Dereva wa UDOM akamatwa kwa madai ya kummwagia Kemikali Afisa Mtendaji

Dereva wa UDOM akamatwa kwa madai ya kummwagia Kemikali Afisa Mtendaji

Huyo mwanaume asiachiwe hadi haki itendekee.
Jamani ndoa haiko kwa kila mtu, na sio lazima.

Duuuh kazi ipooo, polee zao sanaa hao wahanga.
Ni Kweli ila unakuja kuleta hbr za kugawana Mali nilizo ziangaikiaa hpn kwa Kweli Kama Mali s atafute zake

Sijapenda tukio ila pia swala la kugawna Mali siyo sawa angeendele na maish yake na uzuri Ana kazi
 
Umeachana na mumeo Tena inawezekana chanzo ni wewe.

Umepata bwana na umezaa nae. Maana mtoto ana miezi sita na ndoa ilivunjika mwaka juzi.

Bado unataka kumfilisi mtalaka wako eti mgawane mali.
Kuna matatizo yakujitakia.
Sahih kbsaaa
 
View attachment 2674124

Dereva wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Lusajo Makiwelu, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwamwagia kemikali watu wawili akiwemo mtalaka wake, Witness Nguvalwa (31) na mtoto wake mwenye umri wa miezi sita (jina limehifadhiwa).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, alipozungumza na Mwananchi jana Juni 29, akisema lilitokea juzi wakati mwanamke huyo na mtoto wake wakiwa wanasubiri daladala eneo la Maghorofani jijini hapa.

Amesema wamemshikilia dereva huyo kama mshukiwa baada ya mtu asiyejulikana kummwagia mtalaka wake tindikali.

"Ni kweli taarifa hizo zipo tulipata taarifa hizo na tulifanya ufuatiliaji hiyo jana ( juzi) majira ya usiku na huyo mtuhumiwa tayari ametiwa mbaroni, kwa sasa tunaendelea na mahojiano," ameeleza Kamanda Martin Otieno.

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Witness ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Idedelomkazi wilayani Mufindi mkoani Iringa, amesema mkasa huo ulimkuta aliposhuka kituo cha Maghorofani akitokea Mafinga mkoani Iringa alipokuwa akisubiri usafiri wa kumpeleka atakofikia.

Amesema alikuja mkoani Dodoma kuleta wito wa Mahakama ya Mwanzo ya Mafinga kwa aliyekuwa mumewe ambaye walitenganishwa na mahakama hiyo.

"Safari yangu ilianza saa 3:00 asubuhi na Gari ya Shabiby nikitokea Mafinga lengo likiwa ni kuleta wito Mahakama ya Mwanzo ya Dodoma.

"Safari ilienda vizuri hadi nilipofika kituo cha mabasi Maghorofani niliposhuka kusubiri daladala au bajaji ili niende kukabidhi wito huo,” amesema.

Amesema akiwa katika kituo hicho, alipita mwanaume mmoja ambaye hakumfahamu akiwa ameshika kichupa mkononi kilichokuwa na kimiminika na mara baada ya kumsalimia alimwagia usoni.

“Alichofanya ni kunisalimia tu dada habari na kabla sijamjibu akanimwagia tindikali. Kwa muda nilibanwa na pumzi lakini nikajitahidi nikaomba msaada kwa watu waliokuwa pembeni na kituo hicho,” amesema.

Amesema madereva bajaji na bodaboda walimsaidia na kumfikisha kituo cha polisi, ambapo alipewa PF3 na kisha walimpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambako amelazwa.

Witness amesema alikuwa akimpelekea Makiwelu wito wa mahakama uliolenga kugawana mali walizochuma pamoja baada ya ndoa yao kuvunjwa na Mahakakama ya Mwanzo ya Mafinga mwaka juzi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Baraka Mponda amesema walimpokea mama huyo na mtoto wake wa miezi 6 juzi jioni wakiwa wamejeruhiwa usoni kwa kumwagiwa kemikali.

Dk Mponda amesema majeruhi hao walifika wakiwa kwenye maumivu makali, mama akiwa ameathirika maeneo ya usoni, shingoni na begani na usoni kwa upande wa mtoto.

Amesema majeruhi hao wameendelea kupatiwa matibabu zaidi hospitali hapo.

Chanzo: Mwananchi
Hii kesi ina nukta nyingi mno.

Pole sana kwa wahanga
 
Huyo mwanaume asiachiwe hadi haki itendekee.
Jamani ndoa haiko kwa kila mtu, na sio lazima.

Duuuh kazi ipooo, polee zao sanaa hao wahanga.
Kwani umeambiwa yeye ndiyo aliyemmwagia tindikali??? Aachiwe haraka sana mpaka atakapohukumiwa na mahakama kama ana hatia, presumption of innocence ndiyo katiba yetu.Wanawake mmezidi kuchanganya na kula hela za wanaume halafu mnakimbilia kudai talaka na mgawanyo wa mali. Matukio haya ya kikatili hayatakwisha hadi Yesu arudi labda wanawake waache wizi na ukahaba.
 
Tamaa za Mali

Utakuta hapo alikuwa yuko na dume lingine,likamshawish I kwenda kudai Mali hayo ndiyo yamemkuta sasa

Ova
obvious lina midume, ndoa imevunjwa mwaka juzi tu leo ana mtoto mchanga wa mwanaume mwingine. Nimesoma ktk other media ndoa ilivunjwa na mahakama 2020.
 
Mtoto hata mwaka hajafikisha mwanamke anataka mgawane Mali,🤔dah kina mama punguzeni Kasi kidogo mmezidi Sasa.
 
Umeachana na mumeo Tena inawezekana chanzo ni wewe.

Umepata bwana na umezaa nae. Maana mtoto ana miezi sita na ndoa ilivunjika mwaka juzi.

Bado unataka kumfilisi mtalaka wako eti mgawane mali.
Kuna matatizo yakujitakia.
Mahakama ndio zinatuangusha

Talaka ya mwaka juzi haijaisha mpaka leo...

Idara ya Mahakama imeoza. Eti Jaji Mkuu Juma kaongezewa mkataba....
 
Back
Top Bottom