisho wanahitimisha kwa kusema mtuhumiwa aliyekuwa na akitaka kupora silaha aliweza kuwajeruhi askari wengine waliokuwepo karibu na tukio! Maelezo haya ninaona hayako sawa japo nalazimika kuyakubali.