Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Tuseme hivi..., Ukishatenda hizo dhambi mfano uzinzi ni kwamba umejiingiza kwenye maagano na huyo uliyezini nae, maana mmekuwa nae mwili mmoja......

....unapofanya toba unahitaji pia kutumia damu ya Yesu kuvunja huo muunganiko na huyo uliyezini nae...na maombi kama hayo ukiambatanisha sadaka ni vizuri sana maana sadaka hunena na kuwa ukumbusho mbele za Mungu kwamba ulilivunja lile agano la kipepo na sasa umejiunganisha na madhabahu ya Kristo.
 
Na kwa hakika wahusika wanaalikwa bila kusita wala kuona haya, kupata fursa hiyo muhimu ya upatanisho na Mungu, ili wapate msamaha wa madhambi yao na wakawe huru tena, baada ya kutumbukia dhambini na kuharibu uhusiano wao na Mungu.

Na sasa mtoa bandiko anakumbusha na anaelekeza namna ya kurejea na kurejesha uhusiano wa karibu zaidi tena na Mungu,
ni katika sifa na Utukufu wa jina lake..
Aimen....
 
Nilichoandika ndiyo Kweli yote.

Sadaka Si pesa pekee, moyo wako na utayari wako ni sadaka tosha ikiwa Hauna.

Imeandikwa, Usije nyumbani mwa BWANA mikono mitupu.


Neno ni Upanga ukatao kuwili.
 
Mtumishi nawe hujaelewa dhima ya thread.

Mganga wa kienyeji anaweza kujitoa katika kifungo Cha mikataba ya uganga bila msaada wa watumishi?

Si DHAMBI zote, Rudi soma UPYA utaelewa.

Tafadhali πŸ™πŸ™
shida inayowapata hawa wachungaji matapeli, ni kuchukua yale yanayofanyika kwenye uganga wa kienyeji kuyaleta kwenye wokovu. badala ya kuchukua maagizo ya Neno la Mungu na kuapply. hapa ndipo wanafeli sana. kuna wengine wanafundisha hadi aina za majini, na namna ya kuyatoa, na kazi zao. sasa, Yesu yu juu ya yote, akiingia ni kwamba Mfalme ameingia, nini anaweza akashindwa kufanya?
 
Sio kweli tumekombolewa na damu ya yesu nw unaweza kutubu peke yako na mambo yanakuwa safi kabisa
 
Haya ni mambo ya imani no one can prove this.
Ndiyo maana hata mjadala wake hauwezi kuwa na mwisho.
 
aisee huyu jamaa amelishwa matango pori hadi huruma. sadaka ipi inanena zaidi ya Damu ya Yesu Kristo? ukiweka Damu ya Yesu pamoja na sadaka yako hapohapo ukasogea mbele za Mungu, kipi kitanena na Mungu akakisikiliza? au akakumbuka? Damu ya Yesu ni kuu kuliko damu ya mafahari, kiuliko hata damu ya Habil, na Mungu huiangalia hiyo tu kama kafara, hukumbuka hiyo tu kama kafara, hakumbuki kitu kingine. tuwekee mstari wowote unaosapoti hayo mliyolishwa na manabii wenu
 
Ndicho nilichosema Mimi Kwa baadhi ya dhambi.

Watu wamechukua tofauti.

Ikiwa nawe sasa umeelewa, saidia kuwaelewesha walioelewa tofauti.

Sadaka ni Ishara ya moyo kushukuru,ikiwa huna Si lazima utoe,

Muhimu hapa, ni watumishi kusaidia njia sahihi za kumtoa mtu huyo kifungoni.
 
dhambi gani tena hali ya kuwa mulisamehewa
 
Usitoe sadaka kama huoni umuhimu wake.
 
Kwahiyo kesho tena unarud..na kesho kutwa unarud na siku nyingine hivyo hivyo??
 
Nilichoandika ndiyo Kweli yote.

Sadaka Si pesa pekee, moyo wako na utayari wako ni sadaka tosha ikiwa Hauna.

Imeandikwa, Usije nyumbani mwa BWANA mikono mitupu.


Neno ni Upanga ukatao kuwili.
Sidhani, baadhi ya mambo sikubaliani na wewe, ni vile tu una tafsiri tofauti.

Kama sadaka si lazima pesa bali hata kujitoa moyo wako, that means mpaka nimeamua kutubu ni nimeshajutia makosa yangu, sasa iweje ni lazma sadaka tena nisamehewe
 
dhambi gani tena hali ya kuwa mulisamehewa
Mtu aliyesamehewa anaweza kurudi dhambini Kwa uamuzi wake,

Inaitwa kurudi matopeni, dhambini,

BIBLIA imeandikwa, Wala SITA lifuta Jina lako katika kitabu Cha Uzima,

Kumbe uelewe kuwa, Jina Linaweza andikwa na kufutwa vilevile.

Kusamehewa dhambi, Si kudumu katika Dhambi, Bali kuzitubia.

Mbarikiwe.
 
Usitoe sadaka kama huoni umuhimu wake.
ninyi kama mnaona ni muhimu mnatoa kwa kusimamia mstari gani, yatupasa tuwasaidie, manake mjue tunaokolewa na kusamehewa kwa Neema tu wala si kwa matendo yetu wandugu, msije kujisifu na hizo sadaka zenu. mmepotea na ni dhihaka kwa Mungu. unapotoa sadaka unamdhihaki Mungu kwa kafara ya thamani sana ya Damu ya Yesu Kristo aliyoitoa pale msalabani, ni dhiaha na ni dhambi na ni kulilisha upepo hakuna chochote utapata.

Ebr 12:24 SUV​

na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
 

Eti kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume ni dhambi, nmejiuliza ikitokea mume kapata shida na hawezi kufanya tendo daktari amemwambia atumie viagra tayari dhambi.
 
Yeah!......Kuna dhambi ambazo muhusika mwenyekwe ni vigumu kuomba na kusikilizwa maana maagano aliyonayo hayaruhusu hayo, mfano uchawi/ushirikina, uuaji hapo lazima mtumishi amuongoze muhusika sala ya toba na kumtakasa kwa damu ya Kristo.
 
Sidhani, baadhi ya mambo sikubaliani na wewe, ni vile tu una tafsiri tofauti.

Kama sadaka si lazima pesa bali hata kujitoa moyo wako, that means mpaka nimeamua kutubu ni nimeshajutia makosa yangu, sasa iweje ni lazma sadaka tena nisamehewe
Sadaka ya pesa Si lazima, ila ni muhimu kushukuru Kwa mdomo au Kutoa, ni wewe utakavyoongozwa na Mungu .

Muhimu ni kujua kuwa, zipo dhambi huwezi malizana nazo binafsi sirini.

Amen
 
Mtumishi nawe hujaelewa dhima ya thread.

Mganga wa kienyeji anaweza kujitoa katika kifungo Cha mikataba ya uganga bila msaada wa watumishi?

Si DHAMBI zote, Rudi soma UPYA utaelewa.

Tafadhali πŸ™πŸ™
Huyu ni muumini mpya. Hapo sio tu mtumishi bali muumini yoyote amepewa jukumu la kuwatoa huko gizani na kuwaleta nuruni.

Kisha afundiahwe sala na namna ya kumtegemea Mungu peke yake na kutubu dhambi zake hukohuko. Ila kwa mara ya kwanza ataelekezwa na kuongozwa.

Tatizo lililonishanganya ni aina ya dhambi ulizozitaja zinafanywa na wakristo na watumishi wengi wakubwa kwa wadogo wa kisasa mfano zinaq ni dhambi yao pendwa. Kikubwa watu waelekezwe na wafundishwe namna ya kumalizana na Mungu wao wenyewe. Kutaka wamwendee mtumishi ni dini za kikuhani za agano la kale.

Nimekuelewa kwa mtu mpya sio mwenyeji.
 
Baada ya kumsaliti Yesu, petro alienda kutubu kwa mchungaji au kuhani yupi?

Baada ya kukaid maagizo ya Mungu nabii Musa pale mlimani alienda kutubu kwa nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…