mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,735
hilo fumbo halijadiliki mkuu ? au ni siri na fumbo hadi huku mitandaoni.Samahani mm sio mtaalam sana wa mambo ya imani,,,
Ila naona kama mnatafautiana imani hapo,,mwenzio anaamini katika Mungu baba,Mungu mwana na Roho mtakatifu wewe mitale na midimu unaamini YESU ndio Mungu mwenyewe
Wakatoliki wanakitu wanakiita FUMBO LA IMANI,,huwezi kulipinga kwa namna yeyote kwa sababu halikuhusu,,ukifanikiwa kulisoma utaelewa anamaanisha nn,,yaani Fymbo hilo ndio siri ya Kanisa,, mengine yote ni blaa blaa
Please naomba utafute hilo fumbo
ila mkuu nashukuru kwa maoni, hata mimi nimekiri kuwa hata xmass ni mambo ya kikatoliki sio ya kibibilia.
ndio maana siwalaumu kwa mambo yao ya imani, ila nawahoji tu kwa kulazimisha kuyahalalisha kwa kutumia bibilia wakati wanakili kuwa mambo yao bibilia sio hakimu wa Mwisho. wanamahakimu watatu, bibilia, mapokeo wanayoyaita matakatifu na kauli za wakuu zao. Yaani hakuna tofauti kati ya kauli au barua ya papa Fransis kwa katisa katoliki Bugando na Barua za Paulo labda kwa wakorintho. Vyote vinahadhi sawa bila kujali content.
kama nakosea nikosolewe maana wenye imani wamo humu wanaweza kuweka sawa.
Tunapojadili tunasaidia kujua imani zetu, ili kupunguza kuzushiana na kujua nini tunatofautiana na kwa nini.