Azathioprine
JF-Expert Member
- Sep 16, 2013
- 589
- 376
Yesu kristo hakuzaliwa Tarehe 25 December. Hili ni moja kati ya mapokeo ya kitamaduni za kipagani zilizofanikiwa kuingia ndani ya kanisa la kikristo kwa kubebwa na Kanisa Katoliki.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
teh teeh teeeh eeeerh... .. .biblia ni moja na quran ni moja... .. . lakini kundi/dhehebu moja huona mafundisho yao ni bora kuliko ya wengine,
Mkuu, Heshima kwako,
Kama tukiwa sote na tabia ya kula kitu bila kujua kimetokana na nini basi hii Dunia isingefika hapa tulipo, Dunia inahitaji watu wanaojua kuhoji na kudadisi mambo mbalimbali yaliyotokea, yatakayotokea na yanayotokea.
Si kwakua kitu hatukijui basi tukae kimya, Japo dini huwa zinazuia kuhoji kitu ambacho kina sintofahamu ila ni vyema kutatua tatizo mapema kabla halijawa kubwa. Hizi contradictions ndizo ambazo zinafanya waumini wa hizi dini kupungua kadri siku sinavyoenda.
Hakuna mkanganyiko wowote katika hili, wala hakuna wauumini wa dini wanauulizia suala za kuzaliwa Yesu.Nyie ambao hii dini haiwahusu ndio mna viherere vya kuuliza maswali kama hayo.
Kuna mdau mmoja amekujibu vizuri sana, kuwa kinachosheherekewa ni KUZALIWA YESU, sio SIKU YA KUZALIWA YESU!
Nadhani huna takwimu za kutosha juu ya Ukristo duniani. Ndio dini inayoongezeka kwa kasi duniani kuliko dini ingine, na dhehebu la Catholic ndio linaloongoza. Kwa taarifa yako Idadi ya Wakatoliki tu duniani (achana na madhehebu mengine ya kikristo kama Lutheran, SDA, Angalican n.k) ni sawa na Waislamu (watoto wa mama mdogo) wote Ulimwenguni kot e(Shia na Sunni).
Ubarikiwe katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
..................................
Kwani yesu alipozaliwa alizaliwa km Mungu au alizaliwa km Mwanadamu kama sisi? naomba nijibiwe hapo kwanza plz
Ni kumbukumbu. Yesu hakuzaliwa Desemba 25. Ilikuwepo Rome dini pinzani ya Mithra ambao mtume wake,Mithra alizaliwa Desemba 25.Wakristu wakasema Yesu kazaliwa Desemba 25 ili kuwavuta waumini wa dini ile. Baadaye ile dini ikafa na Wakristu wakavunja hekalu lao na kujenga St.Peter's Basilica. Kwa sababu ile dini ya Mighra,hekalu lake lilikuwa limejengwa pale pale ambapo sasa bivi ipo St Peter' Basilica.. Yesu kazaliwa 888. Tarehe 8,mwezi wa nane,August,mwaka wa nane AD8
Hakuna mkanganyiko wowote katika hili, wala hakuna wauumini wa dini wanauulizia suala za kuzaliwa Yesu.Nyie ambao hii dini haiwahusu ndio mna viherere vya kuuliza maswali kama hayo.
Kuna mdau mmoja amekujibu vizuri sana, kuwa kinachosheherekewa ni KUZALIWA YESU, sio SIKU YA KUZALIWA YESU!
Nadhani huna takwimu za kutosha juu ya Ukristo duniani. Ndio dini inayoongezeka kwa kasi duniani kuliko dini ingine, na dhehebu la Catholic ndio linaloongoza. Kwa taarifa yako Idadi ya Wakatoliki tu duniani (achana na madhehebu mengine ya kikristo kama Lutheran, SDA, Angalican n.k) ni sawa na Waislamu (watoto wa mama mdogo) wote Ulimwenguni kot e(Shia na Sunni).
Ubarikiwe katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
..................................
mkuu labda hujaelewa lengo kuu la mleta mada.
tatizo siyo kusherekea christmas,tatizo ni kwanini iwe december 25.na siyo siku nyingine
halafu ile njia ni nyembamba kaka,ndiyo maana wacatholic wapo wengi njia Nene.
Soma 1 Wakorintho 11:23-26: maagizo pekee aliyotuachia Bwana Yesu ni kula mkate na divai kama kumbukumbu ya mwili wake na damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Verse 26 inasema " kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hadi ajapo."
Acheni kujifariji kwa mafundisho ya uongo yasiyotokana na Biblia Takatifu. Bwana Yesu hakuona umuhimu wowote wa kusherehekea kuzaliwa kwake kwani alikuwepo tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Hata yeye wala mitume wake hakuna aliyesherehekea birthday ya Yesu, ninyi mwaitoa wapi?
Jambo la msingi ni kumbukumbu ya mauti yake kwani hilo ndilo kusudi lake kuu lililometa hapa duniani na kuutwaa mwili huu wa dhambi ili afe kwa ajili yetu wadhambi.
Someni maandiko yawaweke huru acheni kusikiliza hadithi za uongo zitawapoteza.
Mkuu hapo nimekuelewa, labda tatizo lipo kwa waandishi wa biblia ya kiswahili, ukisoma hapo vizuri unaweza kuchukua ni mwezi wa sita wa kalenda.
Mkuu nina swali kwako, Je kuna tofauti gani kati ya kusherehekea siku ya kuzaliwa na kukumbuka siku ya kuzaliwa?
Nimeuliza hivyo kwa sababu as per our life ni kwamba huwa tunasheherekea siku ya kuzaliwa pamoja na kukumbuka mpaka pale inapofika tarehe husika na siku husika.
Hapo hamna maagizo au katazo tusifanye KUMBUKUMBU YA kuzaliwa kwake. au naona vibaya.
kwamba ni "maagizo pekee" haimaanishi tusifanya vitu vingine. Nithibitishie kuwa kufanya hivyo ni dhambi
Mfuasi mwaminifu wa Kristo hufanya yale yaliyoagizwa na Bwana wake wala hajitafutii mambo mengine tofauti na yale yaliyoagizwa. Hivyo hayo huitwa mapokeo na kumbuka Bwana Yesu alikemea mapokeo rejea Mathayo 15:8,9
Heshima kwenu wadau,
Inawezekana hili swali likawa limejadiliwa sana hapa, ila nimejaribu kutafuta huo uzi nimeshindwa kuupata, swali langu ni hili hapa,
Je december 25 ambayo si siku ya chrismass ambayo twaambiwa alizaliwa kristo ni kweli alizaliwa siku hiyo au twaadhimisha tu kama kumbukumbu yake?
Kwa mujibu wa Biblia takatifu, Injili ya luka mtakatifu inasema " Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.
28 Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.
29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?
30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
kama maandiko matakatifu yanasema kuwa Maria mtakatifu alipata mimba mwezi wa sita manake tungetarajia kujifungua mwezi wa tatu au wa pili mwishoni.
Swali lingine ambalo ningependa kwa mwenye ujuzi ni je zamani walikua wanatumia kalenda gani kuhesabau siku? nadhani hapa ndipo ukweli wa mambo ulipo.
Naomba kufahamu kwa wenye ujuzi wa mambo ya kiroho na wanahistoria.
NA MUNGU AWABARIKI SANA.
Siyo kukumbuka siku ya kuzaliwa... ila tofauti ni hii; tarehe 25 december ni siku ya kukumbuka "KUZALIWA KWA YESU" unaona tofauti inapokuja?
tunasherekea kwamba Yesu "ALIZALIWA", na faida ya KUZALIWA kwake nadhani unaelewa
Mfuasi mwaminifu wa Kristo hufanya yale yaliyoagizwa na Bwana wake wala hajitafutii mambo mengine tofauti na yale yaliyoagizwa. Hivyo hayo huitwa mapokeo na kumbuka Bwana Yesu alikemea mapokeo rejea Mathayo 15:8,9
Ukipiga mahesabu imeonyesha tunaazimisha tusicho kijua maana inasemekana Tammus ndo alizaliwa tarehe iyo mtt wa kambo wa nimrod
Kadiri nielewavyo 24-25 desemba kulikuwa na mabadliko ya muda wa mwanga kuongezeka na hivyo kusherehekewa kipagani kama siku ya jua kushinda kiza. Ukristu ili kuondo a imani za kipagani, ikumbukwe ku0ngoka kwa Konstantini mfalme kulikuwa na changamoto zake na faida kwa ukristo wakati huo. Moja ya changamoto ilikuwa tafsiri ya Sabato kutoka kuwa jumamosi na kuwa jumapili, baadhi ya sherehe za kipagani kukristishwa ikiwamo christmas na ufungamanisho wa ukristo na utawala. Faida ahueni ya mateso kwa wakristo.Ni kweli kaka, ila kujifunza na kutaka kuelewa kitu kwa undani zaidi sio dhambi.
Kinachonisukuma ni kutaka kujua hasa ni lini kristo alizaliwa ili kujua maana halisi ya hii Christmass ambayo tunasheherekea kila tarehe 25 december kila mwaka.