Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Yule mtu pembeni msalabani alikuwa muuaji na alitubu hadharani na sio sirini, na tunaona Yesu akamsamehe.

Niliyoandika inaitwa INJILI YA UTAKATIFU.

INJILI hiyo Si Rahisi kuisikia Kwa false prophets.

Ubarikiwe.
Ebu soma uniambie ametubu sehemu gani

Luka 23:40-43
[40]Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo?

[41]Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa.

[42]Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.

[43]Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.
 
Kwahio mtumishi wa Mungu anatakiwa kuijua dhambi unayoiungama? Halafu akakutangaze sio?
Swali zuri.

Mtumishi wa Mungu ,mwenye BUSARA za Mungu aliyejazwa Roho mtakatifu hawezi kukudhalilisha hadharani.

Kwenda na kumshirikisha mtumishi, ni kukusaidia kujinasia, dhambi hizo zinaambatana na vifungo na mikataba ya kiroho, mfungwa hawezi JINSIA pekeako.

Mungu akusaidie, pia ikusaidie kuepuka dhambi aina hizo, mfano UZINZI, huwezi tubu sirini, so ukijua Hilo, kimbia kabisa zinaa. Amen
 
dhambi hizo zote umetaja ni kubwa, ila sijakuelewa. kitu ambacho kimenistua ni pale uliposema mtu atafute mtumishi wa Mungu amwombee na aende na sadaka. sadaka ya nini sasa wakati sadaka/kafara ya dhambi Yesu alishaitoa pale msalabani? ina maana unapoenda na sadaka uanenda kununua nini in exchange? Dhambi inaondolewa kwa kumwagika damu sio kwa sadaka yako, awali dhambi iliondoka kwa kumwaga damu ya wanyama, Yesu akaja akamwaga damu mara moja tu ili wamwendeao kwa toba awaonye dhambi kwa Damu. alilipa deni lote ndio maana alisema imekwisha. yote alishamaliza pale kalvary, kinachotakiwa kwako ni kutubu toka moyoni kwa maana ya kuacha dhambi na Mungu akiona umetubu kwa kweli, anakusamehe dhambi hata ingekuwa nyekundu kama damu. nipeleke sadaka yangu kwa mchungaji ambaye pia yawezekana ana madhambi yake yanayohitaji kusamehewa na Yesu, yeye sadaka anapelekega wapi ili asamehewe dhambi? SADAKA YESU ALISHATOA, damu yake haikumwagika bure, na haikuacha deni hata moja.

kwa wale msioelewa, ukishaona mtu wa aina hii kimbia, ana mafundisho potofu. Dhambi zote isipokuwa dhambi moja tu ya kumkufuru Roho Mtakatifu, zinasameheka bila condition nyingine yeyote zaidi ya kafara la Damu ya Yesu. conditions zingine zikiwekwa ni za kibinadamu. Mungu huangalia moyo na mtu anayetubu kwa moyo wote kwa kumaanisha kuacha dhambi, naye husamehe, hasemehi kwasababu umeombewa na mtu mwingine usamehewe, pamoja na kwamba kuombewa nako sio mbaya ila sio condition kwamba lazima, hata ukiombewa Mungu bado anaangalia moyo wako kama umekuja na toba ya kweli.

Luka 18:10 - 14 “Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali: Mmoja Mfarisayo, na mwingine mtozaushuru. 11Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: ‘Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: Walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtozaushuru. 12Nafunga mara mbili kwa juma, natoa zaka sehemu ya kumi ya pato langu.’

13Lakini yule mtozaushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema: ‘Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi.’ 14Nawaambieni, huyu mtozaushuru alirudi nyumbani akiwa amesamehewa. Lakini yule mwingine, sivyo. Kwa maana kila anayejikweza atashushwa, na kila anayejishusha atakwezwa.”
hata kwenye maombi ya kawaida, Mungu huangalia moyo, hahitaji umlipe pesa ili akusamehe, anaangalia moyo.

Mathayo 6:6​

Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
 
Wewe ni mpotoshaji mkuu. Ebu jaribu kusoma maandiko vizuri.
Naomba kifungu hicho kinachosema unatakiwa kwenda kwa mtumishi wa Mungu ili kutubu
 
Nzuri sana hii mkuu, Mungu akubariki. Huyu jamaa anatakiwa afungiwe humu analeta upotoshaji
 
Hii ni mbinu za upigaji kwa wachungaji uchwara
Mada inawahusu WATAKATIFU.

Ikiwa haikuhusu, na hutaki Utakatifu, peleka sadaka Yako Kwa mganga wako ulikozoea.

Lakini nakuombea, uje uwe mwana wa Mungu, uungane na waenda Mbinguni.

Amen
 
Mwenye mamlaka ya mwisho ya kusamehe ni MUNGU na anaweza asiwepo mtu mwingine ila ukatubu kwa MUNGU ukasamehewa, yule mwizi wa msalabani nani alimwongoza sala ya toba? Kama sio Yesu, Paulo nani alimwongoza sala ya toba kama sio Yesu, Musa aliyekuwa muuaji na Mungu kumtokea kwenye kiti kinachowaka nani alimwongoza sala ya toba? Kama sio Mungu mwenyewe? Cha msingi Mungu huangalia moyo uliopondeka na kunyenyekea uliotayari kugeuka kwa toba usikiapo neno lake ISAYA 57:15
 
Si DHAMBI zote Hadi uende Kwa mtumishi, ni baadhi.

Mfano, huwezi kufirana, kuua au kuzini na mke wa Jirani Yako halafu ukatubu sirini, dhambi hizo hapo juu Zina mikataba na vifungo vya kipepo ambavyo lazima uhusishe Mtumishi.
weka msitari ya Biblia inayoonyesha jambo hilo, kwamba ukitaka kusamehewa baadhi ya dhambi shurti uende kwa mchungaji. acheni utapeli na kupotosha injili.
 
Wapi Yesu alikataza watu wasitoe sadaka?

Ujuaji wa nini ndugu?
 
Sala ya toba kwa mwizi umeiona wapi wewe
 
Si DHAMBI zote Hadi uende Kwa mtumishi, ni baadhi.

Mfano, huwezi kufirana, kuua au kuzini na mke wa Jirani Yako halafu ukatubu sirini, dhambi hizo hapo juu Zina mikataba na vifungo vya kipepo ambavyo lazima uhusishe Mtumishi.

Imeandikwa wapi wewe mwongo?
 
Mwizi alitubu hadharani,

Paulo pia alipotokewa na YESU ,alielekezwa amtafute mtumishi Ili amwelekeze Cha kufanya.

Pia sijaweka mpaka, yapo mazingira mfano, mtu Yu katika kufa, ajalini au anazama majini ajalini nk nk na hakuna mtumishi karibu, Mungu lazima atamsamehe.

Karibu 🙏
 
Wapi Yesu alikataza watu wasitoe sadaka?

Ujuaji wa nini ndugu?
unaniuliza mimi tena? Mimi nimesema kwenye Biblia hakuna sehemu hata moja inayoelekeza tutoe sadaka ili tusamehewe dhambi, au kwamba lazima twende tukaombewe na mwanadamu mwingine. wewe unakuja kuniuliza kwamba ni wapi? that means kama haipo kwenye Biblia hayo ni mafundisho ya kibinadamu tu ambayo wewe unajua mlikoyatoa, nje ya Biblia.

mnasimamia kwenye mstari gani? ndio swali.
 
Utakuwa akili huna kwenda kutubu dhambi kwa binadamu mwenzako.
 
Na Mchungaji dhambi zake za kula kondoo wa bwana anatubu kwa nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…