Desemba 25: Je, ni siku aliyozaliwa Yesu au twaadhimisha tu kumbukumbu?

Desemba 25: Je, ni siku aliyozaliwa Yesu au twaadhimisha tu kumbukumbu?

The point is not about historical exactness but faith. Jesus was truly born but no one knows the exact date. What is important is to emulate his life on love and compassion to one another.


Ni kweli kaka, ila kujifunza na kutaka kuelewa kitu kwa undani zaidi sio dhambi.

Kinachonisukuma ni kutaka kujua hasa ni lini kristo alizaliwa ili kujua maana halisi ya hii Christmass ambayo tunasheherekea kila tarehe 25 december kila mwaka.
 
"we live in age of smartphone and stupid peoples"

mkuu,kusherekea siyo tatizo,tatizo ni pagan-root ya christmass

halafu kama wewe unaamini biblia,hakuna sehemu yoyote ambayo yesu wenu alisema mkumbuke kuzaliwa kwake

kama ipo ilete hapa,mkuu tujifunze!


Mkuu, ni kweli hakuna kifungo ambacho katika biblia kinasema tusheherekee siku ya kuzaliwa kwa yesu.

Nataka kujua, Je ni kweli kwamba christmas ilikuwepo kabla ya Yesu kuzaliwa?
 
Unachanganya mambo hapa! Nilikuwa tu najaribu kumsahihisha mleta mada alipouliza kuhusu Wakristo wanasherehekea siku ya kuzaliwa Kristo, ndiyo nikamjibu kwamba wakristo wanasherehekea kuzaliwa kwa kristo na siyo siku ya kuzaliwa!

Sasa hayo mambo ya Upagani au sijui Biblia imeorodhesha siku ya kuzaliwa kristo au la hiyo ni mada nyingine, mimi nilikuwa nataka kumsahihisha tu kulingana na swali lililoulizwa!



Mkuu with thanks.

Kwahiyo unataka kusema kuwa tarehe 25 december wakristo huwa tunasheherekea kuzaliwa kwa kristo na sio siku ya kuzaliwa kristo.

Swali kwako, Je ni kwanini walichagua tarehe 25 december?
 
Huu uzushi kwa wapuu..zi kama wewe unaweza wsingiza chaka....

Ngoja nikae sawa nakurudia..


Mkuu,

Jf ni uwanja huru wa hoja, kuitana wapuuzi ni kuishushia hadhi JF na members wake, lugha za kejeli hapa sio mahali pake.

Kama una documents ambazo ni valid ni vema ukazileta ili sisi akina ndute (tusiojua kitu) tuweze kujifunza na kuelewa usahihi wa mambo yale tulioadithiwa na kujisomea.

JF, Where We Dare to talk Openly.
 
Heshima kwenu wadau,

inawezekana hili swali likawa limejadiliwa sana hapa, ila nimejaribu kutafuta huo uzi nimeshindwa kuupata, swali langu ni hili hapa,

Je december 25 ambayo si siku ya chrismass ambayo twaambiwa alizaliwa kristo ni kweli alizaliwa siku hiyo au twaadhimisha tu kama kumbukumbu yake?

kwa mujibu wa Biblia takatifu, Injili ya luka mtakatifu inasema " Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.
28 Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.
29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?
30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.

kama maandiko matakatifu yanasema kuwa Maria mtakatifu alipata mimba mwezi wa sita manake tungetarajia kujifungua mwezi wa tatu au wa pili mwishoni.

Swali lingine ambalo ningependa kwa mwenye ujuzi ni je zamani walikua wanatumia kalenda gani kuhesabau siku? nadhani hapa ndipo ukweli wa mambo ulipo.

Naomba kufahamu kwa wenye ujuzi wa mambo ya kiroho na wanahistoria.

NA MUNGU AWABARIKI SANA.

Maoni ya Biblia
Yesu Alizaliwa Wakati Gani?
?TAREHE hususa ambayo Kristo alizaliwa haijulikani,? inasema Encyclopedia of Early Christianity. Hata hivyo, mamilioni ya watu wanaodai kuwa Wakristo ulimwenguni pote husherehekea kuzaliwa kwa Yesu Desemba (Mwezi wa 12) 25. Lakini tarehe hiyo haionekani mahali popote katika Biblia. Je, kweli Yesu alizaliwa Desemba?
Ingawa Biblia haitupi tarehe hususa ya kuzaliwa kwa Yesu, inatoa uthibitisho wa kwamba hakuzaliwa Desemba. Mbali na Biblia kuna uthibitisho mwingine unaoweza kutusaidia kujua kwa nini Desemba 25 ilichukuliwa kuwa tarehe ya kusherehekea kuzaliwa kwake.
Kwa Nini Hakuzaliwa Desemba?
Yesu alizaliwa katika jiji la Bethlehemu huko Yudea. Injili ya Luka inaripoti hivi: ?Katika nchi hiyo kulikuwako pia wachungaji wakiishi nje, wakichunga makundi yao usiku.? ( ) Hilo lilikuwa jambo la kawaida. ?Kwa miezi mingi mifugo ilikuwa katika maeneo yaliyo wazi,? kinasema kitabu Daily Life in the Time of Jesus. Lakini je, wachungaji wangekuwa nje na mifugo yao katika usiku wenye baridi wa Desemba? Kitabu hicho kinasema: ?Katika majira ya baridi kali walikuwa ndani ya nyumba; na hilo peke yake linafanya tarehe ya Krismasi, katika majira ya baridi kali, kuwa si sahihi kwa sababu Injili inasema wachungaji walikuwa mashambani.?
Mkataa huo unapatana na habari nyingine katika Injili ya Luka: ?Katika siku hizo Kaisari Augusto alitoa amri kwamba dunia yote inayokaliwa iandikishwe; (uandikisho huu wa kwanza ulitendeka wakati Kirenio alipokuwa gavana wa Siria😉 na watu wote wakaanza kusafiri kwenda kuandikishwa, kila mmoja kwenye jiji lake mwenyewe.?? .
Huenda Augusto aliamuru uandikisho huo ili atumie habari hiyo kuhusiana na kutoza ushuru na kuandikisha watu jeshini. Ili atii amri hiyo, Maria, aliandamana na mume wake, Yosefu, katika safari ya kilomita 150 hivi kutoka Nazareti kwenda Bethlehemu ingawa alikuwa karibu kuzaa. Sasa hebu fikiria kuhusu jambo hilo. Je, inapatana na akili kwamba Augusto, mtawala ambaye hakujihusisha sana na serikali za wilaya, angewaamuru watu ambao walikuwa tayari kuzusha ghasia dhidi ya utawala wa Waroma wafunge safari hiyo ndefu katika majira ya baridi kali?
Ni muhimu kujua kwamba wanahistoria na wasomi wengi wa Biblia wanapinga kwamba Yesu alizaliwa Desemba 25. Bila shaka, utapata habari hiyo katika ensaiklopedia mbalimbali. Our Sunday Visitor?s Catholic Encyclopedia inasema: ?Watu wengi wanakubaliana kwamba Yesu hakuzaliwa Desemba 25.?
Kwa Nini Walichagua Desemba 25?
Mamia ya miaka baada ya kifo cha Yesu, Desemba 25 ilichaguliwa kuwa tarehe ya kuzaliwa kwake. Kwa nini? Wanahistoria wengi wanaamini kwamba wakati ambao sasa Krismasi husherehekewa ulikuwa wakati wa sherehe za kipagani.
Kwa mfano, Encyclop?dia Britannica
inasema: ?Ufafanuzi mmoja ulioenea wa chanzo cha tarehe hii ni kwamba sikukuu ya dies solis invicti nati (?siku ya kuzaliwa kwa jua lisiloshindwa?) iliyosherehekewa Desemba 25, ilifanywa kuwa ya Kikristo. Hiyo ilikuwa sikukuu maarufu ya Milki ya Roma iliyosherehekewa wakati jua linapochomoza katika majira ya baridi kali kama ishara ya mwisho wa majira hayo na mwanzo wa majira ya kupukutika na kiangazi.?
Kitabu The Encyclopedia Americana
kinatuambia hivi: ?Sababu ya kutenga Desemba 25 kuwa Krismasi haijulikani, lakini inaaminiwa kwamba siku hiyo ilichaguliwa ili ilingane na sherehe ya kipagani iliyofanyika jua lilipochomoza katika majira ya baridi kali, wakati mchana ulianza kuwa mrefu, ili kusherehekea ?kuzaliwa tena kwa jua.? . . . Satanalia ya Kiroma (sherehe ya Saturn, mungu wa kilimo, na nguvu mpya za jua), pia ilifanyika wakati huo.? Kwa kawaida, sherehe hizo zilitia ndani mwenendo mpotovu kingono ambapo watu walisherehekea bila kujizuia na kwa kelele nyingi sana. Tabia hizohizo huonekana katika sherehe nyingi za Krismasi leo.
Jinsi ya Kumheshimu Kristo
Watu fulani wanahisi kwamba hata ingawa hatujui tarehe hususa, ni lazima Wakristo washerehekee kuzaliwa kwa Yesu. Kwa maoni yao, sherehe hiyo inapofanywa kwa njia inayofaa ni njia nzuri ya kumheshimu Kristo.
Kwa kweli, kuzaliwa kwa Yesu ni tukio muhimu katika Biblia. Biblia inasema kwamba Yesu alipozaliwa, umati wa malaika ulitokea ghafula na kumsifu Mungu kwa shangwe wakisema: ?Utukufu katika vilele vilivyo juu kwa Mungu, na juu ya dunia amani kati ya watu wa nia njema.? ( ) Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba hakuna mahali popote katika Biblia ambapo inasemekana kwamba siku ya kuzaliwa kwa Yesu inapaswa kusherehekewa. Kinyume na hilo, kuna amri hususa ya kuadhimisha kifo chake. Mashahidi wa Yehova hufanya hivyo mara moja kwa mwaka. (
) Hiyo ni njia moja ya kumheshimu Yesu.
Usiku wake wa mwisho akiwa mwanadamu, Yesu alisema: ?Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mnafanya ninalowaamuru ninyi.? ( ) Pia alisema: ?Ikiwa mnanipenda, mtazishika amri zangu.? ( ) Ni wazi kwamba hakuna njia bora zaidi ya kumheshimu Yesu Kristo kuliko kujifunza na kufuata mafundisho yake.
JE, UMEJIULIZA HIVI?
▪ Kwa nini haiwezekani kuwa Yesu alizaliwa Desemba?? .
▪ Ni nini muhimu kuliko siku ambayo mtu alizaliwa?? .
▪ Ni njia gani bora zaidi ya kumheshimu Yesu?? .
[Picha katika ukurasa wa 11]
Biblia inatoa uthibitisho wa kwamba Yesu hakuzaliwa Desemba
[Picha katika ukurasa wa 10]
Je, wachungaji wangekuwa nje na mifugo yao usiku katika theluji?
[Hisani]
Todd Bolen/Bible Places.com
Luka 2:4-8
Luka 2:1-3
Luka 2:13, 14
Luka 22:19
Yohana 15:14
Yohana 14:15
Luka 2:1-8
Mhubiri 7:1
Yohana 14:15
 
Heshima kwako @RGforever

Naomba kabla hujachangia soma kwanza bandiko vizuri sana, Bible takatifu inasema bikira maria alipata mimba mwezi wa sita na yesu alizaliwa tarehe 25 december kwa maana ya miezi saba mbele baada ya kupata ujauzito bikira maria akajifungua mtoto yesu, nilichotaka kujua ni kwamba kwa sayansi mtoto anaezaliwa akiwa na miezi saba au sita ni ngumu sana kuishi sababu anakua ni njiti (hajatimiza miezi 9 )

Swali, Je tunasherehekea siku ambayo kweli yesu alizaliwa au ni watawala tu wa kale waliamua kuiweka hii siku kama kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na haikuwa siku halisi?

Kwa iyo unataka kusema Mungu hawezi kumsababishia mtu mimba na ndani ya sekunde moja akazaa, ni mpaka atimize miezi 9 sio?
 
"we live in age of smartphone and stupid peoples"

mkuu,kusherekea siyo tatizo,tatizo ni pagan-root ya christmass

halafu kama wewe unaamini biblia,hakuna sehemu yoyote ambayo yesu wenu alisema mkumbuke kuzaliwa kwake

kama ipo ilete hapa,mkuu tujifunze!

Wapi Yesu alioga au alisema tunapaswa kuoga au tupande bajaj?
 
christmass,"the feast of the unconquered sun"


nini maana ya neno "christmas"?,christmass ni muunganiko wa maneno mawili "christ" na "mas"
christ ni kristo,lakini nini maana ya "mas"au mass?

mass:"
mass is service that is held to remember the death of any person for whom the mass is held"...

maana ya "mass" itakushangaza zaidi,kwahiyo unaposema merry christmass,unamaanisha "heri kifo cha kristo,..senseless!..tunafurahia kuzaliwa kwa yesu au kifo chake?...jibu ni kifo chake!

Asili halisi ya christmass ni hii;..Roman empire chini ya constantantine iliunganisha dini zote za kipagani pamoja na kikristo na kuunda kanisa linaloitwa Roman catholic,ili kuunganisha dini zote ilibidi waunganishe pia mafundisho yao,moja kati ya hayo mafundisho ni sherehe ya kifo cha mungu tammuzi ambaye alizaliwa 24-12 akafa usiku wa tarehe 25 december(ref;encyclopeda brittanica,volume 11)

SANTA =S-A-T-A-N,huyo ndiye father christmass,teh teh teh

zamani walikuwa wanatumia julian calender kabla ya gregorian calender!
U.puuzi wa kwanza: ni dini gani huyo constsntine aliziunganisha..?? Lini..??

Upuuz.i wa pili: Hakuna kanisa linaitwa Roman Catholic ila Catholic Church..Roman iliongezwa na protestant mno wakiwa ni Anglican karne ya 16....

Upu.uzi wa tatu..... Hakuna fundisho linalosema tusherehekee kuzaliwa kwa Yesu tarehe 25... Maadam umesema ni fundisho ni vyema utuambie limetoka wapi(nukulu inahitajika hapa)

Kama hutonijibu ipasavyo wewe utaendelea kuwa mp.uuzi...Ila sitakuacha ulete upu.uzi wako hapa
 
Halafu Wasabato na mashahidi wa Yehova kipindi hiki huwa wanapenda kuzilite hizi mada...ila....
 
U.puuzi wa kwanza: ni dini gani huyo constsntine aliziunganisha..?? Lini..??

Upuuz.i wa pili: Hakuna kanisa linaitwa Roman Catholic ila Catholic Church..Roman iliongezwa na protestant mno wakiwa ni Anglican karne ya 16....

Upu.uzi wa tatu..... Hakuna fundisho linalosema tusherehekee kuzaliwa kwa Yesu tarehe 25... Maadam umesema ni fundisho ni vyema utuambie limetoka wapi(nukulu inahitajika hapa)

Kama hutonijibu ipasavyo wewe utaendelea kuwa mp.uuzi...Ila sitakuacha ulete upu.uzi wako hapa

1.mfalme constantine alikuwa ni sun worshiper
ibada ya jua ndiyo ilikuwa imani yenye wafuasi wengi wakati wa falme ya Rumi

mfalme constantine alipoufanya ukristo kuwa official religion mnamo mwaka wa 324 AD,ndipo alipochanganya baadhi ya mafundisho ya kipagani na ya kikristo.kwahiyo dini zilozounganishwa hapo ni upagani na ukristo wa wakati ule

2.ni kweli term ya Roman catholic ilitumiwa na kanisa la Anglicana(karne ya 17 na sio 16)lakini hii haiondoi ukweli.
 
Upu.uzi wa tatu..... Hakuna fundisho linalosema tusherehekee kuzaliwa kwa Yesu tarehe 25... Maadam umesema ni fundisho ni vyema utuambie limetoka wapi(nukulu inahitajika hapa)

Kama hutonijibu ipasavyo wewe utaendelea kuwa mp.uuzi...Ila sitakuacha ulete upu.uzi wako hapa
[/QUOTE]

3.hakuna sehemu niliyosema kuwa wakristo wanatakiwa kusherekea kuzaliwa kwa yesu labda hukunielewa tu mkuu!

4.halafu hapa mpuuzi ni nani?

yule aliyeambiwa kuwa athibitishe kwa ushaidi,kwanini yeye anasherekea christmass,lakini badala ya kutoa ushaidi akaanza kuuliza maswali,

sasa wewe ndiyo utakuwa mpuuzi kama hutothibitisha kuwa ni halali kuadhimisha kuzaliwa kwa yesu wakati wa christmass kwa kutumia biblia!
 
Ni siku ya kipagani ilianzishwa na wapagani kusheherekea kufunguliwa kwa mfungwa wao
 
Kwa iyo unataka kusema Mungu hawezi kumsababishia mtu mimba na ndani ya sekunde moja akazaa, ni mpaka atimize miezi 9 sio?


Mkuu, KakaJambazi

Inawezekana kwa hisia tu, ila kwa hali ya kawaida haiwezekani, Mungu ndiye anaewaunganisha na ni yeye ndie alieweka hizo fomula za mimba kukaa kipindi cha miezi tisa tumboni ndipo kichanga kizaliwe.
 
Last edited by a moderator:
kabla ya maria na yoseph, jesus alikuwepo hukooo kwa baba ake jehova.
 
Kiufupi siku aliyozaliwa yesu haijulikani na wala hakuna picha yake popote ulimwenguni
 
kabla ya maria na yoseph, jesus alikuwepo hukooo kwa baba ake jehova.


Hilo twalijua, Yesu alikuwepo kabla hata ya Ulimwengu kuwako, Ila kitu ambacho tunahitaji kujua ni tarehe ngapi alizaliwa? Je hii siku ambayo twaadhimisha christmass au siku tofauti na hiyo? Hapo ndipo msingi wa swali langu ulipojikita.
 
Kiufupi siku aliyozaliwa yesu haijulikani na wala hakuna picha yake popote ulimwenguni


Mkuu peterchoka

Hapo kwenye tarehe naweza kukubaliana na wewe kutokana na contradictions zilizopo ila hapo kwenye picha umemaanisha nini?

Hizi picha tunazoweka makanisani za Yesu unataka kuniambia sio picha zake?

Kumbuka pia zamani hakukuwa na camera bali kulikuwa na wachoraji wazuri tu ambao wanaweza kukuchora sura yako.Mfano picha ya Herode watu wanayo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom