Desemba 25: Je, ni siku aliyozaliwa Yesu au twaadhimisha tu kumbukumbu?

Desemba 25: Je, ni siku aliyozaliwa Yesu au twaadhimisha tu kumbukumbu?

sio kazi yangu kukufundisha KILATINI lugha ya kanisa na lugha ambayo hata kingereza chenyewe unachojidainacho kimetoa misamiati mingi tu ndani yake

nimekwambia kasome kwanza KILATINI kama lugha ya kanisa na kama lugha yenye athari katika biblia. ukimaliza ndo urudi hapa ili tuongee lugha moja.
mkuu lugha ya kanisa tena???
kanisa Lipi???
maana lilikoanzia(Kanisa la Kwenye Bibilia) hakukuwa na ulatini wowote?
Ila nakuelewa maana hiyo itaingia katika makundi yale mawili unayoyatumia kama authority yako ya kidini ( mapokeo nje ya bibilia na matamko ha kikanisa lako)
 
asante kwa ushauri.
huwa tunajadili humu muda wote chochote humu mkuu.
ila ushauri mzuri, ingawa Bibilia inasema tunapaswa kuwa tayari wakati wowote kutetea tumaini tulilonalo ktk Yesu.
Kama unatumaini katika xmass ni vizuri tuelimishane, hata sisi wagalatia tunahaki ya kufahamishwa kwa upendo lkn bila hofu na matukano.
nakutakia maandalizi mema ya kumpokea MKOMBOZI....amani ya Bwana itawale.
 
mfano wa mungu aliyetumia giza kuwapeleka watu mwangani.
Truth shall set you free, free indeed and not paganism shall set pagans free.
We jamaa kinachokupungua ni logical advocacies, Yesu mwenyewe anasema vyema kuwa hakuja kwa ajili ya watu wema bali wadhambi.

Je, giza lina nguvu kuishinda nuru..??
Kumuondoa Mungu jua (giza-spiritually) na kumweka Yesu (Nuru/mwanga-spiritually) nani amesshinda mpinga Kristo au Kristo mwenyewe..?

Mungu akili zako unahisi Mungu anaongozwa na biblia tu katika kutufundisha mambo yamhusuyo yeye. Bila shaka ni sumu ulizomezeshwa zinakusumbua na kusahau kuwa Mungu kakuumba rational/reasoning ability na zaidi anakufundisha kwa Mtakatifu.
 
Sijui kwa nini kuna watu hii sikukuu inawauma,wanakuja kutuandikia vimaneno vyao vyepesi vyepesi wakihisi watu hawatosheherekea...POLENI SANA Christmas itabaki kuwa Christmas......uhuru wa kuabudu na kuamini...mafundisho yenu FEKI pelekeni kwenye makanisa yenu au misikitini.
tatizo ni ubwabwa wanafikiri tunaula xmas tu au tunakula ili kujaza matumbo kumbe wenzao ni zaidi ya hapo MIOYO NA ROHO ndio mwisho ukifeli hapo kwenye MOYO na ROHO. xmas hata ungekula debe zima la pilau kwako haina maana kabisa. hilo walijui na ukweli huo hawataki kuusikia
 
nakutakia maandalizi mema ya kumpokea MKOMBOZI....amani ya Bwana itawale.
amina ubarikiwe sana.
Umeandika mambo makubwa na ya kunyenyekeza mkuu.
'' Na mimi leo, katika maombi nitakuomba sio mimi tu, wewe na wengine wote wenye nia chanya ya Kumpokea Yesu Kwa Kudumu katika Kumuamini na mafundisho yake, tuokolewa akija siku isiyo na jina''
amina.
 
asante kwa kunifahamisha wigo wako wa authoritative source za imani yako.
Ila wigo huo unaonekana ni endless.
Binafsi naamini katika Bibilia na Bibilia pekee, Vingine vyote nje ya bibilia ni maoni ambayo yale yanayokubaliana na bibilia 66 books nakubaliana nayo, Yanayopingana kapuni, Yaliyoneutral ushauri wa Bibilia utasaidia kuyaendorse au kuyaweka kapuni.

ndio maana nasema krismass na easter ni hekima za kikatoliki na viongozi wao sio bibilia wala halina uhusiano wowote na bibilia hata kama litahusishwa na bibilia. Ni sahihi kwenu na wanaopenda ila sio universal christian practice.
hivyo unakubaliana na mimi kuwa umwilisho ni fundisho la imani kwa sababu imani yote chanzo chake ni biblia hivyo ni la biblia pia au bado unapinga ??? na kusimamia msimamo wako kuwa sio fundisho la imani ila ni biblia ?
 
We jamaa kinachokupungua ni logical advocacies, Yesu mwenyewe anasema vyema kuwa hakuja kwa ajili ya watu wema bali wadhambi.

Je, giza lina nguvu kuishinda nuru..??
Kumuondoa Mungu jua (giza-spiritually) na kumweka Yesu (Nuru/mwanga-spiritually) nani amesshinda mpinga Kristo au Kristo mwenyewe..?

Mungu akili zako unahisi Mungu anaongozwa na biblia tu katika kutufundisha mambo yamhusuyo yeye. Bila shaka ni sumu ulizomezeshwa zinakusumbua na kusahau kuwa Mungu kakuumba rational/reasoning ability na zaidi anakufundisha kwa Mtakatifu.
reasoning yako nzuri imeruka baadhi ya maelezo yangu na ninacjosisitiza.
Huwezi kuyumia GIZA (upagani, uzushi na uongo) kusambaza ukweli wa kuhusu kristo wa watu waliogizani.
Unatumia NENO ambalo ni taa kwa walio gizani.
Kutumia sikukuu za kipagani ili uwafurahishe na kuwavuta wapagani kutoka gizani ni kinyume na fundisho la Yesu.
TRUTH (not pagan traditions and human wisdoms) will set sinners and those who are in darkness free.
 
kusherehekea birthday ya Mungu (Yesu) leo ni kumbinadamisha yeye aliyehai, alikuwa hai milele.
kutumia mbinu za gizani kuwashawishi watu waelekee nuruni ni kupoteza mwelekeo wa kiroho.

'' Nitakapoinuliwa juu, nitawavuta wengi kwangu'' Yesu
Sio '' Mtakapoinua tamaduni za kipagani juu na kuzihusianisha na mimi, wengi watakuwa wakristo'' human opinions.

hatuwezi kuwazidi akili mitume katika hili maana ni jambo sensitive sana. Wangekuwa pioneer wa xmass.
hili litabaki kuwa hekima za wazee na tamaduni za kiimani ila halina baraka za maandiko.
Sisi kwetu Yesu ni MUNGU/MTU, hivyo linakukumbukwa tukio la kuzaliwa Yesu na si kama kitoto tu, bali mfalme na mwokozi aliyekuja kutuwezesha kuishinda dambi/shetani.
 
hivyo unakubaliana na mimi kuwa umwilisho ni fundisho la imani kwa sababu imani yote chanzo chake ni biblia hivyo ni la biblia pia au bado unapinga ??? na kusimamia msimamo wako kuwa sio fundisho la imani ila ni biblia ?
kama bibilia imesema na kufundisha. Ikatokea imani flani ya kidini ikalicompile kama fundisho lao. Litabaki kuwa fundisho la Bibilia kama msingi mkuu. Ila Likichanganyana na hekima yoyote ya kibinadamu nje ya bibilia fundisho hilo linakuwa limenajisika.
huo ndio msingi wa hoja yangu mkuu.
 
"KUNA MSEMO WA KISWAHILI UNAOSEMA, "MWANAFUNZI HAMPITI MWALIMU WAKE" Mwisho utajua kuwa kanisa katoliki ndilo baba wa theolojia na mafundisho yote ya imani za Ukristo.


Katika hili nakaa kimya Nachukua mafundisho ya Mwl. wangu wa Maandiko Matakatifu Pd. Titus Amigu kama yalivyo na kuwapa katika maandalizi ya kusherekea Krismasi hii 2018.

TAREHE YA KUZALIWA KWA KRISTO
Nimeombwa nifafanue tarehe ya kuzaliwa Yesu Kristo kama ni kweli ni tarehe 25 Desemba au la.
Lakini kwa ajili ya kuwekana sana nimeyagundua maswali mawili yanayoweza kufuata baada ya kujibu swali hili la msingi. Ndiposa nimeambatanisha majibu kwa maswali hayo ya nyongeza. Swali moja ni kwa nini tunaadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo kila mwaka na lingine ni Yesu alitungwa mimba lini. Nifuatilie.
Nitaanza kujibu swali la kwa nini tunaadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo kila mwaka, kisha nitajibu swali la tarehe ya kuzaliwa Yesu Kriisto na kumalizia na swali la Yesu alitungwa mimba lini. Mpangilio huu unasababishwa na mantiki ya majibu yenyewe.

1. Kwa nini tunaadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo kila mwaka?
Najibu kifupi. Tunaadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo kila mwaka kwa ajili ya kujichumia faida zake ya kiroho na maadhimisho yenyewe si suala la kumzalisha Yesu tena na tena isipokuwa kuliishi upya tukio hilo kila mwaka. Hivi, tunapoadhimisha Krismasi si kwamba Yesu Kristo anazaliwa upya kila mwaka, isipokuwa tunakumbuka upya kuzaliwa kwake. Ni kumbukumbu (anamnesis).
Narudia, tunachofanya si kumzalisha upya Yesu Kristo kila mwaka isipokuwa ni kuliadhimisha tukio upya au kulikumbuka upya tukio (anamnesis). Tukio hilo lilikuwa muhimu kwa vile mtoto aliyekuwa anazaliwa alikuwa anakuja kuwa shujaa wetu.
Haiwezekani kumzalisha Yesu kimwili kila mwaka na ndivyo isivyowezekana kwa binadamu yeyote. Yesu alikuwa Mungu - Mtu lakini alikuwa mwanadamu kweli na siyo mcheza « Ze comedy » fulani. Kwa ukweli huo, bila shaka, tunajua wote kwamba Yesu, kama binadamu wa kweli, alizaliwa hapa duniani mara moja tu. Aghalabu, tunajua kwamba Yesu hatazaliwa tena na ndiyo kisa tunasubiri kurudi kwake mara ya pili kwa vindumbwendumbwe vya kiyama, ufufuko wa wafu na hukumu ya pili kwa kila mwanadamu. Kwa hilo, tumetahadharishwa wote tukae chonjo: tukeshe usiku na mchana, tujiandae kwa kuishi kwa imani isiyo na mawaa na utendaji wa kiadilifu huku tukiikimbia dhambi kama ukoma.

Kumbe, kuadhimisha tukio upya au kulikumbuka upya tukio siyo KULITUKIZA upya tukio. Acha nikupeni mifano miwili. Kuadhimisha upya tukio la uhuru wa nchi au kukumbuka upya siku ya kupata uhuru si kupata uhuru kwa mara nyingine. Kuadhimisha upya tukio la kufunga ndoa au kukumbuka upya siku ya kufunga ndoa si kufunga ndoa kwa mara nyingine.Vivyo hivyo, kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo fulani si kumzalisha upya.
Si siri, Noeli au Krismasi ni siku ya kuzaliwa shujaa wetu. Siku ya kuzaliwa Mkombozi ni karibu nusu ya ukombozi wenyewe. Au sivyo? Ndiyo kisa basi, furaha haiwezi kuzuiliwa na mtu yeyote wala kwa sababu yoyote. Ni lazima kuifurahia sikukuu ya mtu wa maana hivyo. Mtu asiyeweza kuifurahia siku kama hiyo kuna mawili: ama ni mwendawazimu asiye na habari na mambo ya maana duniani au ni mfanyakazi wa kwenye kiwanda cha sumu. Vinginevyo, mtu mwenye akili timamu na anayefanya kazi za kawaida za kibinadamu sharti afurahi sana.

2. Tarehe ya Kuzaliwa Yesu

i. Tarehe ya Kiblia Ipo
Ili kukata maswali yafaa tuanzie masafa haya. Watu wengine huhaha huko na huko kutafuta tarehe aliyozaliwa Yesu wakati imeandikwa waziwazi kwenye Maandiko Matakatifu. Imeandikwa, usinibishe. Luka anataja tarehe ya kuzaliwa kwa Yesu waziwazi, ilikuwa ni mwaka ule Kaisari Augustino alipotangaza sensa, yaani ile sensa ya kwanza katika enzi za ugavana wa Kwirinus huko Siria.
Imeandikwa: “Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto kuwataka watu wote nchini kote wahesabiwe. Sensa hiyo ilikuwa mara ya kwanza, wakati wa Kwirinus alipokuwa gavana wa Siria. Basi, wote waliohusika walikwenda kuhesabiwa kila mtu katika mji wake. Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazareti mkoani Galilaya, na kwa vile alikuwa wa jamaa na ukoo wa Daudi, alikwenda mjini Bethlehemu mkoani Yudea, alikozaliwa mfalme Daudi. Alikwenda kuhesabiwa pamoja na mchumba wake Maria ambaye alikuwa mjamzito. Walipokuwa huko, siku yake ya kujifungua ikawadia, akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni” (Lk 2:1-7). Umeilewa tarehe hiyo?
Sisi tunaweza kubabaika sana juu ya tarehe hii, kumbe kwa watu wa wakati ule, tarehe hii ilikuwa wazi kama mchana. Ilikuwa ni sawa na kusema huku kwetu, mtoto huyu alizaliwa mwaka ule lilipofunguliwa daraja la Kigamboni, Mheshimiwa Paulo Makonda alipokuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Rais John Pombe Mgufuli. Kwetu tarehe hii ni wazi kabisa, yaani mwaka 2016, lakini baada ya karne nyingi kupita tarehe hii iliyo wazi inaweza kuwa jambo la kubishaniwa sana.

Jambo hili si geni kwetu sisi Waafrika. Anayestaajabu anatustaajabisha wenzake. Waafrika hatukujua kusoma wala kuandika. Hatukuwa na kalenda yenye kueleweka. Hivi si haba Waafrika ambao wakiwauliza wazazi wao tarehe walipozaliwa wanaambiwa mathalani, “Ulizaliwa mwaka wa neema kubwa ya maboga alipotutembelea mjomba wako”. Au “Ulizaliwa mwaka wa nzige wengi nasi tufikwa na njaa kali sana” na kadhalika. Ajabu iko wapi?
Kumbe, sisi sote tukipekua na kutaka kujua tarehe kamili ya kuzaliwa Yesu, kama aliyotuandikia Mwinjili Luka, tunaishia kupata kizunguzungu na kubishana tu. Hata hivyo, duniani si wote tunaoshindwa hesabu. Kumbe, zamani zile, kwa misingi ya tarehe ya kuzaliwa Yesu, Wakristo walishatengeneza kalenda.

ii. Tatizo la Kalenda ya Dunia
Lakini katika kuitumia kulitokea haja ya kuirekebisha. Watu wa kale waliikalia chini kalenda yao. Katika kuirejea wakagundua mushkeli fulani. Waliona kulishafanyika makosa ya miaka minne au sita hivi, yaani kwamba kalenda yao ilitindikiwa miaka minne au sita hivi.

Kasoro hiyo waliigundua pale walipopambanisha miaka ya utawala wa Mfalme Herode Mkubwa na Yesu.
Waliona wameanzia kuhesabu kwenye mwaka wa mbele zaidi wakati walitakiwa kuanzia nyuma miaka minne au sita hivi. Waligundua kwamba walipaswa kurudisha nyuma miaka ya kuzaliwa Yesu hadi ikutane na utawala wa Mfalme Herode Mkubwa. Maana yake kwa kadiri ya kalenda yao, Kristo alizaliwa mapema kuliko mwaka ule iliposemekana kwa ujumla kwamba alizaliwa.

Udadisi wao ulianzia kwenye matumizi ya jina “augustus” linalotajwa na Luka katika 2:1-7. Kumbe, jina hilo ‘augustus’ lenye maana ya “mheshimiwa” kwa Kilatini, ni jina ambalo Gaius Octavius alijipa mnamo 27 K.K. Huyu alikuwa mtawala wa Dola ya Rumi, yaani Kaisari (Mfalme) tangu 31 K.K. mpaka 14 B. K. Na tena, Herodi Mkubwa anayetajwa kutaka kumuua Kristo, alikufa mnamo mwaka 4 K.K. Hivi kuipanga kalenda yao kwa kusema, Yesu alizaliwa mwaka 1, kwa pale walipoanzia hesabu zao, yaani mwaka wa kuanza mji wa Roma, ilimaanisha kuzisahau tarehe hizi muhimu. Wakawa wameisahau miaka minne au sita nyuma.
Walijilaumu kwa kosa hilo kwani iliwapasa wakati ule ule kurudi nyuma kwa miaka michache, ili Yesu azaliwe kabla Herode Mkubwa hajafa. La sivyo, uadui wao usingelikuwapo.

Kwa maelezo haya ya kosa walilofanya wapanga kalenda wa awali zile, mwaka huu 2016 ulipaswa uwe mwaka 2020 au 2021 au 2022. Kwa vyovyote, licha ya kuligundua kosa hilo la miaka minne au sita waliiacha kalenda yao iendelee. Na ndiyo kalenda inayoendelee hadi leo hii. Hii ndiyo kalenda iliyotupatia mwaka huu kama mwaka 2016 na hivi karibuni tutaingia mwaka 2017 badala ya mwaka 2021, 2022 au 2023. Si kitu, twende tu.
Mwenye ubavu wa kiakili, atusaidie kujenga kalenda mpya. Kama unaweza wewe kuitafsiri tarehe aliyozaliwa Yesu na kuipangia kalenda kamilifu jaribu! Lakini nadhani itakuwa kazi isiyo na tija yoyote. Zaidi ya hayo, tusahihishe kalenda leo kwa faida gani au kwa faida ya nani? Acha tuendelee tu!

Je, mnastaajabu? Msistaajabu. Basi, tangu zamani kulikuwa na ugumu wa kupata mwaka aliozaliwa Yesu, sembuse siku na saa. Lakini, pamoja na ugumu huo wa kupata mwaka, mwezi, tarehe na saa kamili alipozaliwa Yesu, ni ukweli usiopingika kwamba, Yesu alizaliwa kama mtu. Ukweli huu hautegemei kujua kwetu mwaka, mwezi, siku na saa. Ni ukweli wa milele,

iii. Hitaji la Kusherehekea Kuzaliwa kwa Mkombozi
Tunaambiwa kwenye Biblia kwamba siku yoyote aliyoifanya Bwana lazima tuisherehekee na kuifurahia. Siyo siku kama siku isipokuwa kile kilichofanywa na Bwana. Unabisha? Bila shaka utanibisha mimi kwa vile hujishughulishi na usomaji na upembuzi wa Maandiko Matakatifu. Basi, kama huna habari imendikwa kwa wino mweusi hivi: “Hii ndiyo siku aliyoifanya Mwenyezi Mungu, tuishangilie na kufurahi” (Zab 118:24). Ndipo likaja swali tusherehekee lini kuzaliwa kwa Mwokozi wetu au kufufuka kwake? Tukio la kuzaliwa kwake ni la thamani kubwa!

iv. Uamuzi wa Utamadunisho
Lakini hapa tuongelee tarehe ya tukio la kuzaliwa tu. Hilo la kufufuka tuliweke pembeni. Kama unakubaliana nami kwa ushuhuda huo, lilibaki deni la kuzipata siku za Mungu, na hapa hiyo siku aliyozaliwa Bwana wetu ili tuishangilie na tuifurahie. Jiulize, haki na wajibu huo tungalitimizaje bila kuitafuta siku aliyozaliwa Yesu Kristo?
Basi, kwa haki waamini walitafiti tafiti mazingira yao, kwa akili waliyokirimiwa na Mungu, ili kupata siku moja waamini wapate kusherehekea kuzaliwa Yesu Kristo. Mwishoni mwa tafiti yao, wakaigundua siku ya kufaa, ndiyo tarehe 25 Desemba. Hivi, kifupi, hii haina maana kuwa 25 Desemba ndio siku kamili alipozaliwa Kristo, ila imewekwa hapo kwa sababu za kihistoria na utamadunisho uliohalalishwa. Tena ingeweza kuwa tarehe nyingine yoyote kwa sababu HATUADHIMISHI SIKU bali TUKIO LA KUZALIWA YESU. Tuelewane hapa. Hatuadhimishi tarehe 25 Desemba isipokuwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Kwa kuwa tunababaishana sana hapa duniani, yafaa leo tupitie historia hiyo japo kifupi. Hata hivyo, kwa kuwa ninayotaka kukueleza hapa yatahusisha namba na hesabu hesabu, jiandae kwa kukishikilia kichwa chako vyema kisije kikaanza kushika moto na kuwaka kwa maumivu yasiyotibika kwa dawa ya maumivu ya dawatatu. Naomba tufuatane kwa karibu sana.
Ni hivi, katika siku za mwisho za dola ya kipagani ya kirumi, ibada za kuabudu jua zilikuwa zikifanyika sana. Mjini Roma dini ya Mithras, mungu - jua wa kiajemi, ilistawi sana. Kaisari Aureliani akajengesha hekalu la jua lisiloshindika, mnamo mwaka 274. Sikukuu kubwa ya mungu - jua, ilifanyika kila tarehe 25 Desemba, siku ambayo tabia ya kupungua pungua kwa mwanga wa jua ilikoma, na hivyo kuanza kuongezeka tena. Yaani, ilikuwa kama siku ya kuzaliwa upya jua. Na tangu tarehe hiyo, siku zilianza kuwa ndefu tena.

Mambo haya ya kupungua na kuongezeka kwa mwanga wa jua, ndiyo yanayotokea huko Ulaya kila mwaka hadi leo hii. Basi, sikukuu hiyo ya jua iliitwa siku ya kuzaliwa jua lisiloshindika, maana ijapo mwanga ulikuwa ukipungua, jua lilikuwa halifi kabisa.
Tangu siku za Kaisari wa kwanza mkristo, Kostantino, tarehe ya sikukuu ya mungu - jua ikafanywa sikukuu ya kuzaliwa Bwana Yesu Kristo, Mungu asiyeshindika kweli badala ya jua, kiumbe chake mwenyewe. Wayahudi walishindwa kummaliza Yesu, alifufuka mzima. Tunajua kwamba hata jua halikupata kuwako bila NENO (Yn 1: 1- 3).
Tukisoma Kalenda ya Mashahidi iliyotengenezwa na Philocalus mnamo mwaka 354, tunaweza kuona kwamba, sikukuu ya kwanza ya Krismasi ilisherehekewa mwaka 336 huko mjini Roma. Katika kalenda hii, Krismasi iliwekwa mwanzoni mwa mwaka wa liturujia.

v. Sababu Tatu za Tarehe 25 Desemba
Yaonekana kulikuwa na sababu tatu zilizosababisha kuwekwa kwa sikukuu ya kuzaliwa Bwana hapo 25 Desemba.

Mosi, mkazo wa kiteolojia kwenye kitendo cha Yesu kujifanya mtu, kujimwilisha, yaani kuadhimisha kanuni ya imani ya Nicea (mwaka 325) kimatendo na kikamilifu zaidi. Ni kanuni hii ya imani na si ile fupi ya mitume, iliyokazia fumbo la Yesu kujifanya mtu kama sisi.

Pili, kumtambua Kristo kama mwanga wa kweli, jambo linalosemwa na Mal 4:2. Basi, Kaisari Kostantino hakuona ni vibaya sikukuu ya Yesu aliye mwanga, ikichukua nafasi ya sikukuu ya mungu - jua, kwa vile mwenyewe alikuwa mwabudu jua hapo mwanzo kabla hajabatizwa.

Tatu, ujenzi wa kanisa la Mt. Petro pale Vatikani. Ujenzi wa kanisa hilo ulikuwa mgumu. Kwa nia ya kujenga juu ya kaburi la Mt. Petro, ilipasa watu wabomoe nusu mlima. Na hapo karibu na kaburi kulikuwa na altare ya mungu - jua, ambayo nafasi yake ilichukuliwa na altare ya kutolea sadaka ya kweli ya Bwana wetu Yesu Kristo.

vi.Krismasi Ilichelewa Mashariki
Kwa upande wa mashariki mwa dunia iliyojulikana wakati ule sherehe ya Krismasi ilifika baadaye kidogo:
- Siria kati ya 363 na 373 kwa ushuhuda wa nyimbo za Ephrem,
- Kostantinople mnamo 380 ambapo Gregory wa Nazienzi alihubiri kwamba Krismasi ni matukio ya Bwana kujifanya mtu na kuzaliwa kwake, taarifa ya malaika kwa wachungaji, kutolewa Bwana hekaluni alikokutana na Simeon na Anna na kutembelewa kwake na mamajusi. Gregory alihubiri kwamba, Tokeo la Bwana maana yake hasa ni Ubatizo wa Bwana, mwanga wa dunia.
- Antiokia, Krismasi ilianza mwaka 386, Misri mwaka 432, Yerusalemu kati ya 424 na 458, n.k.

vii. Tarehe Tofauti Tofauti
Kutokana na migogoro ya kihistoria, makanisa ya magharibi yameachana njia na makanisa ya mashariki. Makanisa hayo ya mwanzo hutenganisha Krismasi (25 Desemba) na Tokeo la Bwana (6 Januari), wakati yale ya mashariki, yaani makanisa ya kiorthodosi husherehekea yote bila kutenga kila tarehe 6 Januari.
Kifupi, tarehe ya kuadhimisha katika Kanisa la Magharibi na baadhi ya Makanisa ya Mashariki pamoja na walimwengu wengine ni tarehe 25 Desemba. Lakini katika baadhi ya Makanisa ya Mashariki huadhimishwa tarehe 7 Januari. Na katika makanisa ya Kiarmeni huadhimishwa tarehe 6 Januari.

Mgawanyiko huu ni wa watu. Biblia inasema kimoja tu kwamba, Kristo alizaliwa (rej. Lk 2:1-7) na akawaletea watu utukufu wa Mungu. Tarehe si jambo la kukosea usingizi. Unabisha? Unabisha nini? Hivi, ikiwa hujui siku aliyozaliwa babu wa babu yako inamaanisha hakuzaliwa na hakuwapo? Usitake nicheke ukayaona mapengo yangu mie!

viii. Je, Tarehe ni Muhimu Sana?
Tujiulize sote. Hivi, hatuwezi kumwamini Kristo mpaka tujue alizaliwa lini? Je, tunaweka kumbukumbu za tarehe za matukio yetu muhimu? Je, tunazo sikukuu zo zote za kale ambazo tunaweza kuzitamadunisha kwa kupisha sikukuu za kikristo? Je, viongozi wetu wakristo wanaweza kutusaidia nini katika kupanga liturujia yetu? Kaisari Konstantino aliwasaidia sana wakristo wenzake. Tunapowaombea viongozi wetu wajali dini zetu tunataka wafanye nini? Tunataka wasifanye chochote? Mbona Konstantino alifanya na sasa analaumiwa?

3. Tarehe ya Kutungwa Mimba Yesu Kristo
Baada ya kulijibu swali la tarehe ya kuzaliwa Yesu Kristo, nadhani sasa tunaweza kujibu swali dogo zaidi, “Bikira Maria alipata mimba lini?” Kwa maneno mengine swali dogo ni Yesu alituungwa mimba lini?
Pasipo mashaka yoyote, kwa vile Yesu alikuwa mwanadamu halisi, alichukuliwa kwenye mimba kama mwanadamu halisi yaani kwa miezi tisa vile vile. Biblia inataja tarehe ya kutungwa kwake sawia na tarehe ya kuzaliwa kwake.
Hata hivyo, tarehe ya kutungwa mimba ya Yesu Kristo kumetajwa kwa tarehe inayotupasa kuielewa vyema. Biblia inatuambia ilikuwa ni mwezi wa sita, malaika Gabrieli alipotumwa kumwendea mwanamwali Bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo lilikuwa Mariamu (rej. Lk 1:26-27).
Hata hivyo, mwezi huu wa sita si kwa hesabu za kuanzia mwanzoni mwa mwaka, isipokuwa kwa hesabu ya ujauzito wa Elizabeti, mke wa mzee Zakaria. Aya 26 inaendeleza yaliyosemwa kabla yake yaani kwamba Elizabeti alipata mimba yake uzeeni (rej. Lk 1:23-25). Hivi basi ni mwezi wa sita kwa mimba ya bi mkubwa huyo na si mwezi wa kizungu Juni.
Watu wanapoelewa mwezi wa sita kuwa mwezi wa kizungu Juni, hushikwa na homa wanapoona Wakristo wakisherehekea kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo mwezi Desemba. Hao huchanganyikiwa kwa mikokotoo ya hesabu zao batili kwa kiasi kile zilivyoegemezwa kwenye mwezi walioukosea.
Wachache hawaiendi mbali ya kuajabia. Lakini wengine hudhani, kwa kituko hicho kwamba Yesu alizaliwa “njiti”. Na hapo ndipo wengine huenda kwenye kosa kubwa zaidi la kudai Yesu alikuwa mtu wa pekee kwa vile alikaa tumboni mwa mama yake kwa miezi pungufu na bado akazaliwa vyema na kukua vyema.
Huko kote ni kukosea. Yesu alitungwa mimba na kukaa tumboni kama watoto wa kawaida wa wanadamu. Kwa kuwa tarehe ya 25 Desemba ni mapato ya utekaji sikukuu ya kipagani, kwa akili, ndio utamadunisho (rej. Mt 22:37), kusudi siku ya Mungu-jua wa wapagani itumike kumtukuzia Mungu Jua wa kweli yaani Yesu Kristo (rej. Yn 1:5-9), kutungwa kwake huadhimishwa kimahesabu nyuma, tarehe 25 Machi, ndiyo sikukuu ya Kupashwa Habari Bikira Maria. Tangu tarehe 25 Machi hadi 25 Desemba ni miezi tisa kamili. Hii ndiyo mantiki ya utamadunisho wa Kikristo.

Je, Kutamadunisha Kitu ni Halali?
Ni halali kabisa. Wapo wanaokasirika na kufoka kwa nini Wakristo walichukua tarehe ya wapagani, 25 Desemba kusherekea jambo la Kikristo. Watu kama hao ni wasahaulifu tu, usiwajali. Utamadunisho ni uchukuaji wa kitu fulani, kukipa maana mpya au nzuri zaidi na kukitumia. Wakristo hawawezi kukataa mambo ya wapagani wala wapagani hawawezi kukataa mambo ya Wakristo. Dunia ni moja, tunashirikishana. Wakristo hawana uwezo wa kuvumbua kila kitu chao. Tena hawapo Wakristo wa kanisa lolote waliovumbua vyote wanavyovitumia wenyewe. Asikudanganye mtu.
Kumbe, wanachogundua upande mmoja wa dunia, wewe wa upande mwingine unaweza kukichukua na kukitumia kwa manufaa yako. Cha wapagani kinaweza kutamadunishwa na Wakristo wakakitumia, na cha Wakristo kinaweza kuchukuliwa na Wapagani wakakitumia. Usinibishe.
Yafuatayo ni mambo ya uvumbuzi wa wapagani nasi tunatumia tena kwa furaha kabisa. Labda hatujui. Suruali, viatu, miwani, kioo, herufi, hesabu, kusoma na kuandika, matibabu ya hospitali n.k. Kama wewe ni mmoja wa wale wasiotaka kabisa mambo ya wapagani, usivitumie vitu hivi kuanzia kesho.

Huenda majibu haya yamekuzidi urefu. Lakini yasome moja moja kwa umakini mkubwa kama unataka kuujua ukweli. Kuyasoma majibu haya kwa umakini ndiyo gharama ya kujua tarehe ya kuzaliwa Bwana Yesu.
NAWATAKIENI NYOTE MAANDALIZI MEMA YA SIKUKUU YA KRISMASI. KILA LA HERI NYOTE!

(Kwa hisani ya Pd. Titus Amigu aliyetoa mafundisho haya)
Hiki ni kitu kinaelewa kiujanjaujanja na misemo mingi ili kuchanganya watu. Mnatumia maneno kama vile fumbo la Imani. Hii ni tarehe ya kipagani tangu zamani sana, ndio tarehe kalizaliwa kale kajamaa kanatokoonekana kwenye sanamu kamebebwa kwenye sanamu na kudanganywa kuwa ni mtoto Yesu, Yule siyo Yesu ni hako katoto ka siku nyingi huko nyuma, kalikuwa kana abudiwa na warumi wa kipagani. Sasa ili kaendelee kuabudiwa mnasema ni Yesu. Ni Uongo. Xmas siyo jambo la kiblia ni mojawapo ya sherehe za kipagani kabisa.Kwenye Biblia ni wapagani waliokuwa wakisherehekea siku zao za kuzaliwa
 
mkuu lugha ya kanisa tena???
kanisa Lipi???
maana lilikoanzia(Kanisa la Kwenye Bibilia) hakukuwa na ulatini wowote?
Ila nakuelewa maana hiyo itaingia katika makundi yale mawili unayoyatumia kama authority yako ya kidini ( mapokeo nje ya bibilia na matamko ha kikanisa lako)

unaniuliza kuhusu lugha ya kanisa ??
nilidhani huo ujuaji wako juu ya kanisa katoliki hasa historia ungekusaidia kujua walau kuwa kanisa kama TAIFA LA MUNGU lina lugha yake rasmi.

endelea kufukua ivoivo utaelewa mengi tu

nafikiri sasa umeanza kunielewa
 
Sisi kwetu Yesu ni MUNGU/MTU, hivyo linakukumbukwa tukio la kuzaliwa Yesu na si kama kitoto tu, bali mfalme na mwokozi aliyekuja kutuwezesha kuishinda dambi/shetani.
Yesu sio Mungu/Mtu weka maelezo vizuri.
Alikuwa Mungu.
akawa Mungu katika ubinadamu, baada ya Kumaliza mission yake leo tunapoongea ni MUNGU 100% hakuna cha Mungu mtu.
Kumsherekea kama ameanzia pale kwenye banda la ng'ombe ni mtazamo mfinyu wa Mungu. Maana Bibilia inasema alichinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, maana yake maamuzi ha kifo chake ni ya kitambo tu hata kabla ya dunia kuumbwa.
Mitume kwa kujua hilo hawakuanzisha sikukuu kama hizo, bali walijikita daily kuwa naye moyoni. Hiki ndicho kinachosisitizwa na bibilia, walikuwa nanuwezo wa kucopypaste hekima na sikukuu za kipagani maana wazee wa kiyahudi waliwahi kufanya hayo ila walidumu katika hekima walizopewa na Yesu. Ila sisi mitume wa baadae naona tumekuja na ubunifu mpya.
 
reasoning yako nzuri imeruka baadhi ya maelezo yangu na ninacjosisitiza.
Huwezi kuyumia GIZA (upagani, uzushi na uongo) kusambaza ukweli wa kuhusu kristo wa watu waliogizani.
Unatumia NENO ambalo ni taa kwa walio gizani.
Kutumia sikukuu za kipagani ili uwafurahishe na kuwavuta wapagani kutoka gizani ni kinyume na fundisho la Yesu.
TRUTH (not pagan traditions and human wisdoms) will set sinners and those who are in darkness free.
Hahahh..! Nacheka si kwa kukucheka bali kwa namna ambayo unajilazimisha kutoelewa, na aulewi kwasababi labda hujasoma maana hekima/maarifa/elimu ya Mungu anawapa wenye kinyenyekea.

Labda ni nikuulize ni tukio gani ambalo linatajwa na biblia kuhusu kuzaliwa Yesu linapindishwa kwa kuachwa na kufuata huyo Mungu jua, kilichofanyika ni kufuta upagani na kutangaza wokovu/Ukristo sasa logic ya kuwa kutamadunisha upagani ni ipi??
 
Hiki ni kitu kinaelewa kiujanjaujanja na misemo mingi ili kuchanganya watu. Mnatumia maneno kama vile fumbo la Imani. Hii ni tarehe ya kipagani tangu zamani sana, ndio tarehe kalizaliwa kale kajamaa kanatokoonekana kwenye sanamu kamebebwa kwenye sanamu na kudanganywa kuwa ni mtoto Yesu, Yule siyo Yesu ni hako katoto ka siku nyingi huko nyuma, kalikuwa kana abudiwa na warumi wa kipagani. Sasa ili kaendelee kuabudiwa mnasema ni Yesu. Ni Uongo. Xmas siyo jambo la kiblia ni mojawapo ya sherehe za kipagani kabisa.Kwenye Biblia ni wapagani waliokuwa wakisherehekea siku zao za kuzaliwa
2 peter 2: 2 Many will follow their depraved conduct and will bring the way of truth into disrepute. 3 In their greedthese teachers will exploit you with fabricated stories. Their condemnation has long been hanging over them, and their destruction has not been sleeping.
 
Hahahh..! Nacheka si kwa kukucheka bali kwa namna ambayo unajilazimisha kutoelewa, na aulewi kwasababi labda hujasoma maana hekima/maarifa/elimu ya Mungu anawapa wenye kinyenyekea.

Labda ni nikuulize ni tukio gani ambalo linatajwa na biblia kuhusu kuzaliwa Yesu linapindishwa kwa kuachwa na kufuata huyo Mungu jua, kilichofanyika ni kufuta upagani na kutangaza wokovu/Ukristo sasa logic ya kuwa kutamadunisha upagani ni ipi??
tatizo watu wanaojiita Bigmind huwa wanadhani wanaelewa mapema lkn mara nyingi wanasumbua.
zile ni sikukuu za kipagani zilizovalishwa koti zuri la ukristo.
maneno mazuri yakifilosofia uliyoyaleta ni kupiga pasi koti hilo hakuna jipya
 
Yesu sio Mungu/Mtu weka maelezo vizuri.
Alikuwa Mungu.
akawa Mungu katika ubinadamu, baada ya Kumaliza mission yake leo tunapoongea ni MUNGU 100% hakuna cha Mungu mtu.
Kumsherekea kama ameanzia pale kwenye banda la ng'ombe ni mtazamo mfinyu wa Mungu. Maana Bibilia inasema alichinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, maana yake maamuzi ha kifo chake ni ya kitambo tu hata kabla ya dunia kuumbwa.
Mitume kwa kujua hilo hawakuanzisha sikukuu kama hizo, bali walijikita daily kuwa naye moyoni. Hiki ndicho kinachosisitizwa na bibilia, walikuwa nanuwezo wa kucopypaste hekima na sikukuu za kipagani maana wazee wa kiyahudi waliwahi kufanya hayo ila walidumu katika hekima walizopewa na Yesu. Ila sisi mitume wa baadae naona tumekuja na ubunifu mpya.
Ninacho zungumza uelewi maana akili yako umeiset kufanya league/mabishano kwangu sijawahi na sitawahi kubishana au kujifanya kumwelezea Mungu. Ninachojua Yesu ni mtu katika hali ya kusema yeye ni njia na atakayetaka kwenda kwa baba lazima amfuate kwa maana Yesu katika fumbo la umiilisho/kuuvaa mwili hapa nikiwa na Yesu nayaweza magumu ya ubinadamu. Yesu ni kielelezo cha utu wa binadamu ukifikiria uzima wa milele na si kama unavyodhani na kutafsiri kama Mungu/mtu wewe na mimi.
 
Back
Top Bottom