Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

huyu jamaa anachanganya sana pia kuhusu kukutana na Mungu, kukutana na Mungu sio lazima ukutanishwe kwa kuwekewa mikono ya mtu mwingine, unakutana na Mungu moyoni. kuna watu wameingia chumbani kusali, Mungu akawashukia kwa kuangalia mioyo yao, na Mungu akishuka, huhitaji tena kwenda kuondolewa sijui laana sijui nini za ukoo kama anazosema, Mungu ameingia moyoni, hayo mataputapu yataendelea kukaa kwako yanatafuta nini sasa? manake ukiona bado yapo, haujakutana na Mungu, tafuta Mungu.

wengi wa waliotegemezi wa maombezi kama huyu anayetaka kutapeli watu hapa, siku zote huwa hawakutani na Mungu. ni wapenzi wa miujiza na wamefanya ukristo kuwa kama uganga wa kienyeji, na hakuna hata mstari mmoja wa Biblia wanasimamia kuwasapoti, ni mawazo ya kibadamu na chanzo chake ni shetani. imefika wakati watu hata kusoma Neno, kufunga kutafuta uso wa Mungu, kuabudu kwa kweli au kuomba ujazo wa Roho Mtakatifu hawahitaji, wanachotaka waende pale kwa nabii awatabirie wapate wanachopata, waondoke, maisha rahisi tu hivyo. hawajui kuwa shetani pia huwa anaweza kufanay miujiza, na ukiangalia miujiza yao yote haidumu kwasababu ni mazingaombwe tu ya shetani. mshindwe kwa Jina la Yesu.
 
Salaam shalom.

INTRODUCTON.

Imeandikwa, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na haki, hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.( 1 Yoh 1:9).

Dhambi ni kutotii, kwenda kinyume na maelekezo ya Mungu. Na Roho mtakatifu yupo kutukumbusha dhambi zetu Ili tuzitibie Ili tuendelee kuwa WATAKATIFU.

DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:


1. ZINAA NA UASHERATI.

UASHERATI ni kufanya Tendo la zinaa na mtu nje ya NDOA asiye mkeo au mumeo.

UZINZI ni kufanya tendo la uchafu, zinaa kabla ya Kuoa au Kuolewa.

Ukizini na mke wa mtu au mume wa Mtu, usijidanganye kuwa ukitubu sirini utasamehewa, HATIA itaendelea kuwepo Hadi uwatafute watumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi. Watumishi Wana BUSARA ya kusuluhisha dhambi hiyo pande zote mbili Ili ufunguliwe.

2. USHOGA.

Ikiwa uliwahi kuwa shoga, ukaamua kuacha, kamwe usitubu sirini na kuishiwa hapo, USHOGA huambatana na mapepo na kufungwa NAFSI, mfungwa kamwe hawezi jifunguanpingu mwenyewe, unawahutaji watumishi wa Kweli Ili UOMBEWE na kuwekwa huru, sadaka ni LAZIMA Ili itolewe huko.

3. USAGAJI.

Mwanamke pia aliyewa kufanya dhambi hiyo, huwezi kufunguliwa na Utumwa na HATIA hiyo pekeako Kwa kutubu sirini, nenda Kwa watumishi wa Kweli, Ukiwa na sadaka ya Ukombozi.

4. PUNYETO/ KUJICHUA.

Ikiwa uliwahi kujichua, ukaamua kuacha, unahitaji kwenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi Ili ufunguliwe, Mpiga PUNYETO ni mfungwa, ni mke au mume wa Roho chafu katika Ulimwengu wa Roho, hivyo kufunguliwa ni LAZIMA utoe sadaka, uvunje NDOA chafu hiyo ya kiroho na hati ya NDOA chafu ya kiroho iondolewe, usipofanya hivyo, unajidanganya. Mbinguni huingii ng'o!!
Neno Hilo hapo juu ni ROHO. Amen.

5.MWANAMKE KUOA MWANAMKE/MWANAUME KUOA MWANAUME MWENZIE.

Kutubu dhambi hii sirini bila watumishi wa Mungu ni kujidanganya. Chukua sadaka, nenda Kwa mtumishi, Sema Kweli Ili UOMBEWE na kufunguliwa, NDOA haramu ivunjwe na ufungwa wako kiroho uondolewe. Amen.

6. ORAL SEX.

Ikiwa uliwahi kushiriki oral sex, kunyonya au kuramba Kwa mdomo sehemu za Siri za mwanamke au Mwanaume na ukatambua ni DHAMBI, ukaacha, Bado u kifungoni.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli wa Mungu ufunguliwe na Mungu.

7. ABORTION./ UTOAJI MIMBA/ KUFUNGA UZAZI/ KUTUMIA VIDONGE VYA KUPANGA UZAZI.

Kimbia haraka Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli ,beba sadaka kulingana na uwezo wako, UOMBEWE ufunguliwe.

Ukipuuza Utakataliwa GETI la Mbinguni.

9. IKIWA ULIWAHI TUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME/ KIKE.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.

10. MAUAJI.

Ikiwa uliwahi kuua bila kukusudia ,ukahukumiwa JELA ukatoka, ikiwa uliua Kwa Siri na hukubainika, ikiwa ulishiriki kuua, usijidanganye kuwa unaweza kutubu sirini, HATIA Ili ikuondoke uwe na Amani, Tafuta kiongozi wa Mungu wa Kweli mwenye BUSARA za Mungu, akuongoze Cha kufanya, utoe pia sadaka ya Ukombozi.

11. IBADA ZA SANAMU, KUSHIRIKI IBADA ZA WAFU NA KUTOA SADAKA KWA MIZIMU KIMILA NK NK.

Kushiriki Ibada za KIMILA na Kutoa sadaka Kwa Roho za kishetani za Mababu, ni DHAMBI pia, ni kufungwa ni Utumwa ambao huwezi kujifungua pekeako.

Ukiamua kuacha na kuokoka, hatua inayofuata ni kushirikisha watumishi kukusaidia kukutenga na madhabahu hizo.

Sadaka ni LAZIMA, sababu, Ulimwengu wa Nuru na Giza sadaka ni inevitable. Amen

HITIMISHO.

Dhambi nilizotaja hapo juu, ni baadhi tu ya dhambi ambazo huwezi tubu pekeako, zimetajwa sawasawa na Ruhusa ya Roho mtakatifu Kwa mtumishi wake sawasawa na ufunuo wake apendavyo.

NB: Si DHAMBI zote zinahitaji kuona mtumishi wa Kweli kukusaidia kufunguliwa pingu za dhambi, ni baadhi ya dhambi ambazo Zina vifungo na attachment na maagano ya kipepo na kishetani.

Mungu awabariki.

Source: Nabii Justine Ibrahim.

Amen.
ukitembea na mke/mume wa m2 hautasamehewa ata ukiombewa na watumishi,,,sharti ni lazima atafutwe mume/mke wa uliyezini nae na uwaombe msamaha akikusamehe utasamehewa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
dini safi
sadaka ya ukombozi
madhabahu
mtumishi a.k.a mchungaji? why kwanini?
hata kale za wana wa israel walitumia madhabahu, sadaka ya ukombozi na dini safi,
sasa hata mimi naomba kueleweshwa ndugu? mtumishi atacheza kama nani au kazi yake halisi katika kutubu dhambi hizo ni ipi je atakua reporter au ni kazi zipi tafadhali naomba elimu hii inifae
 
Ikiwa Mungu alimtoa mwanawe wa pekee Yesu kristo awe sadaka ya kutukomboa,

Nani wewe usitoe sadaka. Sadaka ni Kwa ajili Yako, usidhani unamfaidisha Mchungaji.

Elia alilishwa na Mungu kupitia kunguru, usidhani watumishi wa Mungu wanategenea sadaka zako.

Na usijidanganye ukaenda Kutoa sadaka ya wizi, au ya kutapeli madhabahuni, utaondoka na LAANA.

Ubarikiwe.
Jinsi mlivyokuwa wa mchongo WIZI haujaorodhesha badala yake umeweka dawa za nguvu ya kiume na punyeto.
Wizi mmeshindwa kuuweka kwasababu watanzania wote ni wezi.
Mmechagua vile vitu ambavyo ni popular ili mzidi kuwatisha watu muendelee kutafuna sadaka.
 
unaniuliza mimi tena? Mimi nimesema kwenye Biblia hakuna sehemu hata moja inayoelekeza tutoe sadaka ili tusamehewe dhambi, au kwamba lazima twende tukaombewe na mwanadamu mwingine. wewe unakuja kuniuliza kwamba ni wapi? that means kama haipo kwenye Biblia hayo ni mafundisho ya kibinadamu tu ambayo wewe unajua mlikoyatoa, nje ya Biblia.

mnasimamia kwenye mstari gani? ndio swali.
Sadaka niliyoiongelea Si sadaka ya kufanyika mbadala Ili usamehewe dhambi, HAPANA.

Mtu anayejichua Kwa Mfano, awe kwenye NDOA au nje ya NDOA,

Ukijichua, katika Ulimwengu wa Roho umefunga NDOA kabisa katika Ulimwengu wa Roho.

Na ndoa hiyo, lazima Mahari imetolewa na mapepo, hivyo ajichuaye, ni mfungwa kamili.

Kuondoa hati ya NDOA ya NDOA ya kiroho, kuondoa sadaka hiyo na Mahari hiyo, lazima ukomboe na sadaka na Damu ya Yesu.

Unahitaji kufundishwa na Roho mtakatifu.

Pia maandiko yapo, nikikuletea maandiko utaamini?
 
Sala ya toba kwa mwizi umeiona wapi wewe
LUKA 23:42-43 mwizi anamwambia ee Yesu unikumbuke katika ufalme wako na YESU anajibu leo hii tutakuwa wote peponi. Toba kwa Yesu haina formula yeye ndie mwamuzi
 
Madalali mapato yamepungua mnaanza vitisho 😂 😂 😂
Ujumbe ni Kwa waliookoka. Ikiwa umesoma na kuamini, Sharti uokoke kwanza ndo utoe sadaka,

Sadaka za mbwa hazipokelewi madhabahuni,

Amen
 
Unachekesha sana
Huo ndo UKWELI.

Elia mtishibi alilishwa na Mungu kupitia kunguru.

TOBA itangulie sadaka, kamwe usitoe au usilete sadaka madhabahuni sadaka chafu, umeiba, umetapeli,hiyo unajidanganya.

Ni LAANA unajitafutia Kutoa sadaka itokanayo na wizi. Nk nk
 
HUMU NDANI KILA MTU NI LECTURER HAKUNA KILAZA NDIO MWANZO WA UPOTOFU KILA MTU NI MJUAJI
 
Haya maneno ya Yesu Kristo:
‭Mathayo ‭11:28‬-29

[28] Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

[29] Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;


**Dini imekuwa sehemu sehemu ya kumweka mwanadamu na Mungu.

Inataka control juu ya maisha ya mwanadamu badala ya Mungu kuwa kiongozi wa maisha ya mwanadamu.
 
LUKA 23:42-43 mwizi anamwambia ee Yesu unikumbuke katika ufalme wako na YESU anajibu leo hii tutakuwa wote peponi. Toba kwa Yesu haina formula yeye ndie mwamuzi
Asante mtumishi Kwa majibu murua.

Muuaji alitubu hadharani mchana kweupe,na akasamehewa.

Ubarikiwe.
 
Sadaka niliyoiongelea Si sadaka ya kufanyika mbadala Ili usamehewe dhambi, HAPANA.

Mtu anayejichua Kwa Mfano, awe kwenye NDOA au nje ya NDOA,

Ukijichua, katika Ulimwengu wa Roho umefunga NDOA kabisa katika Ulimwengu wa Roho.

Na ndoa hiyo, lazima Mahari imetolewa na mapepo, hivyo ajichuaye, ni mfungwa kamili.

Kuondoa hati ya NDOA ya NDOA ya kiroho, kuondoa sadaka hiyo na Mahari hiyo, lazima ukomboe na sadaka na Damu ya Yesu.

Unahitaji kufundishwa na Roho mtakatifu.

Pia maandiko yapo, nikikuletea maandiko utaamini?
Weka andiko ya haya unayosema tofauti na hapo hizi ni porojo na upotoshaji.
 
Jinsi mlivyokuwa wa mchongo WIZI haujaorodhesha badala yake umeweka dawa za nguvu ya kiume na punyeto.
Wizi mmeshindwa kuuweka kwasababu watanzania wote ni wezi.
Mmechagua vile vitu ambavyo ni popular ili mzidi kuwatisha watu muendelee kutafuna sadaka.
Sadaka itokanayo na wizi haipokelewi madhabahuni.

Ukitoa sadaka ya aina hiyo unajidanganya.

Kahaba, ukilipwa malipo ya ukahaba, ukachukua sadaka ukatoa madhabahuni, haipokelewi na Mungu.

Sadaka za aina hizo zimepelekea wengi kufa kabla ya wakati wao.

Kamwe, usitoe sadaka ya mbwa madhabahuni, UTALAANIWA Badala ya kubarikiwa.

Amen
 
Sadaka niliyoiongelea Si sadaka ya kufanyika mbadala Ili usamehewe dhambi, HAPANA.

Mtu anayejichua Kwa Mfano, awe kwenye NDOA au nje ya NDOA,

Ukijichua, katika Ulimwengu wa Roho umefunga NDOA kabisa katika Ulimwengu wa Roho.

Na ndoa hiyo, lazima Mahari imetolewa na mapepo, hivyo ajichuaye, ni mfungwa kamili.

Kuondoa hati ya NDOA ya NDOA ya kiroho, kuondoa sadaka hiyo na Mahari hiyo, lazima ukomboe na sadaka na Damu ya Yesu.

Unahitaji kufundishwa na Roho mtakatifu.

Pia maandiko yapo, nikikuletea maandiko utaamini?
hayo mafundisho mnayatoa kwenye mstari gani wa Biblia? ukiona huna mstari jua ni mafundisho ya kuzimu, na mnayafurahia. sikia;
1. mfano wako wa mtu kujichua, anayezini, shoga, mwizi, au dhambi yeyote ile, unapoifanya unakuwa umefungua mlango wa mashetani kuingia kwako, na yanakufanya mfungwa; sawa. kuondoa hati ya ndoa ya kiroho au kifungo chochote hakuhitaji jitihada ya mali zetu/sadaka au chochote, ni kuomba Neema ya Yesu Kristo kwa njia ya kafara la Damu yake afute hati hizo za ndoa, avunje vifungo hivyo vyote, akuweke huru. kwani nini maana ya "njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha?", mzigo wowote wa dhambi Yesu hakushindwa kulipa garama. unachohitaji ni kumwendea Mungu kwa kusikitika toka moyoni kwamba umetenda dhambi na unahitaji neema yake akusamehe na kukuondoa kwenye vifungo hivyo kwa Yesu Kristo, nawe unasamehewa.

najua shida yako, umepokea mafundisho ya manabii wa uongo ukayameza kama yalivyo, na ni ngumu sana kwako kufunguka, hadi Mungu mwenyewe akufungue. nakuomba leta maandiko uliyonayo ili tukufafanulie, manake hapa unapotosha watu na unamkosea Mungu.
 
Back
Top Bottom