Nasadiki kwa Mungu mmoja. Baba Mwenyezi, muumba mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Nasadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristu, Mwana wa pekee wa Mungu. Alyezaliwa kwa Baba, tangu milele yote. Mungu aliyetoka kwa Mungu, mwanga kwa mwanga, Mungu kwel kwa Mungu kweli. Aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na baba, ambaye vitu vyote vimeumbwa naye. Ameshuka toka mbinguni kwa ajil yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu. Akapata mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwake yeye Bikira Maria, akawa mwanadamu.
Hiyo ni sehemu ya nasadiki ambayo kila mkatoliki anaisema kila siku kwernye sala ya asubuhi, anapunguza vipi Umungu wa Yesu kwa kusherekea kuzaliwa kwake?