Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

hakuna aliyebisha kuombewa, tunachobisha hapa ni sadaka. hata mimi nilipookoka nilitubu kwa kuombewa, na ninawaombea watu kwa kuwawekea mikono wanapotubu waokoke au kuomba pamoja nao rehema kwa Mungu. lakini hawatakiwi kuja na sadaka. hoja hapa Ni SADAKA. sadaka sadaka.
Tumeshakubaliana kwamba damu ya Yesu pekee ndio itakayokuondolea dhambi na sio sadaka yako.
 
Mbona sasa hajanukuu mistari ya biblia walau kwa kila dhambi ili kuback up mafundisho yake?

2 Mambo ya Nyakati 7
14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
 
DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.

kwa kifupi, nimejaribu kusoma andiko lako, hayo maneno mekundu hapo juu ndio yameharibu kila kitu. na huo ndio msingi wa mafundisho ya kishetani. tunasamehewa dhambi bure, Yesu alilipa deni la dhambi bure, msitoze watu ili wasamehewe dhambi, ni wizi kama wizi mwingine tu, Yesu angekuwa anatoza watu pesa hivyo wengine tusingeokoka manake hatukuwa na pesa.
Sadaka ni AMRI.
 
Yaani uzini na mke wa Jirani Yako sirini halafu utubu sirini?

Mwombee Mungu Roho mtakatifu akufunulie aloyasema mwenyewe kabla ya kupinga.
Hakuna kitu kama hicho mzee acha kukaririshwa ujinga na wasaka tonge, huyo sijui mchungaji sijui nabii mwenyewe unaye amini atakutubisha anakula mkeo sirini,

mambo ya imani ni magumu sana ila jua tuu kwamba mungu anafanya kazi na kila nafsi individually hakuna nafsi inayo weza iombea msamaha nafsi nyingine na ndio maana kila mtu atahukumiwa kwa makosa nandhambi zake mwenyewe.
 
Ikiwa Mungu alimtoa mwanawe wa pekee Yesu kristo awe sadaka ya kutukomboa,

Nani wewe usitoe sadaka. Sadaka ni Kwa ajili Yako, usidhani unamfaidisha Mchungaji.

Elia alilishwa na Mungu kupitia kunguru, usidhani watumishi wa Mungu wanategenea sadaka zako.

Na usijidanganye ukaenda Kutoa sadaka ya wizi, au ya kutapeli madhabahuni, utaondoka na LAANA.

Ubarikiwe.
Yaani fedha unampa mchugaji harafu unasema humfaidishi
 
Tumeshakubaliana kwamba damu ya Yesu pekee ndio itakayokuondolea dhambi na sio sadaka yako.
hicho ndio msimamo wangu tangu awali. ila wenzako wanasema uende na sadaka unapoenda kutubu. angalia alichoandika huyu mwenzio, nimekata baadhi ya maneno; ni sadaka ya ukombozi ipi na upi anaongelea huyu jamaa hapa? sadaka ya ukombozi ilishatolewa na Yesu, tunasamehewa bure.

DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.
 
Mbona sasa hajanukuu mistari ya biblia walau kwa kila dhambi ili kuback up mafundisho yake?

2 Mambo ya Nyakati 7
14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
(1 Wakorintho 6:9-10)
Au hamjui ya kuwa, wadhalimu, hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike, waasherati, hawataurithi ufalme wa Mungu,

Wala WAABUDU SANAMU, Wala wazinzi, Wala wafirahi, Wala WALAWITI,Wala wevi, Wala watamanio, Wala WALEVI, Wala watukanaji, Wala wanyanganyi.

(Ufunuo 21:8)

Bali waoga, na wasioamini,na wachukizao, na wauwaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote,sehemu Yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo MAUTI ya pili.
 
hahahaha, nadhani unahitaji kwa kila dhambi uweke mstari kwamba utatubu na kusamehewa kama utatubu kwa mtumishi tena ukiwa na sadaka.

hiyo mistari kama ilivyo ni ya jumla, kwamba usipotubia dhambi hizo ulizoorodhesha (bila kuweka condition kwamba ukatubu wapi) hautaurithi ufalme wa Mungu. Mungu akusaidie, najua kuna siku utaelewa, na kama utajifanay shingo ngumu utalazimishwa kuelewa. hata sisi tulikuwa kama wewe.
 
hicho ndio msimamo wangu tangu awali. ila wenzako wanasema uende na sadaka unapoenda kutubu. angalia alichoandika huyu mwenzio, nimekata baadhi ya maneno; ni sadaka ya ukombozi ipi na upi anaongelea huyu jamaa hapa? sadaka ya ukombozi ilishatolewa na Yesu, tunasamehewa bure.

DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.
Hayo ni maelekezo ya Mungu.

Sitaongeza Wala kupunguza. Ikiwa huamini, Ingia maombini uliza.

Hakuna popote nimesema lazima ubebe sadaka ikiwa huna.

Sadaka ni amri, Si Kwa ajili ya kununua msamaha.

Sadaka ni hiari na ni shukurani .

Ukombozi unahusika Kwa kutumia Damu ya Yesu, na kuvunja NDOA za kipepo na mikataba ya kipepo Kwa dhambi husika hapo juu.

Sadaka inatumika kureplace Mahari mapepo yalitoka Kwa mfungwa Ili kuzini naye Rohoni.

Amen
 
hahahaha, nadhani unahitaji kwa kila dhambi uweke mstari kwamba utatubu na kusamehewa kama utatubu kwa mtumishi tena ukiwa na sadaka.

hiyo mistari kama ilivyo ni ya jumla, kwamba usipotubia dhambi hizo ulizoorodhesha (bila kuweka condition kwamba ukatubu wapi) hautaurithi ufalme wa Mungu. Mungu akusaidie, najua kuna siku utaelewa, na kama utajifanay shingo ngumu utalazimishwa kuelewa. hata sisi tulikuwa kama wewe.
Aliyefundisha ni somo Hilo ni ROHO MTAKATIFU,

Sihitaji kufundishwa na wewe, nimeweka alichosemea Yeye na sijaongeza uongo mimi.

Wewe unaongea Kweli ya BIBLIA Kwa kupindua nilichoeleza katika thread.
 
Hayo ni maelekezo ya Mungu.

Sitaongeza Wala kupunguza. Ikiwa huamini, Ingia maombini uliza.

Hakuna popote nimesema lazima ubebe sadaka ikiwa huna.

Sadaka ni amri, Si Kwa ajili ya kununua msamaha.

Sadaka ni hiari na ni shukurani .

Ukombozi unahusika Kwa kutumia Damu ya Yesu, na kuvunja NDOA za kipepo na mikataba ya kipepo Kwa dhambi husika hapo juu.

Sadaka inatumika kureplace Mahari mapepo yalitoka Kwa mfungwa Ili kuzini naye Rohoni.

Amen
acha kujifurahisha dogo, maelekezo ya Mungu toka mstari gani kwenye Biblia? utaje mstari unaotoa maelekezo kwamba " DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa
". au ni maelekezo ya Mungu kwenye ndoto au maono, maelekezo yako yameegemea wapi, hebu tueleze. ni kipi hicho alichosema Mungu ambacho huwezi kuongeza wala kupunguza,hahahahaha, unachekesha kweli kweli.
 
Kuhusu sadaka ya ukombozi
Mafundisho ya kipepo pekee ndiyo yatataja sadaka ya ukombozi.
Hakuna kinachoweza kumkomboa mwanadamu kutoka katika hatari ya jehanamu au mateso yoyote ya kiroho zaidi ya DAMU na JINA LA YESU.
Kama mwanadamu angekuwa na namna yoyote ya kujikomboa zaidi ya jina na damu ya Yesu basi Kristo asingekuja duniani.
Ni heri hilo jambo la kuwashirikisha watumishi wakuombee toba na kukufungua kutoka katika dhambi ila hilo la sadaka ya ukombozi ni mafunzo ya kipepo
 
(Acts 9:3-6)
MATENDO 9:3 - 6 INASEMA:

Wakati alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafla nuru kutoka mbinguni ikamwangaza kotekote. 4Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona wanitesa? 5 Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayemtesa. 6Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. 7Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, waliisikia sauti, lakini hawakuona mtu. 8Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. 9Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.

HAYA WEWE SASA TUAMBIE WAPI HAPO SAULI/PAULO ALITUBU KWA KUPELEKA SADAKA KWA MCHUNGAJI, manake tunachopishana na wewe hapa ni kwanini ubebe sadaka wakati unaenda kutubu, huoni kama umepigwa sana na hao manabii?

wewe ndio wale wanaokotaka kimstari kimoja afu wanaenda kufungua hadi kanisa, wanajiita wachungaji kufundisha watu mapotofu kama hayo.
 
acha kujifurahisha dogo, maelekezo ya Mungu toka mstari gani kwenye Biblia? utaje mstari unaotoa maelekezo kwamba " DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa
". au ni maelekezo ya Mungu kwenye ndoto au maono, maelekezo yako yameegemea wapi, hebu tueleze. ni kipi hicho alichosema Mungu ambacho huwezi kuongeza wala kupunguza,hahahahaha, unachekesha kweli kweli.
Ni hayo tu Kwa Leo.

Ubarikiwe.
 
Ni hayo tu Kwa Leo.

Ubarikiwe.
wewe umechanganyikiwa au umepagawa na pepo la upotoshaji, shetani hutumia wanadamu kupotosha yaliyo ya Mungu, hata dini za ajabuajabu zilianza na watu wasiojua Neno la Mungu kama wewe na shetani anawapenda sana watu kama wewe. Mungu akusaidie, upo too vulnerable na umepotea mbali mno.
 
Message sent!!

Ubarikiwe, Mungu akipenda atakuokoa Kwa muda wake,

Muhimu umesoma message, KAZI ya muhubiri ni kuhubiri basi.

Amen
wewe hujaokoka, kaokoke upya kabisa na unatakiwa ukae mikononi mwa mtumishi anayejua Neno la Mungu akufundishe manake unaeneza mapotofu matupu na hapo ulipo wala hufanyi kazi yeyote ya Mungu, uhaiharibu.
 
Salaam shalom.

INTRODUCTON.

Imeandikwa, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na haki, hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.( 1 Yoh 1:9).

Dhambi ni kutotii, kwenda kinyume na maelekezo ya Mungu. Na Roho mtakatifu yupo kutukumbusha dhambi zetu Ili tuzitibie Ili tuendelee kuwa WATAKATIFU.

DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

1. ZINAA NA UASHERATI.

UASHERATI ni kufanya Tendo la zinaa na mtu nje ya NDOA asiye mkeo au mumeo.

UZINZI ni kufanya tendo la uchafu, zinaa kabla ya Kuoa au Kuolewa.

Ukizini na mke wa mtu au mume wa Mtu, usijidanganye kuwa ukitubu sirini utasamehewa, HATIA itaendelea kuwepo Hadi uwatafute watumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi. Watumishi Wana BUSARA ya kusuluhisha dhambi hiyo pande zote mbili Ili ufunguliwe.

2. USHOGA.

Ikiwa uliwahi kuwa shoga, ukaamua kuacha, kamwe usitubu sirini na kuishiwa hapo, USHOGA huambatana na mapepo na kufungwa NAFSI, mfungwa kamwe hawezi jifunguanpingu mwenyewe, unawahutaji watumishi wa Kweli Ili UOMBEWE na kuwekwa huru, sadaka ni LAZIMA Ili itolewe huko.

3. USAGAJI.

Mwanamke pia aliyewa kufanya dhambi hiyo, huwezi kufunguliwa na Utumwa na HATIA hiyo pekeako Kwa kutubu sirini, nenda Kwa watumishi wa Kweli, Ukiwa na sadaka ya Ukombozi.

4. PUNYETO/ KUJICHUA.

Ikiwa uliwahi kujichua, ukaamua kuacha, unahitaji kwenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi Ili ufunguliwe, Mpiga PUNYETO ni mfungwa, ni mke au mume wa Roho chafu katika Ulimwengu wa Roho, hivyo kufunguliwa ni LAZIMA utoe sadaka, uvunje NDOA chafu hiyo ya kiroho na hati ya NDOA chafu ya kiroho iondolewe, usipofanya hivyo, unajidanganya. Mbinguni huingii ng'o!!
Neno Hilo hapo juu ni ROHO. Amen.

5.MWANAMKE KUOA MWANAMKE/MWANAUME KUOA MWANAUME MWENZIE.

Kutubu dhambi hii sirini bila watumishi wa Mungu ni kujidanganya. Chukua sadaka, nenda Kwa mtumishi, Sema Kweli Ili UOMBEWE na kufunguliwa, NDOA haramu ivunjwe na ufungwa wako kiroho uondolewe. Amen.

6. ORAL SEX.

Ikiwa uliwahi kushiriki oral sex, kunyonya au kuramba Kwa mdomo sehemu za Siri za mwanamke au Mwanaume na ukatambua ni DHAMBI, ukaacha, Bado u kifungoni.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli wa Mungu ufunguliwe na Mungu.

7. ABORTION./ UTOAJI MIMBA/ KUFUNGA UZAZI/ KUTUMIA VIDONGE VYA KUPANGA UZAZI.

Kimbia haraka Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli ,beba sadaka kulingana na uwezo wako, UOMBEWE ufunguliwe.

Ukipuuza Utakataliwa GETI la Mbinguni.

9. IKIWA ULIWAHI TUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME/ KIKE.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.

10. MAUAJI.

Ikiwa uliwahi kuua bila kukusudia ,ukahukumiwa JELA ukatoka, ikiwa uliua Kwa Siri na hukubainika, ikiwa ulishiriki kuua, usijidanganye kuwa unaweza kutubu sirini, HATIA Ili ikuondoke uwe na Amani, Tafuta kiongozi wa Mungu wa Kweli mwenye BUSARA za Mungu, akuongoze Cha kufanya, utoe pia sadaka ya Ukombozi.

11. IBADA ZA SANAMU, KUSHIRIKI IBADA ZA WAFU NA KUTOA SADAKA KWA MIZIMU KIMILA NK NK.

Kushiriki Ibada za KIMILA na Kutoa sadaka Kwa Roho za kishetani za Mababu, ni DHAMBI pia, ni kufungwa ni Utumwa ambao huwezi kujifungua pekeako.

Ukiamua kuacha na kuokoka, hatua inayofuata ni kushirikisha watumishi kukusaidia kukutenga na madhabahu hizo.

Sadaka ni LAZIMA, sababu, Ulimwengu wa Nuru na Giza sadaka ni inevitable. Amen

HITIMISHO.

Dhambi nilizotaja hapo juu, ni baadhi tu ya dhambi ambazo huwezi tubu pekeako, zimetajwa sawasawa na Ruhusa ya Roho mtakatifu Kwa mtumishi wake sawasawa na ufunuo wake apendavyo.

NB: Si DHAMBI zote zinahitaji kuona mtumishi wa Kweli kukusaidia kufunguliwa pingu za dhambi, ni baadhi ya dhambi ambazo Zina vifungo na attachment na maagano ya kipepo na kishetani.

Mungu awabariki.

Source: Nabii Justine Ibrahim.

Amen.
Chukua sadaka kamuone mtumish akuombee.
Kwamba ww huna mdomo w kuomba
 
Back
Top Bottom