Dhambi 5 zisizoepukika hata kwa washika dini

Dhambi 5 zisizoepukika hata kwa washika dini

Yote naweza kuepuka hasa uchoyo,dhuluma,chuki yani sina historia ya kumdhurumu mtu wala kuwa na chuki na yoyote wala choyo, uzinzi sio sana,uongo kiasi, ushirikina never ,ulevi kiasi, ntaenda motoni kwa kuwa maskini labda
 
Dhulma huanzia mbali kabisa utotoni.Unakula na wenzako halafu unamega matonge "manene" au kuchukua nyama harakaharaka kabla ya wenzako.Hiyo ni dhulma.Kumnyima mwenza wako mahaba bila sababu.Hiyo ni dhulma.Kumchapa mtoto kimakosa ni dhulma.Kutokusalimu wengine kwa kiburi tu ni dhulma.Kukataa kupisha wengine njiani ni dhulma.Kupewa kitu na kutosema asante ni dhulma nk.
Dhuluma ni nini mkuu
 
Hata uwe mtu wa dini vipi kwa siku angalau utatenda mojawapo ya hizi dhambi.

1. Uongo

2. Uzinzi/uasherati

3. Dhuluma

4. Ubinafsi/Uchoyo

5. Chuki
Inawezekana kabisa kuacha zote hizo. Lakini hii inategemea na hofu yako kwa Mungu na kujua nini Mungu anataka utende na nini usitende. Mimi nilikuwa na hizo mbili za mwanzo ila kwa sasa nimezishinda kwa msaada wa Mungu miaka inakatika. Ni ngumu usipokuwa na Yesu ila Yesu akiingia ndani yako ya kale yanapita na yanakuwa mapya. Mkabidhi Yesu maisha yako atakufundisha jinsi gani ya kuzishinda hizo dhambi.
 
Dhambi ni mtazamo tu!

Hivi mimi nimekubaliana na mdada fresh sijamlaghai wala kumpa ahadi hewa, akaja geto jioni tukafurahia tofauti zetu asubuhi tukapiga supu akarudi kwake. Yeye kaenjoy mimi nimeenjoy afu mtu anasema tulichofanya ni dhambi
😀😀😀 si ndio!!
 
Nasikia hata kuwazia tu hayo already utakuwa umetenda dhambi achilia mbali kuyafanya kwa vitendo
 
Hapo uongo ndio ngumu, hizo zingine nyepesi sana ukiamua
 
Nasikia hata kuwazia tu hayo already utakuwa umetenda dhambi achilia mbali kuyafanya kwa vitendo
Dhambi pekee inayoeleza hayo ni ya... 'Usitamani mwanamke asiyekuwa mke wako'
Hayo mengine huwezi kuyachuma kwa kuwaza tu.
 
Dhulma huanzia mbali kabisa utotoni.Unakula na wenzako halafu unamega matonge "manene" au kuchukua nyama harakaharaka kabla ya wenzako.Hiyo ni dhulma.Kumnyima mwenza wako mahaba bila sababu.Hiyo ni dhulma.Kumchapa mtoto kimakosa ni dhulma.Kutokusalimu wengine kwa kiburi tu ni dhulma.Kukataa kupisha wengine njiani ni dhulma.Kupewa kitu na kutosema asante ni dhulma nk.
Kumega matonge makubwa makubwa na kuchukua nyama haraka haraka kumbe ni dhulma!

Ndiyo maana tumebadili mtindo wa nidhamu ya chakula mezani siku hizi.
Kila mtu na sahani yake, atajaziwa kwa kujichotea ama kugawiwa.

Hii hupunguza sana hiyo tabia ya uroho ama dhulma.
 
Hata uwe mtu wa dini vipi kwa siku angalau utatenda mojawapo ya hizi dhambi.

1. Uongo

2. Uzinzi/uasherati

3. Dhuluma

4. Ubinafsi/Uchoyo

5. Chuki
Hii ya pili si dhambi kwani ni wajibu wa kila mtu au kiumbe wa Mwenyezi Mungu kuwajibika. Mungu ametupa alivyotupa ili tupeane na kuburudishana.
 
Kumega matonge makubwa makubwa na kuchukua nyama haraka haraka kumbe ni dhulma!

Ndiyo maana tumebadili mtindo wa nidhamu ya chakula mezani siku hizi.
Kila mtu na sahani yake, atajaziwa kwa kujichotea ama kugawiwa.

Hii hupunguza sana hiyo tabia ya uroho ama dhulma.
Dhulma kubwa sana.Ndiyo chanzo cha wizi na ufisadi/uchoyo/ubinafsi na dharau kwa wengine kwa kuwaona dhalili.
 
Kwa siku? Mbona rahisi sana kuepuka hayo hasa kwa siku. Ungesema kwa mwezi au mwaka labda ila siku ni muda mfupi sana.
 
Kwa siku? Mbona rahisi sana kuepuka hayo hasa kwa siku. Ungesema kwa mwezi au mwaka labda ila siku ni muda mfupi sana.
Kwa siku lazima uingie kingi mojawapo ya hizo dhambi, wewe inaweza pita siku hujasema uongo, hujatamani mwanamke asiye wako au hujadhulumu??
 
Kwa siku lazima uingie kingi mojawapo ya hizo dhambi, wewe inaweza pita siku hujasema uongo, hujatamani mwanamke asiye wako au hujadhulumu??

Siku inapita vizuri kabisa. Kudhulumu sijawahi my whole life actually. Uongo every now and then ila sio kila siku. Unadangaya kila siku kisa nini?

Kutamani pisi hapo ndo kipengele ila na yenyewe sio kila siku sasa. Hamna mambo mengine ya kuwaza?
 
kusengenya. ndo inabid iwe namba 1
 
Hata uwe mtu wa dini vipi kwa siku angalau utatenda mojawapo ya hizi dhambi.

1. Uongo

2. Uzinzi/uasherati

3. Dhuluma

4. Ubinafsi/Uchoyo

5. Chuki
Sio kweli hata kidogo. Hakuna dhambi isiyoepukika, ukiamua unaweza kuepuka kila aina ya dhambi.

Kama ingekuwa siyo rahisi kuepuka dhambi, BWANA MUNGU, asingemwambia Kaini maneno haya;

"tazama dhambi iko mlangoni inakuotea nayo inakutamani wewe, walakini yakupasa uishinde".

Zingatia hilo agizo la BWANA MUNGU "yakupasa uishinde". BWANA MUNGU alijua fika kuwa Mwanadamu anao uwezo wa kuishinda dhambi.
 
Back
Top Bottom