Salaam shalom.
INTRODUCTON.
Imeandikwa, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na haki, hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.( 1 Yoh 1:9).
Dhambi ni kutotii, kwenda kinyume na maelekezo ya Mungu. Na Roho mtakatifu yupo kutukumbusha dhambi zetu Ili tuzitibie Ili tuendelee kuwa WATAKATIFU.
DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:
1. ZINAA NA UASHERATI.
UASHERATI ni kufanya Tendo la zinaa na mtu nje ya NDOA asiye mkeo au mumeo.
UZINZI ni kufanya tendo la uchafu, zinaa kabla ya Kuoa au Kuolewa.
Ukizini na mke wa mtu au mume wa Mtu, usijidanganye kuwa ukitubu sirini utasamehewa, HATIA itaendelea kuwepo Hadi uwatafute watumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi. Watumishi Wana BUSARA ya kusuluhisha dhambi hiyo pande zote mbili Ili ufunguliwe.
2. USHOGA.
Ikiwa uliwahi kuwa shoga, ukaamua kuacha, kamwe usitubu sirini na kuishiwa hapo, USHOGA huambatana na mapepo na kufungwa NAFSI, mfungwa kamwe hawezi jifunguanpingu mwenyewe, unawahutaji watumishi wa Kweli Ili UOMBEWE na kuwekwa huru, sadaka ni LAZIMA Ili itolewe huko.
3. USAGAJI.
Mwanamke pia aliyewa kufanya dhambi hiyo, huwezi kufunguliwa na Utumwa na HATIA hiyo pekeako Kwa kutubu sirini, nenda Kwa watumishi wa Kweli, Ukiwa na sadaka ya Ukombozi.
4. PUNYETO/ KUJICHUA.
Ikiwa uliwahi kujichua, ukaamua kuacha, unahitaji kwenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi Ili ufunguliwe, Mpiga PUNYETO ni mfungwa, ni mke au mume wa Roho chafu katika Ulimwengu wa Roho, hivyo kufunguliwa ni LAZIMA utoe sadaka, uvunje NDOA chafu hiyo ya kiroho na hati ya NDOA chafu ya kiroho iondolewe, usipofanya hivyo, unajidanganya. Mbinguni huingii ng'o!!
Neno Hilo hapo juu ni ROHO. Amen.
5.MWANAMKE KUOA MWANAMKE/MWANAUME KUOA MWANAUME MWENZIE.
Kutubu dhambi hii sirini bila watumishi wa Mungu ni kujidanganya. Chukua sadaka, nenda Kwa mtumishi, Sema Kweli Ili UOMBEWE na kufunguliwa, NDOA haramu ivunjwe na ufungwa wako kiroho uondolewe. Amen.
6. ORAL SEX.
Ikiwa uliwahi kushiriki oral sex, kunyonya au kuramba Kwa mdomo sehemu za Siri za mwanamke au Mwanaume na ukatambua ni DHAMBI, ukaacha, Bado u kifungoni.
Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli wa Mungu ufunguliwe na Mungu.
7. ABORTION./ UTOAJI MIMBA/ KUFUNGA UZAZI/ KUTUMIA VIDONGE VYA KUPANGA UZAZI.
Kimbia haraka Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli ,beba sadaka kulingana na uwezo wako, UOMBEWE ufunguliwe.
Ukipuuza Utakataliwa GETI la Mbinguni.
9. IKIWA ULIWAHI TUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME/ KIKE.
Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.
10. MAUAJI.
Ikiwa uliwahi kuua bila kukusudia ,ukahukumiwa JELA ukatoka, ikiwa uliua Kwa Siri na hukubainika, ikiwa ulishiriki kuua, usijidanganye kuwa unaweza kutubu sirini, HATIA Ili ikuondoke uwe na Amani, Tafuta kiongozi wa Mungu wa Kweli mwenye BUSARA za Mungu, akuongoze Cha kufanya, utoe pia sadaka ya Ukombozi.
11. IBADA ZA SANAMU, KUSHIRIKI IBADA ZA WAFU NA KUTOA SADAKA KWA MIZIMU KIMILA NK NK.
Kushiriki Ibada za KIMILA na Kutoa sadaka Kwa Roho za kishetani za Mababu, ni DHAMBI pia, ni kufungwa ni Utumwa ambao huwezi kujifungua pekeako.
Ukiamua kuacha na kuokoka, hatua inayofuata ni kushirikisha watumishi kukusaidia kukutenga na madhabahu hizo.
Sadaka ni LAZIMA, sababu, Ulimwengu wa Nuru na Giza sadaka ni inevitable. Amen
HITIMISHO.
Dhambi nilizotaja hapo juu, ni baadhi tu ya dhambi ambazo huwezi tubu pekeako, zimetajwa sawasawa na Ruhusa ya Roho mtakatifu Kwa mtumishi wake sawasawa na ufunuo wake apendavyo.
NB: Si DHAMBI zote zinahitaji kuona mtumishi wa Kweli kukusaidia kufunguliwa pingu za dhambi, ni baadhi ya dhambi ambazo Zina vifungo na attachment na maagano ya kipepo na kishetani.
Mungu awabariki.
Source: Nabii Justine Ibrahim.
Amen.