heartbeats
JF-Expert Member
- Feb 10, 2014
- 6,736
- 10,669
Namba 2 niaje?;Namba 3 mimi naweza kuiepuka kwa 99.999% sikumbuki kama nishawahi kudhulumu.
Dhuluma ni nini mkuuDhulma huanzia mbali kabisa utotoni.Unakula na wenzako halafu unamega matonge "manene" au kuchukua nyama harakaharaka kabla ya wenzako.Hiyo ni dhulma.Kumnyima mwenza wako mahaba bila sababu.Hiyo ni dhulma.Kumchapa mtoto kimakosa ni dhulma.Kutokusalimu wengine kwa kiburi tu ni dhulma.Kukataa kupisha wengine njiani ni dhulma.Kupewa kitu na kutosema asante ni dhulma nk.
Inawezekana kabisa kuacha zote hizo. Lakini hii inategemea na hofu yako kwa Mungu na kujua nini Mungu anataka utende na nini usitende. Mimi nilikuwa na hizo mbili za mwanzo ila kwa sasa nimezishinda kwa msaada wa Mungu miaka inakatika. Ni ngumu usipokuwa na Yesu ila Yesu akiingia ndani yako ya kale yanapita na yanakuwa mapya. Mkabidhi Yesu maisha yako atakufundisha jinsi gani ya kuzishinda hizo dhambi.Hata uwe mtu wa dini vipi kwa siku angalau utatenda mojawapo ya hizi dhambi.
1. Uongo
2. Uzinzi/uasherati
3. Dhuluma
4. Ubinafsi/Uchoyo
5. Chuki
😀😀😀 si ndio!!Dhambi ni mtazamo tu!
Hivi mimi nimekubaliana na mdada fresh sijamlaghai wala kumpa ahadi hewa, akaja geto jioni tukafurahia tofauti zetu asubuhi tukapiga supu akarudi kwake. Yeye kaenjoy mimi nimeenjoy afu mtu anasema tulichofanya ni dhambi
Kunyima au kupora/kuficha kilaghai kilicho stahiki,haki,manufaa,ridhio au hali stahili ya mwingine kwa kiburi,dharau na uonevu.Dhuluma ni nini mkuu
1&2 vinakubungua😀😀😜Namba 3 mimi naweza kuiepuka kwa 99.999% sikumbuki kama nishawahi kudhulumu.
Dhambi pekee inayoeleza hayo ni ya... 'Usitamani mwanamke asiyekuwa mke wako'Nasikia hata kuwazia tu hayo already utakuwa umetenda dhambi achilia mbali kuyafanya kwa vitendo
Kumega matonge makubwa makubwa na kuchukua nyama haraka haraka kumbe ni dhulma!Dhulma huanzia mbali kabisa utotoni.Unakula na wenzako halafu unamega matonge "manene" au kuchukua nyama harakaharaka kabla ya wenzako.Hiyo ni dhulma.Kumnyima mwenza wako mahaba bila sababu.Hiyo ni dhulma.Kumchapa mtoto kimakosa ni dhulma.Kutokusalimu wengine kwa kiburi tu ni dhulma.Kukataa kupisha wengine njiani ni dhulma.Kupewa kitu na kutosema asante ni dhulma nk.
Hii ya pili si dhambi kwani ni wajibu wa kila mtu au kiumbe wa Mwenyezi Mungu kuwajibika. Mungu ametupa alivyotupa ili tupeane na kuburudishana.Hata uwe mtu wa dini vipi kwa siku angalau utatenda mojawapo ya hizi dhambi.
1. Uongo
2. Uzinzi/uasherati
3. Dhuluma
4. Ubinafsi/Uchoyo
5. Chuki
Dhulma kubwa sana.Ndiyo chanzo cha wizi na ufisadi/uchoyo/ubinafsi na dharau kwa wengine kwa kuwaona dhalili.Kumega matonge makubwa makubwa na kuchukua nyama haraka haraka kumbe ni dhulma!
Ndiyo maana tumebadili mtindo wa nidhamu ya chakula mezani siku hizi.
Kila mtu na sahani yake, atajaziwa kwa kujichotea ama kugawiwa.
Hii hupunguza sana hiyo tabia ya uroho ama dhulma.
Kwa siku lazima uingie kingi mojawapo ya hizo dhambi, wewe inaweza pita siku hujasema uongo, hujatamani mwanamke asiye wako au hujadhulumu??Kwa siku? Mbona rahisi sana kuepuka hayo hasa kwa siku. Ungesema kwa mwezi au mwaka labda ila siku ni muda mfupi sana.
Kwa siku lazima uingie kingi mojawapo ya hizo dhambi, wewe inaweza pita siku hujasema uongo, hujatamani mwanamke asiye wako au hujadhulumu??
Sio kweli hata kidogo. Hakuna dhambi isiyoepukika, ukiamua unaweza kuepuka kila aina ya dhambi.Hata uwe mtu wa dini vipi kwa siku angalau utatenda mojawapo ya hizi dhambi.
1. Uongo
2. Uzinzi/uasherati
3. Dhuluma
4. Ubinafsi/Uchoyo
5. Chuki