Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Wewe unasema neema ni mlango mgumu
Wakati Yesu alisema watu waende kwake maana nira yake ni laini na mizigo wake ni wepesi
Sasa huyo roho uliyenaye mbona kama anajipinga vile
Mimi najua ni neema pekee ndiyo inayoweza kumfanya mtu aweze kukataa hayo unayoyaita wewe kwamba ni matendo mabaya ambapo sheria ilishindwa,Warumi 8:3
 
Mbona unakwepa kujibu,

Neema inatoa Utaratibu Gani wa mtu aliyeanguka dhambini , aliyeokoka, amjuaye Mungu, Kwa kuzini na mke wa mtu?

Ni sawa tutubu chumbani pekeako na kuamini umesamehewa?

Jibu Hilo, acha chenga.
 

Biblia inasema nini kuhusu Roho Mtakatifu:

"Unapoituma Roho wako, vinaumbwa, nawe waufanya upya uso wa nchi. (Kutoka Biblia ya NIV, Zaburi 104:30)"

Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Nitakimbilia wapi uso wako? (Kutoka Biblia ya NIV, Zaburi 139:7)

"Unifundishe kuyafanya mapenzi yako, kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema na unitongoze mahali tambarare. (Kutoka Biblia ya NIV, Zaburi 143:10)"

mistari hii inazungumza juu ya Roho kutoka kwa MUNGU Mwenyezi.

Mstari wa kwanza hapo juu, Zaburi 104:30, unakubaliana kikamilifu na Mistari Adhimu hapo juu kuhusu MUNGU Mwenyezi Akiipulizia Roho yake ndani ya matumbo ya mama zetu tukiwa fetusi.


 
Mbona unakwepa kujibu,

Neema inatoa Utaratibu Gani wa mtu aliyeanguka dhambini , aliyeokoka, amjuaye Mungu, Kwa kuzini na mke wa mtu?

Ni sawa tutubu chumbani pekeako na kuamini umesamehewa?

Jibu Hilo, acha chenga.
Kwa nini uzinzi tu lakini?
Fikiria jamaa amekukamata na akakufanya chochote hata kukuauwa, na haujapata nafasi ya kwenda kwa mchungaji wako, itakuwaje hapo? Utaenda motoni eti si ndiyo unavyo fikiria
 
Kwa nini uzinzi tu lakini?
Fikiria jamaa amekukamata na akakufanya chochote hata kukuauwa, na haujapata nafasi ya kwenda kwa mchungaji wako, itakuwaje hapo? Utaenda motoni eti si ndiyo unavyo fikiria
Acha chenga.

Naongelea uliyezini na hukukamatwa, katika kipindi hiki unachoita Cha neema,

Ni sawa kutubu pekeako kimya kimya, bila mkeo kujua ulichofanya, bila mume wa uliyezini naye kujua na kusamehe?

Jibu Hilo, usilete siasa.
 
"Mbingu ipo na ndimo Mungu anamokaa"
Kwani Mungu anakaa?
Mbingu ipo na ndimo Mungu anamokaa.
Kuhusu dhambi, hakuna dhambi, zote zilichukuliwa na Yesu,
Dhambi ya kumkufuru roho ni mtu kutokuamini ya kwamba Mungu alimtoa mwanaye kama ondoleo la dhambi ili kila aaminie asife bali aishi
 
Exactly
 
Kwangu mimi naona dhambi kubwa kuliko zote ni ile ya kujiondoa uhai(Kujinyonga hadi kufa,kujipiga bastola nk)

Dhambi nyingine zote,mtu anakuwa na fursa ya kupatana na Mungu kwa njia ya toba(Kutubu).

Dhambi ya kujiondoa uhai inakuwa kubwa kwasababu mtu anakuwa ameondoa uhai wake mwenyewe.

Anakuwa amekiuka amri ya Mungu inayosema usiue,na wakati huohuo anakuwa amejiondolea fursa ya kuweza kutubu(Toba).
 
Anayesamehe dhambi ni Mungu.

Mtumishi wa Mungu ni chombo chake na msaada wa kukufungua pingu wewe uliye mtumwa.

Amen
Watumishi wa Mungu waadilifu wamebaki wachache siku hizi.
Wengi wanakwenda kimwili..hii inaondoa kuaminiwa na jamii.
Hili nalo hulioni?
Na Mtumishi naye akitenda dhambi,akatubie kwa nani?
Je,Biblia imeweka utaratibu gani katika Toba?
 
mkuu
Katika kutafuta toba kwa Mungu hakuna masharti zaidi ya kumuamini Bwana Yesu Kristo kwamba alikufa kwa ajili ya dhambi zetu na kupitia toba ya kumaanisha kuacha dhambi tunasamehewa dhambi zetu.

Hayo ya kusema baadhi ya dhambi lazima Mtumishi wa Mungu ndo akutubishe ama akuongoze ni sawa na kuweka Lango jipya zaidi ya Yesu Kristo ili kumfikia Baba kwa minajili ya ondoleo la dhambi.

Yesu aliweka category mbili za dhambi,
  1. Dhambi zote atendazo mwanadamu dhidi ya mwanadamu -- Hizi zote zinasameheka kwa toba ya kumaanisha kuziacha
  2. Dhambi atendayo mwanadamu dhidi ya Mungu nayo ni Kumkufuru ROHO MTAKATIFU -- Hii HAISAMEHEKI hata ufanye toba ya kuongozwa na mitume na manabii. Pia hii mpaka uifanye unakuwa umefungua mageti mengi sana kumsogelea Mungu na kuzijua siri za Mbinguni na kuishi katika tumaini la Roho Mtakatifu. Hivyo ukimsaliti unakuwa fungu moja na ibilisi muasi ambaye tayari adhabu yake imewekwa tangu kale
Tunachohitaji kutoka kwa Watumishi yaani mitume na manabii ni muongozo namna ya kukisogelea Kiti cha Enzi cha Mungu Baba kwa unyenyekevu, kujikana, kujuta na kutubu kwa kumaanisha kuziacha dhambi.
 
Watumishi wa Mungu waadilifu wamebaki wachache siku hizi.
Wengi wanakwenda kimwili..hii inaondoka kuaminiwa na jamii.
Hili nalo hulioni?
Na Mtumishi naye akitenda dhambi,akatubie kwa nani?
Je,Biblia imeweka utaratibu gani katika Toba?
Upo Sahihi

Ikumbukwe yule Towashi aliyekutana na Philipo alifanya maamuzi yake binafsi baada ya kusikia Neno na siyo kuongozwa kutubu. Alisema, hapa kuna maji kwa nini nisibatizwe? Yusufu akamjibu kuwa Ukiamini kwa moyo wako wote... naye akasema Naamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. Akabatizwa.

Kila mmoja ana style yake ya kujileta kwa Mungu.

Kuna wakati Yesu akiwa kwenye Sinagogi (msikiti) anafundisha na watu wamemsonga sana. Familia fulani walitaka ndugu yao aliyepooza aponywe, walichofanya ni kuondoa sehemu ya paa la Sinagogi na kumshusha mgonjwa na kitanda chake kwa kamba. Yesu bila kupepesa alimwambia mgonjwa MWANANGU UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO.... Hii kauli ina maana kubwa sana kwenye ulimwengi wa Kiroho na pia ni maelekezo rasmi kwamba uponyaji pia ni matokeo ya kusamehewa dhambi. Na ukiangalia yule mgonjwa hakutubu wala kuongozwa na Yesu kukiri imani. Ambapo haina tofauti na yule mwanamke aliyeletwa kwa Yesu akituhumiwa Uzinzi. Hakupewa nafasi na washtaki wake kujutia makosa yake bali kwa sababu Roho wa Mungu uliwaconvict washtaki wake wakakimbia. Yesu alimwambia USITENDE DHAMBI TENA......

Haya mambo ya kujiaminisha kuwa mitume na manabii ndiyo walioshika funguo za kuelekea toba ni fundisho la mwovu shetani
 
Tupe mfano wa category ya pili
 
Tupe mfano wa category ya pili
Mkuu
Kama umeshindwa kuelewa description yake basi hata mfano hautasaidia kukuelewesha.... Na bahati mbaya hakuna mfano kwenye Maandiko unaoelezea binadamu aliyemkufuru Roho Mtakatifu baada ya Yesu Kupaa kwenda Mbinguni lakini kuna waasi wa kwanza katika Agano Jipya ambao haijasemwa kama walimkufuru Roho Mtakatifu lakini waliadhibiwa vikali sana na Mungu. Mkumbuke Anania na mkewe Safira


Kila kitu nimeweka humo kwa lugha nyepesi sana kueleweka.
 
In life what you believe is what you get,km kichwani mwako inasema huwezi mpk mchungaji ajue umezini that’s you kwakua mchungaji sio mungu ilaunapotubu unaongea na mungu wangu wako and read a correct mistari ya kutubu sidhani km hutasamehewa your mind is your driver
 
Ila nyie watumishi kausha damu ni shida Sana. Kumbe ndo mnadanga watu huko Ili mpate sadaka
. Tuwekee mafungu ya uliyoyandika hapa. Mimi nitakutumia sadaka laki 2. Unitumie no ya mpesa.
 
Kuna dhambi ambazo kwame Mungu awezi kuzisamehe ata ukitubuni pamoja na uchafu (ushoga,kumdhihaki nk )
 
Mkuu uko sahihi kabisa! Lakini hata hivyo Sadaka ya Ukombozi ni ile iliyopatikana pale Msalabani,yaani damu ya Yesu,si vinginevyo,
(Mathayo26:28)
Hakuna Sadaka nyingine inayoweza kumridhisha Mungu atusamehe zaidi ya hiyo iliyopatikana pale Msalabani,
(Waebrania10:6-10)
Chakuzingatia tu kwa kuwa Sadaka hiyo ilitolewa mara moja mara mtu anapaswa kutubu dhambi zake kwa KUMAANISHA KUZIACHA hata kama dhambi hiyo ni kubwa kiasi gani mf.Kuua,Kuzini,Kulawiti,kubaka,kunyanganya,nk atasamehewa tu,
(Isaya1:18) (Mithali28:13)
HATARI iliyopo ni pale mtu ambapo ametubu dhambi,harafu baada ya kujifunza Kweli ya Neno la Mungu kwa muda mrefu ikatokea AKAFANYA DHAMBI KWA KUKUSUDIA huku akijua ni dhambi mf.ni mtumishi wa Mungu,askofu,nk pale anamhuzunisha Roho Mtakatifu! Kusamehewa siyo rahisi hivi hivi,ni shughuli kweli kweli,(Waebrania10:26-29)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…