Desemba 25: Je, ni siku aliyozaliwa Yesu au twaadhimisha tu kumbukumbu?

Ndo maama huwa nasemaga zitapita makanisa yote ila RC litabaki.....point ya msingi ni kwamba 25 dec ni siku kuu ya mungu jua ambayo ilikuwa inasheherekewa na watu wa roman empire miaka mingi ilopita...kwanin 25 dec...ni kwamba...kwa wale waliofika atleast form two katika elimu yao wanaweza kulielewa hili..jua huwa lautosi tropic of kapricon tar 22 dec...katika kipindi iki mwanga huwa hafifu sana katika northen hemisphere hivyo wanaamini kuwa mungu jua amezidiwa nguvu na mungu wa giza....ila inapofika tar 23 24 mpaka 25 mwanga huwa unaanza kuongezeka katika maeneo hayo kwa vile jua huwa linaanza tena kurudi kuelekea juu hivyo wanasema mungu jua kashinda na ameregain his power....ukiangalia siku ambazo jua huwa limeadimika kule ni almst siku tatu...ni siku izo izo ambazo yesu nae alikuwa kaburin kabla ya kufufuka...kwanini katholic litasimama daima...bible kama inavoonekana leo ni kazi ya kanisa katoliki...miaka ya 1200 kuna mijadala mizito ilifanyika na kanisa katika kuamua vitabu vipi viwepo na vipi visiwepo kwa sababu moja au nyingine...ndo maana chanzo kikubwa cha mafundisho ya wakatoliki ni kotoka kwenye bible...roho mtakatifu na from mapokeo...mapokeo yanainclude vile vitabu ambavyo havijakuwa cooporated kwenye bible..makanisa mengine hawavijui wanategemea bible tu ilioundwa na wakatoliki..think deep...unadhani mtume mkubwa kama petro hana maandiko yake kuhusu yesu...mpaka injili ije kuandikwa na luka na marko ambao hawakuwai kukutana na yesu hata kwa bahati mbaya....petro ana maandiko yake abt yesu..na mitume wengine pia ila kanisa limeyahifadhi kwa sababu mbalimbali...kuna mwenye swali
 
Mwanamke akishazaa atakuwaje bikira?

Kweli kabisa! sio tu kuzaa watasema kwa uwezo bla blah, pia Joseph alimuingilia na kuzaa naye watoto wengi tu! Kila mwanamke anazaliwa bikra kisha ubikira unakoma! Kwa nini ubikira wa Mary mnauendeleza!
 
Kweli kabisa! sio tu kuzaa watasema kwa uwezo bla blah, pia Joseph alimuingilia na kuzaa naye watoto wengi tu! Kila mwanamke anazaliwa bikra kisha ubikira unakoma! Kwa nini ubikira wa Mary mnauendeleza!

Ilirudi tena!!!!
 

hii ni siku ya kumbumbuku tu,si exact siku aliyozaliwa
 
Jamani hawa watu hawapo hapa kuelewa!!! na sidhani kama kuna umuhimu wa kumwelewesha mtu kitu asichokiamnini? hawayaamini yetu kama sisi tusivyomwamini ya kwao na mtume wao!!! Je mnadhani wakianza kutuconvience juu ya mtume wao tutawaamini na kuwasikia? vivo hivyo wao chochote tutakachowaambia hawataaelewa na kuamini...tusubiri siku ileeeee ijayo ambayo wao wanaiita ya kiyama ndo tutajua pumba na mchele

wanatumia jukwaa hili si kueleweshwa bali kusanifu na kukejeli!! Stop wasting time guys educating the non believers... tuwaache waamini kile wanachokiamini na sisi tuendelee na kile tunachoendelea kuamini na huo hasa ndio uhuru wa kuabudu.... tusipoteze muda juu yao
 

Kama ndivyo basi hatupaswi kusherehekea mwezi wa 12,maana mariamu mama wa yesu alishukiwa na malaika mwezi wa sita na kupashwa habari ya ujauzito,how come ajifungue mwezi wa 12?ni mawazo 2 jamani
 
mtoa mada una point kubwa sana..inahitaji kujibiwa kwa ushahidi..

lakini ushauri wangu ni kwamba kama huamini na hauna ushahidi wa kibiblia..usisherehekee mbona wengi katika watu hawasherehekei?
 
kuna issue leo kwenye moderation, maana naona mambo ya dini yanakimbizwwa kweli huku general public
 
kuna issue leo kwenye moderation, maana naona mambo ya dini yanakimbizwwa kweli huku general public
Kule kuna tatizo mkuu,
Mimi na u-premium member wangu thread ikimuvuzishiwa kule siwezi tena kuifungua!!
Ndio maana tunakimbilia huku
 
Cha msingi ni ukweli kwamba Yesu alizaliwa na 25 dec ndio imetokea kuwa siku ya kumbukumbu.
Asiyetaka kusherekea anaweza akaacha sio kila kitu kwa ajili ya kila mtu.
 
nakumbuka bibi yangu mzaa baba hakuwa anafahamu siku yake ya kuzaliwa anachokumbuka tu ni wakati wa nzige nyingi ndo alizaliwa, sinze alikuwa anapenda kusherehekea na kukumbuka kuzaliwa kwake, alitafuta tarehe moja akawa anafanya sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Je, kutokufahamu kwake amezaliwa hasa tarehe ngapi mwezi gani, kunamuondolea yeye kuwa amezaliwa na kwamba alikuwa duniani?

back to mada, as watu waliokwisha kusema, hii ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu, Biblia haijasema alizaliwa tarehe ngapi, bali inaeleza alizaliwa. Ndio maana kama unasoma vizuri Biblia yako utakuta unaambiwa kuna mambo mengi sana aliyoyafanya Yesu na yaliyotukia, ambayo kama yangeandikwa vitabu visingetosha.

Usijaribu kulazimisha kitu ambacho hauamini. kama hauamini don't remember kama unaamini kwa Mujibu wa hiyo Biblia unaoisema haijaandika, then sherehekea.

Kwake Yesu, Kila Goti litapigwa, Kila ulimi Utamkiri, Hadi Ninyi Waislamu mnalitaja hapa jina la Yesu bila kujijua. Haleluyaaaaaaa, Asifiwe Bwana Yesu na kupewa Sifa Milele, kwa kuwa Enzi na Mmlaka vipo mabegani mwake Milele na Milele
 
Kwanza kabisa nakupa hongera kwa kuibua mada nzuri na yenye kutufanya 2we watu wa kusoma biblia na kuielewa kwa undan.

Laki kwa uelewa wako ambao umeupata kwa kusoma biblia naomba nirudishe swali kwako tena, je kuna mahali ambapo biblia imetaja mwezi na tarehe ya kuzaliwa Yesu kristo.
 

Mkuu unazungumzia watu gani?
 
Haya maswali mara nyingine yanatia mashaka moyoni. Tutaaenza kuulizana boxingday kama ipo kwenye maandiko!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…