Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Umwombe radhi muibiwa Tena… you can’t be serious 🧐
Ndo maana ya kumwambia zipo dhambi huwezi tubu pekeako,

Soma (Mathayo 5:25), yasema patana na mshitaki wako muwapo njiani kabla hajakupeleka Kwa kadhi, kadhi akakupeleka Kwa liwali, ukatupwa GEREZANI.

Dhambi ya UZINZI ni Moja wapo inayomfanya aliyeitenda kuwa gerezani.

Maana ya kuwa gerezani ni ugumu uliouongelea wa mazingira ya kumalizana na kupata msamaha Kwa uliyemuibia Mume, Mungu anataka umwombe radhi akusamehe ndipo Mungu akusamehe.

Ukitubu pekeako unajidanganya, ndomana ninashauri TUMIA mtumishi wa Mungu asaidie kukupatanisha upate msamaha wake.

Tofauti na hapo, ukitubu bila kufanya hivyo, dhambi hiyo haikuondoki, na ukifa ni Kuzimu direct.

Amen
 
Kumbe tangazo la biashara ya Nabii feki Justine...
 
nimekufatilia tangu mwanzo wa uzi wako nilitegemea nitaona umetoa fungu la biblia linalokusapot twende kuombewa kwa mtumishi, lakini naona porojo za kupiga sadaka tu
Rudi kusoma,

KATIKA Kila category nimeambatisha na vifungu vya maandiko ya BIBLIA.
 
Kah maokoto yamezingatiwa sana aisee eti Mungu alimtoa mwanae
 
Tukirudi kwenye uhalisia wa kutubu na kusamehewa, uhalali wa kwamba lazima ukatubu pamoja na mtumishi unatoka wapi?.

Maana kufa kwa Yesu msalabani kulipunguza formalities nyingi sana, kipindi cha Torati watu waliishi kwa sheria, bali sisi tunaishi kwa neema.

Yesu alisema hakuja kuivunja torati bali kuitimiliza. Tafsiri yake kuna mambo yaliwekwa sawa baada ya yeye kuja duniani kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu.

Mwisho kabisa, yule mwanamke aliyezini na wakataka kumpiga mawe na akaletwa mbele ya Yesu, embu tuambie, alipelekwa kwa kuhani gani ambaye alimuombea ili dhambi zake zisamehewe?
 
Mwanamke aliyezini aliletwa Kwa Yesu Ili Yesu atoe HUKUMU.

Mahakama Ile ikifanyika wazi mchana kweupe, Yesu akamsamehe na kumwambia usifanye dhambi tena.

Paulo alipotokewa na YESU na kupigwa upofu, aliambiwa nenda mjini utamkuta mtumishi atakuombea,

Wakati Paulo anaambiwa hayo, tayari lilikuwa kipindi Cha neema.

Mchawi Kwa Mfano, Unadhani anaweza kutubu mwenyewe chumbani anaweza kuvunja mikataba ya kichawi aliyofunga na shetani?

Leo ukizini na mke wa mtu, unaamini unaweza kutubu pekeako chumbani, mwenye mume akakusamehe na Mungu akakuondolea HATIA moyoni?

Kizazi hiki mbona hamtaki kuambiwa Kweli ya Mungu?
 
Haya mafundisho ya lazima ukatubu kwa mtumishi mnayatoa wapi kiongozi?.

Huyo mtumishi yeye akifanya dhambi anatubu mbele ya nani?. Mwanadamu ni nani mpaka atumike kama daraja la kusamehe dhambi?.

Yesu mwenyewe alisema tukiomba kwa jina lake, hiyo ndo connection tuliyonayo kati ya Mungu na Mwanadamu.

Sipingi watumishi kuombea watu, ila siaminj katika kauli ya dhambi fulani haisameheki isipokuwa kuwe na intervention ya mwanadamu katikati.
 
Nimekuuliza mchawi anaweza kujifungia ndani akatubu pekeake na kujitenga na mikataba ya kichawi pekeake?

Nimekuuliza, ukizini na mke wa mtu, ukijifungia ndani pekeako ukatubu bila kumwomba msamaha mwibiwa mke Kwa msaada wa watumishi wa Mungu unaamini Mungu atakusamehe?

Hivi m asomaga maandiko na kuyaelewa Kweli?

Ujuaji unakusaidia nini kuondoa Giza kichwani mwako?
 
Picha linaanza kushindwa kutofautisha kati ya uzinzi na uasherati
 
We umezaliwa na mwanamke tu huwezi kujifanya huna dhambi na hao watumishi pia wana dhambi ova
 
Huu ni upuuzi kiwango cha juu kbs karne hii ya sayansi na technology, hao unaewambia dhambi hizo nao wanazitenda. Wao wenyew wanahamasisha ushoga we uende ukawaungamie, amkeni acheni ujinga na upumbavu.
 
Kwani Kutubu ni nini?
 
Kwanza tunatakiwa Tuanze hapo kwenye neno Kutubu,
Kutubu ni kugeza mtazamo
Wayahudi siku zote waliamini katika torati na mafundisho ya Musa kwamba yangewapatia haki mbele za Mungu Lakini haikuwezekana
Yesu anakuja anawaambia, Matthew 4v17 watubu yaani waigeukie injili, habari njema (waachane na torati ambayo si njema) ambayo kwa hiyo injili wataingia kwenye ufalme wa Mungu yaani watahesabiwa haki
Kwa hiyo KUTUBU ni kuacha TORATI na kuiamini INJILI kwa mujibu wa bibilia
 
Neema ni mlango mgumu kuliko hata Ule wa SHERIA ya Musa.

Anania na Saphira waliishi kipindi Cha neema, lakini neema hiyo haikuwapa kuishi walipomdanganya Roho mtakatifu.

Kuwapo katika kipindi Cha neema, hakikupi Ruhusa ya kuzini na mke wa mtu Kisha ukapiga kimya na kujidanganya Eti utafunikwa na neema.

Yaliyoandikwa hapo juu ni maelekezo ya Mungu kupitia Roho MTAKATIFU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…