Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

dogo kalishwa matapishi afu kayameza kama yalivyo. shetani mbaya sana. halafu shetani hajampa hata mistari ya kusimamia, ila anasema ni maagizo ya Mungu.
 
Yaani fedha unampa mchugaji harafu unasema humfaidishi
Hujui SHERIA ya kiroho inavyofanya KAZI.

Usilolijua ni kuwa, kipato upewacho Huwa ni njia ya kufikia wengine,

Ndani ya kipato chako Kuna pesa Kwa ajili Yako, pesa ingine imepitishwa kwako Kwa ajili ya wahitaji,

Kwenye kipato hicho hicho Kuna mbegu nk nk,

Atoaye ndiye apokeaye katika Roho, na apokeaye KIMWILI ndiye Atoaye katika Roho.

Hujui matajiri ambao huwaita maskini na kuwapa sadaka Huwa wanachukua baraka za maskini hao na kujiongezea utajiri.?

Imeandikwa heri Kutoa kuliko kupokea.

Soma thread: DAWA ya Umaskini, madeni, ukata, mifuko kutoboka, uhitaji, kufilisika hii hapa - Rabbon

Itakusaidia Amen
 
Mmeona kupiga kelele masokoni haitoshi mkaamua mje huku walokole wenye vidole!
 
Hujui SHERIA ya kiroho inavyofanya KAZI.

Usilolijua ni kuwa, kipato upewacho Huwa ni njia ya kufikia wengine,

Ndani ya kipato chako Kuna pesa Kwa ajili Yako, pesa ingine imepitishwa kwako Kwa ajili ya wahitaji,

Kwenye kipato hicho hicho Kuna mbegu nk nk,

Atoaye ndiye apokeaye katika Roho, na apokeaye KIMWILI ndiye Atoaye katika Roho.

Hujui matajiri ambao huwaita maskini na kuwapa sadaka Huwa wanachukua baraka za maskini hao na kujiongezea utajiri.?

Imeandikwa heri Kutoa kuliko kupokea.

Soma thread: DAWA ya Umaskini, madeni, ukata, mifuko kutoboka, uhitaji, kufilisika hii hapa - Rabbon

Itakusaidia Amen
hakuna sheria ya kiroho iliyo nje ya Neno la Mungu wewe. acha kudanganya watu. huoni aibu?
 
(1 Wakorintho 6:9-10)
Au hamjui ya kuwa, wadhalimu, hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike, waasherati, hawataurithi ufalme wa Mungu,

Wala WAABUDU SANAMU, Wala wazinzi, Wala wafirahi, Wala WALAWITI,Wala wevi, Wala watamanio, Wala WALEVI, Wala watukanaji, Wala wanyanganyi.

(Ufunuo 21:8)

Bali waoga, na wasioamini,na wachukizao, na wauwaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote,sehemu Yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo MAUTI ya pili.

Lakini mistari hiyo inaelezea hatma ya wanaotenda dhambi zilizotajwa...

Haioneshi namna ambayo mtenda dhambi tajwa inapaswa atubu au ajutie dhambi zake kwa namna "Nabii" alivyoeleza...

Maana biblia inaweka wazi kwamba afanyaye dhambi inampasa kutubu, lakini sikumbuki kuona namna hii ya kutubu kwa kumfuata "pastor, kuhani, mchungaji, askofu n.k" kama imetajwa...
 
Salaam shalom.

INTRODUCTON.

Imeandikwa, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na haki, hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.( 1 Yoh 1:9).

Dhambi ni kutotii, kwenda kinyume na maelekezo ya Mungu. Na Roho mtakatifu yupo kutukumbusha dhambi zetu Ili tuzitibie Ili tuendelee kuwa WATAKATIFU.

DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

1. ZINAA NA UASHERATI.

UASHERATI ni kufanya Tendo la zinaa na mtu nje ya NDOA asiye mkeo au mumeo.

UZINZI ni kufanya tendo la uchafu, zinaa kabla ya Kuoa au Kuolewa.

Ukizini na mke wa mtu au mume wa Mtu, usijidanganye kuwa ukitubu sirini utasamehewa, HATIA itaendelea kuwepo Hadi uwatafute watumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi. Watumishi Wana BUSARA ya kusuluhisha dhambi hiyo pande zote mbili Ili ufunguliwe.

2. USHOGA.

Ikiwa uliwahi kuwa shoga, ukaamua kuacha, kamwe usitubu sirini na kuishiwa hapo, USHOGA huambatana na mapepo na kufungwa NAFSI, mfungwa kamwe hawezi jifunguanpingu mwenyewe, unawahutaji watumishi wa Kweli Ili UOMBEWE na kuwekwa huru, sadaka ni LAZIMA Ili itolewe huko.

3. USAGAJI.

Mwanamke pia aliyewa kufanya dhambi hiyo, huwezi kufunguliwa na Utumwa na HATIA hiyo pekeako Kwa kutubu sirini, nenda Kwa watumishi wa Kweli, Ukiwa na sadaka ya Ukombozi.

4. PUNYETO/ KUJICHUA.

Ikiwa uliwahi kujichua, ukaamua kuacha, unahitaji kwenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi Ili ufunguliwe, Mpiga PUNYETO ni mfungwa, ni mke au mume wa Roho chafu katika Ulimwengu wa Roho, hivyo kufunguliwa ni LAZIMA utoe sadaka, uvunje NDOA chafu hiyo ya kiroho na hati ya NDOA chafu ya kiroho iondolewe, usipofanya hivyo, unajidanganya. Mbinguni huingii ng'o!!
Neno Hilo hapo juu ni ROHO. Amen.

5.MWANAMKE KUOA MWANAMKE/MWANAUME KUOA MWANAUME MWENZIE.

Kutubu dhambi hii sirini bila watumishi wa Mungu ni kujidanganya. Chukua sadaka, nenda Kwa mtumishi, Sema Kweli Ili UOMBEWE na kufunguliwa, NDOA haramu ivunjwe na ufungwa wako kiroho uondolewe. Amen.

6. ORAL SEX.

Ikiwa uliwahi kushiriki oral sex, kunyonya au kuramba Kwa mdomo sehemu za Siri za mwanamke au Mwanaume na ukatambua ni DHAMBI, ukaacha, Bado u kifungoni.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli wa Mungu ufunguliwe na Mungu.

7. ABORTION./ UTOAJI MIMBA/ KUFUNGA UZAZI/ KUTUMIA VIDONGE VYA KUPANGA UZAZI.

Kimbia haraka Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli ,beba sadaka kulingana na uwezo wako, UOMBEWE ufunguliwe.

Ukipuuza Utakataliwa GETI la Mbinguni.

9. IKIWA ULIWAHI TUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME/ KIKE.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.

10. MAUAJI.

Ikiwa uliwahi kuua bila kukusudia ,ukahukumiwa JELA ukatoka, ikiwa uliua Kwa Siri na hukubainika, ikiwa ulishiriki kuua, usijidanganye kuwa unaweza kutubu sirini, HATIA Ili ikuondoke uwe na Amani, Tafuta kiongozi wa Mungu wa Kweli mwenye BUSARA za Mungu, akuongoze Cha kufanya, utoe pia sadaka ya Ukombozi.

11. IBADA ZA SANAMU, KUSHIRIKI IBADA ZA WAFU NA KUTOA SADAKA KWA MIZIMU KIMILA NK NK.

Kushiriki Ibada za KIMILA na Kutoa sadaka Kwa Roho za kishetani za Mababu, ni DHAMBI pia, ni kufungwa ni Utumwa ambao huwezi kujifungua pekeako.

Ukiamua kuacha na kuokoka, hatua inayofuata ni kushirikisha watumishi kukusaidia kukutenga na madhabahu hizo.

Sadaka ni LAZIMA, sababu, Ulimwengu wa Nuru na Giza sadaka ni inevitable. Amen

HITIMISHO.

Dhambi nilizotaja hapo juu, ni baadhi tu ya dhambi ambazo huwezi tubu pekeako, zimetajwa sawasawa na Ruhusa ya Roho mtakatifu Kwa mtumishi wake sawasawa na ufunuo wake apendavyo.

NB: Si DHAMBI zote zinahitaji kuona mtumishi wa Kweli kukusaidia kufunguliwa pingu za dhambi, ni baadhi ya dhambi ambazo Zina vifungo na attachment na maagano ya kipepo na kishetani.

Mungu awabariki.

Source: Nabii Justine Ibrahim.

Amen.
Ujinga tu na fundisho la kipumbavu hiyo sadaka ya ukombozi ya nini inamana kazi ya msalaba ilikuwa na upungufu

Alafu anayesamehe ni Mungu huyo huyo nani anaejipa hatimiliki ya kuniambiwa siwezi kusamehewa mpaka niombewe na yeye

Mbona tunarudishana agano la kale hebu acheni kushare mafundisho manyonge na potofu
 
Lakini mistari hiyo inaelezea hatma ya wanaotenda dhambi zilizotajwa...

Haioneshi namna ambayo mtenda dhambi tajwa inapaswa atubu au ajutie dhambi zake kwa namna "Nabii" alivyoeleza...

Maana biblia inaweka wazi kwamba afanyaye dhambi inampasa kutubu, lakini sikumbuki kuona namna hii ya kutubu kwa kumfuata "pastor, kuhani, mchungaji, askofu n.k" kama imetajwa...
Hukusoma Yesu akisema nimwafundisha machache, Roho mtakatifu atawafundisha Kweli yote.

Ninakushauri ikiwa umeokoka, ingia katika maombi, Roho mtakatifu akuthibitishie ikiwa neno na maelekezo hapo juu ni yake au la.
 
Ikiwa Mungu alimtoa mwanawe wa pekee Yesu kristo awe sadaka ya kutukomboa,

Nani wewe usitoe sadaka. Sadaka ni Kwa ajili Yako, usidhani unamfaidisha Mchungaji.

Elia alilishwa na Mungu kupitia kunguru, usidhani watumishi wa Mungu wanategenea sadaka zako.

Na usijidanganye ukaenda Kutoa sadaka ya wizi, au ya kutapeli madhabahuni, utaondoka na LAANA.

Ubarikiwe.
Shida si sadaka mkuu shida ni kuacha kukombolewa Kwa kazi ya msalaba na kutumia sadaka
hivyo ni sawa na kusema ukombozi Wa Kristo hauna nguvu ya kukukomboa

Si madharau hayo sasa
 
Hukusoma Yesu akisema nimwafundisha machache, Roho mtakatifu atawafundisha Kweli yote.

Ninakushauri ikiwa umeokoka, ingia katika maombi, Roho mtakatifu akuthibitishie ikiwa neno na maelekezo hapo juu ni yake au la.
ninakuombea tu kwa Mungu akusaidie, kwasababu fundisho lako hilo umelishwa na mtume wako, na ni ngumu sana kutoka kwenye kifungo chako hicho. inaumiza sana, ndio maana tunasenma mitume na manabii wa uongo wauza mafuta na keki za upako ni adui wa mwanadamu kama alivyo shetani tu kwasababu wakiweka doctrine kwa mtu, hata umsaidiaje haelewi ni kama wanaondoka na ubongo wote anabaki hana kitu.
 
Ujinga tu na fundisho la kipumbavu hiyo sadaka ya ukombozi ya nini inamana kazi ya msalaba ilikuwa na upungufu

Alafu anayesamehe ni Mungu huyo huyo nani anaejipa hatimiliki ya kuniambiwa siwezi kusamehewa mpaka niombewe na yeye

Mbona tunarudishana agano la kale hebu acheni kushare mafundisho manyonge na potofu
Hakuna Mahali pameandikwa kuwa sadaka tutoazo zinakaa Badala ya Damu ya Yesu.

Kila kitu kina KAZI yake, sadaka Ina KAZI yake, sadaka Ina KAZI yake.

Ubarikiwe.
 
Shida si sadaka mkuu shida ni kuacha kukombolewa Kwa kazi ya msalaba na kutumia sadaka
hivyo ni sawa na kusema ukombozi Wa Kristo hauna nguvu ya kukukomboa

Si madharau hayo sasa
manake anataka kusema kifo cha Yesu hakikutosha, lile kafara la Yesu lilitosha hauhitaji kingine chochote, unapata msamaha bure tena wa neema. wa neema kwasababu hatustahili tulitakiwa kuuawa ila yeye akauawa kwa ajili yetu ili wamwendeao wapate ukombozi bure. hauhitaji kulipa chochote.
 
MATENDO 9:3 - 6 INASEMA:

Wakati alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafla nuru kutoka mbinguni ikamwangaza kotekote. 4Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona wanitesa? 5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayemtesa. 6Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. 7Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, waliisikia sauti, lakini hawakuona mtu. 8Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.

HAYA WEWE SASA TUAMBIE WAPI HAPO SAULI/PAULO ALITUBU KWA KUPELEKA SADAKA KWA MCHUNGAJI, manake tunachopishana na wewe hapa ni kwanini ubebe sadaka wakati unaenda kutubu, huoni kama umepigwa sana na hao manabii?

wewe ndio wale wanaokotaka kimstari kimoja afu wanaenda kufungua hadi kanisa, wanajiita wachungaji kufundisha watu mapotofu kama hayo.
Narudia tena: Mafunzo yoyote yanayotaja sadaka ya ukombozi ni mafunzo ya kipepo, yanatoka kuzimu.
Mwakasege kwa makusudi au kwa kutokujua anatumiwa na Ibilisi kueneza mafunzo ya sadaka ya ukombozi.
Kama mwanadamu angekuwa na namna yoyote ya kujikomboa kwa sadaka basi Yesu asingekuja duniani.
Jina na damu ya Yesu vinatosha.
Vinatosha.
 
Roho mtakatifu ndiye aliyetoa ujumbe huo kupitia mtumishi wake.

Kabla ya kupinga, ikiwa umejazwa Roho mtakatifu, omba akuthibitishie ikiwa ujumbe huo umetoka kwake au la.
Acha kumuhusisha Roho mtakatifu kwenye upuuzi mkuu huyo nabii kunasiku atatamani yakati zirudi Nyuma afute pumba hizi nakuhakikishia hilo

Kwa ufinyu Wa maarifa na mihemko na uchanga Wa Kiroho wengi walifundisha pumba na wakasema asema Bwana

Baada ya kukua na kuelewa neno vyema walitamani siku zirudi nyuma wafutte ujinga wao
 
Hakuna Mahali pameandikwa kuwa sadaka tutoazo zinakaa Badala ya Damu ya Yesu.

Kila kitu kina KAZI yake, sadaka Ina KAZI yake, sadaka Ina KAZI yake.

Ubarikiwe.
hivi wewe mwenyewe unajiona unaelewa? unajua inawezekana tunajadiliana na majini humu wengine sio watu, wapo kwaajili ya kupotosha Neno la Mungu na wametumwa kabisa toka kuzimu.
 
manake anataka kusema kifo cha Yesu hakikutosha, lile kafara la Yesu lilitosha hauhitaji kingine chochote, unapata msamaha bure tena wa neema. wa neema kwasababu hatustahili tulitakiwa kuuawa ila yeye akauawa kwa ajili yetu ili wamwendeao wapate ukombozi bure. hauhitaji kulipa chochote.
Hongera Kwa kuwa miongoni mwa walioifahamu kweli hakika upo huru kwelikweli

Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
 
Narudia tena: Mafunzo yoyote yanayotaja sadaka ya ukombozi ni mafunzo ya kipepo, yanatoka kuzimu.
Mwakasege kwa makusudi au kwa kutokujua anatumiwa na Ibilisi kueneza mafunzo ya sadaka ya ukombozi.
Kama mwanadamu angekuwa na namna yoyote ya kujikomboa kwa sadaka basi Yesu asingekuja duniani.
Jina na damu ya Yesu vinatosha.
Vinatosha.
bora wewe umefunguka. hili ni fundisho la mwalimu wao, pamoja na lile la ukombozi wa mzaliwa wa kwanza. alishaambiwa aokoke kitambo sana ila yeye ameng'ang'ania lutheran kwasababu ya sadaka, ndio anafundisha watu mambo ya aina hii.
 
Shida si sadaka mkuu shida ni kuacha kukombolewa Kwa kazi ya msalaba na kutumia sadaka
hivyo ni sawa na kusema ukombozi Wa Kristo hauna nguvu ya kukukomboa

Si madharau hayo sasa
Wewe ndiye unapotosha. Kubeba sadaka ni kutimiza tu agizo kuwa,

Tusiende nyumbani mwa BWANA mikono mitupu,

Yesu Kristo, alimwona mjane maskini akitoa chote kidogo alicho nacho, hakumkataza.

Kutoa Si kumnunua Mungu au kununua Muujiza, ni shukrani. Na kuweka ulinzi juu ya kipato chako Ili mwovu asikiharibu.

Muhimu uelewe, zipo dhambi kamwe huwezi tubu gizani bila kushare na mtumishi wa Mungu wa Kweli.

Amen
 
Back
Top Bottom