Desemba 25: Je, ni siku aliyozaliwa Yesu au twaadhimisha tu kumbukumbu?

Kinachowauma watu ni kufungamanisha upagani na mambo ya kimungu, hili ndio tatizo
 
Kwanj petro alikua anaongea kiswahili
Petro akuongea kiswahili, aya na mimi nijibu swali langu Petro aliwai angalau mara moja kuadhimisha hii official day 25/December kuwa kumbukumbu ya mazazi ya Yesu?
 
Bora zetu za kuzaliwa enzi za nzige maana utajua ilikuwa ni masika na sio mwaka
Sijui kuna mtu kanielewa
 
petro alikutuma ukabadili verse za vitabu vyake kama iyo 2 petro 2:3 toka KIGIRIKI kwenda KIINGEREZA/KISWAHILI au huo utaratibu ulijitungia mwenyewe ??

petro alikutuma ukacompile vitabu na maandiko yake kisha uyaweke kwenye kitabu kinaitwa BIBLIA au huo utaratibu ulitungia mwenyewe ??

mlolongo wa mambo uliojitungia mwenyewe ni mrefu sana. mengine unaweza ongeza mwenyewe.
 
naona umeibuka na nadharia za kikatoliki.
"There is in them no evidence whatever to suggest that it was the expectation of the writers that what they had written would one day be gathered together to become a part of the New Testament." (Campaigners for Christ Handbook, p. 162).

2 Timotheo 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

Hata kama yangekuwa vipandevipande tungeyasoma. Hata kama Yasingekusanywa pamoja ningeyakusanya mimi leo na kutengeneza app kulingana na current technology wala sio jambo la kujivunia au swali la kuuliza.

maoni ya wananzuoni wa imani yako naona yamekukaa kuliko hata Maandishi wazi ya maandiko.
 
Kinachowauma watu ni kufungamanisha upagani na mambo ya kimungu, hili ndio tatizo
nyie msiofungamanisha endeleeni,acheni watu wafanye mambo yao na nyie fanyeni yenu mbinguni kila mtu anakwenda mwenyewe,tangu mmeanza hili zoezi mshapata wangapi????😀😀😀😀 mnachekesha kweli
 
maoni ya wananzuoni wa imani yako naona yamekukaa kuliko hata Maandishi wazi ya maandiko.
mwanazuoni wangu mkuu ni Yesu kristo mwenyewe na baadae ni mitume 12 aliopenda waendeleze kazi yake hapa duniani kisha wakifuatiwa (succesors) na wazee(maaskofu) kuanzia holy father (pope) st peter mpaka pope francis kisha wafuasi wengine wengi wa kristo kuanzia karne ya kwanza kabisa mpaka sekunde hii unaposoma hii post. HAO NDIO WANAZUONI WANGU MIMI ONESHA WA KWAKO SASA.
naona umeibuka na nadharia za kikatoliki
nawe ibuka na panguzi kwa kutumia nadharia za kisabato. na ukimaliza ulete ushahidi wa kimaandiko wa mambo lukuki ambayo umejitungia (kinyume kabisa na 2 peter 2:3) ukianza na niliokuonesha hapo juu

imeandikwa
Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.
 
Asante kwa maoni yako kuhusu Yesu. Hata wafuasi wa Kibwetere walikuwa na kauli hizohizo hadi siku wanajikuta majivu.

Msaada tu kidogo.
Petro hajawahi kuwa papa. Ukatae ukubali haibadilishi huu ukweli. Hayo ni mapokeo na makaririsho ya imani tu.
Kumuita huyo Papa Holy father ni Kufuru kwa Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi na Kumdharau Yesu na Mafundisho yake.
Mimi Yesu sio Mwananzuoni wangu Bali ni Mungu wangu, Bwana na Mwokozi wangu aliye Hai.
Maneno Yake, Kupitia Maandiko matakatifu Mwanzo hadi Ufunuo, Vitabu 66 aliyoyanena kupitia mawakala wa kibinadamu ndio Mwanzo na Mwisho wa wananzuoni wangu.
Nadhani unajenga hofu na wasiwasi na EGW, Hata Yeye sio mwananzuoni wangu ila ni mtumwa mwenza wa Yesu na anasema

“He [Christ] pointed to the Scriptures as of unquestionable authority, and we should do the same. The Bible is to be presented as the word of the infinite God, as the end of all controversy and the foundation of all faith” (COL 39, 40).
'' Yeye Yesu alielekeza katika Maandiko kama mamlaka isiyokosolewa, na sisi tunapaswa kufanya hivyohivyo. Bibilia inapaswa kuchukuliwa kama neno la Mungu asiye na ukomo, na Mwisho wa migogoro yote na misingi ya imani yote''.
Mwananzuoni yoyote anapaswa kupigia magoti Neno la Mungu maoni yake yote lazima yafungwe katika Bibilia.
Siamini kama wewe kuwa hata kauli ya Papa inauzito sawa na Bibilia, Tamko la kikanisa linauzito sawa na Bibilia. Kwaku Kuamini hayo ni ukafiri. Siku Papa akiingiwa na Shetani kama Petro dakika chache Baada ya Kusifiwa na Yesu kwa Kumtambua na kutoa tamko la kishetani na Yesu akamwambia '' Rudi nyuma wewe Shetani''. kwa Imani yako wewe na kanisa zima la katoliki hamtakuwa na Jinsi itabidi mpigia magoti hiyo kauli na kuifuata. Yesu hawezi kuhatarisha maneno yake kizembe hivyo. Msingi Ni Bibilia, Sio hao watu mashuhuri wa imani na matamko yao.

Angalia Ndugu yangu Sala na Kazi, pamoja na Yeyete atakayependa. Umejiweka kwenye hatari Kubwa ya Kupotezwa na Mwovu shetani kwa Kitoboa Ufunuo wa Yohana na kukubwisha matamko na kauli za mitume wako wa .com kuwa na uzito sawa na Maandiko Matakatifu.

Mambo haya nitaendelea kusema, kuonya na kufundisha hadi utimilifu wa dahali. Maana ni Kweli na hakika.

Mfano Mdogo tu.
Unaposema Petro ni Papa wa Kwanza, Kwa Nini Yohana asiwe papa wa pili maana ndiye mtume wa Mwisho kufa kwa mujibu wa masimulizi. Badala Yake mmempa Upapa wa Pili Baada ya Petro St Linus. Na Andiko lwa wananzuoni wako hao Catholic Encyclopedia (1913) Vol 9 inasema haina uhakika kama Linus huyo ndio wa kwenye bibilia (Kitabu cha timotheo) au ni mtu mwingine?
 
hao wafuasi Wa kibwetele hawana tofauti yeyote kabisa na wale wafuasi Wa bwana mmoja kule marekani aliyewaambia wafuasi wake kuwa kristo angerudi tarehe Fulani, mwezi Fulani then wafuasi wake wakafanya mambo fulanifulani yasio na tofauti yeyote na wafuasi Wa kibwetele. tofauti ni moja tu kibwetele aliwapiga moto wafuasi wake ila huyo bwana Wa huko maeekani yeye aliwatungia wimbo kwamba BWANA ATARUDI UPESI wimbo ambao unaimbwa mpaka leo na wafuasi wake wasiojua kuwa yesu alitahadharisha HAKUNA AIJUAYE SIKU WALA SAA.

Sasa hapo sijui mjinga Wa kuchomwa moto mpaka majivu ni nani ?
Ni wale walioambiwa yesu atarudi TAREHE FULANI MWEZI FULANI au ni KANISA lenye kuwaambia wakristo KESHENI MKISALI NA KUFUNGA MAANA HAMJUI SIKU WALA SAA WALA TAREHE WALA MWEZI HATA MWAKA WALA KARNE WALA MILENIA HAIJULIKANI, NI KAMA MWIZI TU AJAVYO. Hivyo Ni nani Wa kuchomwa moto mpaka majivu natumaini una akili na utashi hapo utajaza mwenyewe.

Hàlafu umaanza lini kuleta habali ambazo ni masimulizi/mapokeo (nazungumzia kuhusu yohane uliemtaja hapo mwisho nataka maandiko tena matakatifu na sio masimulizi/mapokeo). Umeanza lini kunukukuu habali za mapokeo/masimulizi amabayo kwako ni upagani sababu yako nje ya biblia. Unajua ni nani aliyekuletea hayo unayoyaita masimulizi kuhusu yohane kuwa ni mtume wa mwisho kufa nikikwambia ni kabisa katoliki utakataa ??

Leta andiko linaloonesha kuwa Hugo yohane unayemtaja hapo mwisho ndiye mtume Wa mwisho kufa na sio habali za mapokeo ya wanazuoni wako au masimulizi ya kipagani.
 
nyie msiofungamanisha endeleeni,acheni watu wafanye mambo yao na nyie fanyeni yenu mbinguni kila mtu anakwenda mwenyewe,tangu mmeanza hili zoezi mshapata wangapi????😀😀😀😀 mnachekesha kweli
Mkuu sio tatizo lao ni tatizo la kihistoria na vipaumbele vya waanzilishi wao. Kipaumbele naomba moja ni kupambana na ukristo kwa mwavuli Wa kabisa katolki
 
Samahani mm sio mtaalam sana wa mambo ya imani,,,

Ila naona kama mnatafautiana imani hapo,,mwenzio anaamini katika Mungu baba,Mungu mwana na Roho mtakatifu wewe mitale na midimu unaamini YESU ndio Mungu mwenyewe
Wakatoliki wanakitu wanakiita FUMBO LA IMANI,,huwezi kulipinga kwa namna yeyote kwa sababu halikuhusu,,ukifanikiwa kulisoma utaelewa anamaanisha nn,,yaani Fymbo hilo ndio siri ya Kanisa,, mengine yote ni blaa blaa

Please naomba utafute hilo fumbo
 
Mkuu sio tatizo lao ni tatizo la kihistoria na vipaumbele vya waanzilishi wao. Kipaumbele naomba moja ni kupambana na ukristo kwa mwavuli Wa kabisa katolki
watapata tabu sana kama ndio mapambano wanayaendesha kwa hoja nyepesi namna hiyo.......wanapaswa kuangalia na ukubwa wa hicho wanachopambana nacho.
wanatia huruma
 
Kumbe kweli nyie mna nia ovu kwa binadamu. Yaani mnaweza jitungia mambo yenu wenyewe kwa kuwa hamuwi limited kwenye Biblia na mkafanya mafundisho ya uongo kwa kisingizio hicho. Mungu anawaona. Lazima uwe na akili ya kujiuliza. Kama Yesu mwenyewe alibaki kwenye maandiko nyie ni nani hata muwe na mafundisho yasiyotokana na Biblia takatifu. Hiyo ina tofauti gani na upagani, kwani nao chanzo cha Imani yao siyo Biblia.
Kama kanisa linaweza kuamua kuwa na chanzo chake cha rejea badala ya Biblia, sasa hiyo itakuwa ni machafuko. Kumbe ndio maana tafisri ya kwamba nyie ndio Babel inawahusu

YESU aliwachochea watu waliheshimu Neno la Mungu, Biblia. Jambo hilo linaonekana wazi kutokana na majibu yake alipojaribiwa na Ibilisi. (Mathayo 4:4-11) Kwa mfano, Yesu alitenda jinsi gani Shetani alipomshawishi ageuze mawe yawe mikate? Yesu alipinga kishawishi hicho kwa kunukuu maneno ya Musa ambayo yaliongozwa na roho ya Mungu, na unaweza kuyasoma kwenye Kumbukumbu la Torati 8:3. Na wakati Ibilisi alipomtolea Yesu utawala wa falme zote za ulimwengu kwa kubadilishana na tendo moja tu la ibada, Yesu alimjibu namna gani? Alikataa na kutaja kanuni ya Kimaandiko ambayo unaweza kuipata kwenye Kumbukumbu la Torati 6:13.

Fikiria jambo hili! Ingawa Yesu alikuwa Mwana wa Mungu, alitegemea kabisa Biblia alipokuwa akifundisha. Na bila shaka hakupuuza kamwe Neno la Mungu na kufuata mapokeo ya wanadamu. (Yohana 7:16-18) Hata hivyo, viongozi wengi wa kidini wa siku za Yesu hawakuliheshimu Neno la Mungu kama Yesu alivyoheshimu. Kwa nini? Waliyaona mapokeo ya wanadamu kuwa ya maana sana kuliko Maandiko Matakatifu. Yesu aliwaambia hivi waziwazi wanaume hao wa kidini: “Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu. Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami. Nao huniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.”—Mathayo 15:6-9, Union Version.

Dini nyingi ulimwenguni, za Kikristo au zisizo za Kikristo, zinadai kwamba zinaiheshimu Biblia. Lakini unajua dini ngapi ambazo zinakataa mapokeo ya wanadamu wakati mapokeo hayo yanapopingana na mafundisho yaliyo wazi ya Neno la Mungu? Fikiria mifano miwili peke yake.

BIBLIA INAFUNDISHA HIVI: Yesu aliwashutumu viongozi wa kidini wa siku zake kwa sababu walipenda majina ya cheo na walitamani kuwa mashuhuri. Alisema kwamba wanaume hao walipenda “viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.” Kisha Yesu akawaambia hivi wanafunzi wake: “Ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu. Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.”—Mathayo 23:1-10, UV.

SWALI: Je, viongozi wa dini Yenu wanapenda kuitwa kwa majina ya cheo na kutaka kuwa mashuhuri katika jamii, au wanatii amri ya Yesu na kuepuka kufanya hivyo?

Kutumia sanamu katika ibada.

BIBLIA INAFUNDISHA HIVI: “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia.”—Kutoka 20:4, 5, UV.

Mtume Yohana aliwaandikia hivi Wakristo: “Epukaneni na sanamu za miungu!”—1 Yohana 5:21, Biblia Habari Njema.

SWALI: Je, dini hiyo inatii amri ya Biblia iliyo wazi ya kuepuka kutumia mifano na sanamu katika kumwabudu Mungu?
''Other' sources of your faith allow you overlook those bible facts and behave on your own way. na mnataka kutufundisha kuwa tusifuate Biblia.
Za kuambiwa changanya na zako ndugu
 
umeeleweka vyema
 
Yeye mwenyewe vip hanaga birthday?
 
Hao jamaa wafuate uwahoji mwenyewe ila mimi naamini haya.
Yesu anakuja Upesi licha ya kutojulika siku au saa.
Hakutaja siku lkn alitaja dalili, Nawaambia wakazi wa ulimwengu kuwa Yeye aliyesema anakuja mambo aloyotabiri yanatokea kwa spidi kubwa.
Nawaambia wajiandae muda wote sekunde zote maana hawajui saa wala siku.
Sio Mimi tu na wote wanaoamini Bibilia kama kitabu chao kukuu cha imani bila matamko ya wakuu wa kidini au masimulizi ya kimapokeo.

Hayo nimekupa maana unayaamini wewe. Nilitegemea uonyeshe msimamo imara kutetea na kuyafafanua.
Kama unakana na unavyoamini na unaogopa kuvijengea hoja, mkuu unakuwa unautoa mjadal kwenye uhalisia na kuusimika kwenye unafiki na usanii.

Ubarikiwe. naomba maoni yako kwenye mambo yako unayoyaamini, na umekiri kwa maandishi kuwa unayaamini, na umeayatumia kujenga hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…