Heshima kwenu wadau,
Inawezekana hili swali likawa limejadiliwa sana hapa, ila nimejaribu kutafuta huo uzi nimeshindwa kuupata, swali langu ni hili hapa,
Je december 25 ambayo si siku ya chrismass ambayo twaambiwa alizaliwa kristo ni kweli alizaliwa siku hiyo au twaadhimisha tu kama kumbukumbu yake?
Kwa mujibu wa Biblia takatifu, Injili ya luka mtakatifu inasema " Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.
28 Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.
29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?
30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
kama maandiko matakatifu yanasema kuwa Maria mtakatifu alipata mimba mwezi wa sita manake tungetarajia kujifungua mwezi wa tatu au wa pili mwishoni.
Swali lingine ambalo ningependa kwa mwenye ujuzi ni je zamani walikua wanatumia kalenda gani kuhesabau siku? nadhani hapa ndipo ukweli wa mambo ulipo.
Naomba kufahamu kwa wenye ujuzi wa mambo ya kiroho na wanahistoria.
NA MUNGU AWABARIKI SANA.