Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

dogo kalishwa matapishi afu kayameza kama yalivyo. shetani mbaya sana. halafu shetani hajampa hata mistari ya kusimamia, ila anasema ni maagizo ya Mungu.
 
Yaani fedha unampa mchugaji harafu unasema humfaidishi
Hujui SHERIA ya kiroho inavyofanya KAZI.

Usilolijua ni kuwa, kipato upewacho Huwa ni njia ya kufikia wengine,

Ndani ya kipato chako Kuna pesa Kwa ajili Yako, pesa ingine imepitishwa kwako Kwa ajili ya wahitaji,

Kwenye kipato hicho hicho Kuna mbegu nk nk,

Atoaye ndiye apokeaye katika Roho, na apokeaye KIMWILI ndiye Atoaye katika Roho.

Hujui matajiri ambao huwaita maskini na kuwapa sadaka Huwa wanachukua baraka za maskini hao na kujiongezea utajiri.?

Imeandikwa heri Kutoa kuliko kupokea.

Soma thread: DAWA ya Umaskini, madeni, ukata, mifuko kutoboka, uhitaji, kufilisika hii hapa - Rabbon

Itakusaidia Amen
 
Mmeona kupiga kelele masokoni haitoshi mkaamua mje huku walokole wenye vidole!
 
hakuna sheria ya kiroho iliyo nje ya Neno la Mungu wewe. acha kudanganya watu. huoni aibu?
 

Lakini mistari hiyo inaelezea hatma ya wanaotenda dhambi zilizotajwa...

Haioneshi namna ambayo mtenda dhambi tajwa inapaswa atubu au ajutie dhambi zake kwa namna "Nabii" alivyoeleza...

Maana biblia inaweka wazi kwamba afanyaye dhambi inampasa kutubu, lakini sikumbuki kuona namna hii ya kutubu kwa kumfuata "pastor, kuhani, mchungaji, askofu n.k" kama imetajwa...
 
Ujinga tu na fundisho la kipumbavu hiyo sadaka ya ukombozi ya nini inamana kazi ya msalaba ilikuwa na upungufu

Alafu anayesamehe ni Mungu huyo huyo nani anaejipa hatimiliki ya kuniambiwa siwezi kusamehewa mpaka niombewe na yeye

Mbona tunarudishana agano la kale hebu acheni kushare mafundisho manyonge na potofu
 
Hukusoma Yesu akisema nimwafundisha machache, Roho mtakatifu atawafundisha Kweli yote.

Ninakushauri ikiwa umeokoka, ingia katika maombi, Roho mtakatifu akuthibitishie ikiwa neno na maelekezo hapo juu ni yake au la.
 
Shida si sadaka mkuu shida ni kuacha kukombolewa Kwa kazi ya msalaba na kutumia sadaka
hivyo ni sawa na kusema ukombozi Wa Kristo hauna nguvu ya kukukomboa

Si madharau hayo sasa
 
Hukusoma Yesu akisema nimwafundisha machache, Roho mtakatifu atawafundisha Kweli yote.

Ninakushauri ikiwa umeokoka, ingia katika maombi, Roho mtakatifu akuthibitishie ikiwa neno na maelekezo hapo juu ni yake au la.
ninakuombea tu kwa Mungu akusaidie, kwasababu fundisho lako hilo umelishwa na mtume wako, na ni ngumu sana kutoka kwenye kifungo chako hicho. inaumiza sana, ndio maana tunasenma mitume na manabii wa uongo wauza mafuta na keki za upako ni adui wa mwanadamu kama alivyo shetani tu kwasababu wakiweka doctrine kwa mtu, hata umsaidiaje haelewi ni kama wanaondoka na ubongo wote anabaki hana kitu.
 
Hakuna Mahali pameandikwa kuwa sadaka tutoazo zinakaa Badala ya Damu ya Yesu.

Kila kitu kina KAZI yake, sadaka Ina KAZI yake, sadaka Ina KAZI yake.

Ubarikiwe.
 
Shida si sadaka mkuu shida ni kuacha kukombolewa Kwa kazi ya msalaba na kutumia sadaka
hivyo ni sawa na kusema ukombozi Wa Kristo hauna nguvu ya kukukomboa

Si madharau hayo sasa
manake anataka kusema kifo cha Yesu hakikutosha, lile kafara la Yesu lilitosha hauhitaji kingine chochote, unapata msamaha bure tena wa neema. wa neema kwasababu hatustahili tulitakiwa kuuawa ila yeye akauawa kwa ajili yetu ili wamwendeao wapate ukombozi bure. hauhitaji kulipa chochote.
 
Narudia tena: Mafunzo yoyote yanayotaja sadaka ya ukombozi ni mafunzo ya kipepo, yanatoka kuzimu.
Mwakasege kwa makusudi au kwa kutokujua anatumiwa na Ibilisi kueneza mafunzo ya sadaka ya ukombozi.
Kama mwanadamu angekuwa na namna yoyote ya kujikomboa kwa sadaka basi Yesu asingekuja duniani.
Jina na damu ya Yesu vinatosha.
Vinatosha.
 
Roho mtakatifu ndiye aliyetoa ujumbe huo kupitia mtumishi wake.

Kabla ya kupinga, ikiwa umejazwa Roho mtakatifu, omba akuthibitishie ikiwa ujumbe huo umetoka kwake au la.
Acha kumuhusisha Roho mtakatifu kwenye upuuzi mkuu huyo nabii kunasiku atatamani yakati zirudi Nyuma afute pumba hizi nakuhakikishia hilo

Kwa ufinyu Wa maarifa na mihemko na uchanga Wa Kiroho wengi walifundisha pumba na wakasema asema Bwana

Baada ya kukua na kuelewa neno vyema walitamani siku zirudi nyuma wafutte ujinga wao
 
Hakuna Mahali pameandikwa kuwa sadaka tutoazo zinakaa Badala ya Damu ya Yesu.

Kila kitu kina KAZI yake, sadaka Ina KAZI yake, sadaka Ina KAZI yake.

Ubarikiwe.
hivi wewe mwenyewe unajiona unaelewa? unajua inawezekana tunajadiliana na majini humu wengine sio watu, wapo kwaajili ya kupotosha Neno la Mungu na wametumwa kabisa toka kuzimu.
 
Hongera Kwa kuwa miongoni mwa walioifahamu kweli hakika upo huru kwelikweli

Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
 
bora wewe umefunguka. hili ni fundisho la mwalimu wao, pamoja na lile la ukombozi wa mzaliwa wa kwanza. alishaambiwa aokoke kitambo sana ila yeye ameng'ang'ania lutheran kwasababu ya sadaka, ndio anafundisha watu mambo ya aina hii.
 
Shida si sadaka mkuu shida ni kuacha kukombolewa Kwa kazi ya msalaba na kutumia sadaka
hivyo ni sawa na kusema ukombozi Wa Kristo hauna nguvu ya kukukomboa

Si madharau hayo sasa
Wewe ndiye unapotosha. Kubeba sadaka ni kutimiza tu agizo kuwa,

Tusiende nyumbani mwa BWANA mikono mitupu,

Yesu Kristo, alimwona mjane maskini akitoa chote kidogo alicho nacho, hakumkataza.

Kutoa Si kumnunua Mungu au kununua Muujiza, ni shukrani. Na kuweka ulinzi juu ya kipato chako Ili mwovu asikiharibu.

Muhimu uelewe, zipo dhambi kamwe huwezi tubu gizani bila kushare na mtumishi wa Mungu wa Kweli.

Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…