View attachment 957929
nadhani ameeleza vizuri sikukuu hiyo ni makubaliano ya kanisa lake ila sio agizo la Yesu.
Haikukumbukwa na Mitume.
Haikukumbukwa hata na hao wafuasi wa mitume wa awali.
Watu ni vizuri wakaelewa hilo pia.
Maoni ya kikundi binafsi yasibebeshwe hadhi ya kuwa universal obligation kwa kila mcha Mungu.
Kuiga mambo ya wapagani ni sawa na Kutoka Nuruni kwenda kutafuta mwanga gizani.
Watu wa Bibilia hawakuhangaika na haya masherehe maana walijua Kuzaliwa na Kufa kwa Yesu mioyoni mwao ni Jukumu la Kiroho la mkristo kila siku sio sikukuu ya kula ubwabwa na kununua mimea kuijaza sebuleni.
Maoni ya wanadamu, yanapaswa kutenganishwa na maandiko katika matamshi na maandishi.
maelezo mengi mazuri yalioandikwa kwa lugha shawishi ila hayana uzito wowote kwenye maandiko matakatifu mzani umeelemea kwenye utamadunishwaji na masimulizi ya kale.