Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

1. Watumishi wa Mungu.
-Mungu asiyekuwepo,unaaminishwa uwepo waki
2. Sadaka: umpe nani? Hayo majizi? Huo ni ushuru wa wizi.
Yaani,umtafute mtu kama wewe,eti utubu. Akusaidie nini? Wake za watu wenyewe wamaishia huko na wanagegedwa na hao hao. Huwezi tunza siri zako,af unampelekea mtu eti akutunzie. Huo ni wehu tena kupita maelezo.
Uliwahi kusikia mikesha ya wasabato kwamba wakifanya yao wakiwa huko wanasafishana? Ndo kama hivyo. Hatudanganyiki. Siku hizi hela ngumu. Msitegemee mtaendelea kulishwa na mnaowadanganya. Ukweli wameshaujua
 
Wewe ndiye unapotosha. Kubeba sadaka ni kutimiza tu agizo kuwa,

Tusiende nyumbani mwa BWANA mikono mitupu,

Yesu Kristo, alimwona mjane maskini akitoa chote kidogo alicho nacho, hakumkataza.

Kutoa Si kumnunua Mungu au kununua Muujiza, ni shukrani. Na kuweka ulinzi juu ya kipato chako Ili mwovu asikiharibu.

Muhimu uelewe, zipo dhambi kamwe huwezi tubu gizani bila kushare na mtumishi wa Mungu wa Kweli.

Amen
kwahiyo dhambi zetu tunaenda kutubu madhabahuni tu, kama nikiamua kukubaliana na hoja yako nikaenda nyumbani kwa mchungaji nimweleze dhambi ashiriki pamoja nami kuomba rehema kwa Mungu, napo nibebe sadaka? wagonjwa mahospitalini ambao hawawezi hata kusimama nao wanatakiwa wabebwe mzobamzoma hadi kanisani wakatubishwe ili watoe sadaka? atawadanganya hadi lini huyu mtu?
 
bora wewe umefunguka. hili ni fundisho la mwalimu wao, pamoja na lile la ukombozi wa mzaliwa wa kwanza. alishaambiwa aokoke kitambo sana ila yeye ameng'ang'ania lutheran kwasababu ya sadaka, ndio anafundisha watu mambo ya aina hii.
Jamaa mafundisho yake yote atazunguka mwisho analenga sadaka.
Alivyo mjanja jamaa anateka wakristo wa madhehebu yote.
Yaani Kristo afe msalabani lakini anakuja mtu anatamka upumbavu wa sadaka ya kukomboa ardhi, sadaka ya kujenga madhabahu, sadaka ya kumkomboa mzaliwa wa kwanza, sadaka ya malango, sadaka ya kukomboa uzao n.k
Haihitajiki mtu aende chuo cha biblia kujua kuwa yale ni mafunzo yenye uvuvio wa kipepo
 
Narudia tena: Mafunzo yoyote yanayotaja sadaka ya ukombozi ni mafunzo ya kipepo, yanatoka kuzimu.
Mwakasege kwa makusudi au kwa kutokujua anatumiwa na Ibilisi kueneza mafunzo ya sadaka ya ukombozi.
Kama mwanadamu angekuwa na namna yoyote ya kujikomboa kwa sadaka basi Yesu asingekuja duniani.
Jina na damu ya Yesu vinatosha.
Vinatosha.
Kama nimekuelewa hivi.
 
Kwa maana hiyo unamaanisha aliyezini na mume au mke wa jirani yake, aende kwa huyo mlengwa amuambie. Nimezini na mumeo au mkeo? au kipi unamaanisha mkuu?
Nimeandika aende Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli, BUSARA za madhabahuni zitatumika kupata ufumbuzi wa DHAMBI husika Kwa pande zote.

Sijui umeelewa mtumishi?

Kwenda direct kutubu Kwa uliyemcgukulia mke Si BUSARA hiyo. Yaeza zaa kitu kingine kabisa.

Ubarikiwe.
 
Wewe ndiye unapotosha. Kubeba sadaka ni kutimiza tu agizo kuwa,

Tusiende nyumbani mwa BWANA mikono mitupu,

Yesu Kristo, alimwona mjane maskini akitoa chote kidogo alicho nacho, hakumkataza.

Kutoa Si kumnunua Mungu au kununua Muujiza, ni shukrani. Na kuweka ulinzi juu ya kipato chako Ili mwovu asikiharibu.

Muhimu uelewe, zipo dhambi kamwe huwezi tubu gizani bila kushare na mtumishi wa Mungu wa Kweli.

Amen
Shida ni hiyo sadaka ya ukombozi mkuu

Sina tabu na sadaka na huwa nafundisha umuhimu sadaka na andiko linasema usiingie nyumbani mwa Bwana mikono mitupu

Huwezi kutenganisha ibada na sadaka

Ila linapokuja swala la sadaka ya ukombozi Wa dhambi hilo alilimaliza Mungu pale msalabani kupitia mwana wake wapekee Yesu Kristo

Sisi tunachotakiwa ni kuamini na kupokea msamaha tu sasa ukitaka kujilipisha Kwa kudhani kazi ya msalaba haitoshi huo niupumbavu wako binafs
 
Kama nimekuelewa hivi.
Ibilisi ana hila nyingi sana.
Watu wanaoaminiwa ndio vyombo vya Ibilisi kueneza ushetani wake.
Yesu kaja kafa kamaliza kila kitu, sasa hizi sadaka za kukomboa ardhi, uzao, na malango zinatoka wapi kama si kwa baba wa uongo ibilisi?
 
Wewe jamaa mimi sikielewi hata unachoongea.

Kwani Biblia si ndiyo mwongozo wa wakristo.

Ni wapi kumeandikwa romamce na mmeo au mkeo ni dhambi.
Nimeandika Oral Sex Si Romance.

Usijifiche chini ya kivuli Cha mchicha.

Imeandikwa, afichaye dhambi hatafanikiwa, Bali atubuye na kuacha, atabarikiwa.
 
Jamaa mafundisho yake yote atazunguka mwisho analenga sadaka.
Alivyo mjanja jamaa anateka wakristo wa madhehebu yote.
Yaani Kristo afe msalabani lakini anakuja mtu anatamka upumbavu wa sadaka ya kukomboa ardhi, sadaka ya kujenga madhabahu, sadaka ya kumkomboa mzaliwa wa kwanza, sadaka ya malango, sadaka ya kukomboa uzao n.k
Haihitajiki mtu aende chuo cha biblia kujua kuwa yale ni mafunzo yenye uvuvio wa kipepo
mimi nilishamwuliza, hasa hapo kwenye mzaliwa wa kwanza, kuna familia naijua,walizaa mtoto wa kwanza akafa, wa pili akafa, wanne huko ndio kwao kama mtoto wa kwanza, akaongeza na mdogo wake. kwahiyo hao hawana lango tena la baraka, manake yeye kang'ang'ania kuwa mtoto wa kwanza ni lango, huwa anasoma vitabu vya wanijeria huko na wengine, anajifungia hata miezi 2 anasomaa anaanda notes, anaitisha semina anapiga pes andefuu imekwisha hiyo. hapo watu wanatoka ati mwalimu mwalimu anafundisha kumbe mwenzao kakopi hata yaliyo mapotofu. hata hii sadaka ya ukombozi wa nini sijui, kwani Yesu alifanya nini pale msalabani? na ametuachia Jina lake kwamba kwa Jina lake mashetani yatutuii.

tumepewa Mamlaka ya kukanyaka nyoka na ng'e na nguvu zote za yule adui shetani wala hakuna kitakachotudhuru (kama tutakuwa ndani yake), Jina la Yesu ndio jina pekee tulilopewa sisi wanadamu litupasalo kuokolewa kwako, kwa Jina la Yesu kila goti litapigwa, la vitu vilivyoko mbinguni, vilivyoko duniani na chini ya nchi. sasa kama nina silaha maridadi kama hii inayotoka tu kwenye kinywa changu, sadaka ni ya nini sasa? hawaoni kuwa unapobeba sadaka unapoenda kutubu ni dhihaka kwa Mungu? unadhihaki kazi ya msalaba? tutamtolea nini sisi Mungu chenye thamani kuzidi kazi ya msalaba? pesa kiasi gani, kitu gani kitazidi ile garama Yesu alitoa msalabani? Mungu awasaidie sana wafunguke.
 
Ibilisi ana hila nyingi sana.
Watu wanaoaminiwa ndio vyombo vya Ibilisi kueneza ushetani wake.
Yesu kaja kafa kamaliza kila kitu, sasa hizi sadaka za kukomboa ardhi, uzao, na malango zinatoka wapi kama si kwa baba wa uongo ibilisi?
Yesu hakukataza watu Kutoa sadaka.

Halafu mada inaongelea kitu kingine, ninyi mmeshikilia sadaka pekee,

KAZI IPO!!
 
Yesu hakukataza watu Kutoa sadaka.

Halafu mada inaongelea kitu kingine, ninyi mmeshikilia sadaka pekee,

KAZI IPO!!
kwani sisi tunapinga watu kutoa sadaka? au kwenda na sadaka ya ukombozi kwa mtumishi akuombee unapotubu? sisi tunasema sadaka unatakiwa kutoa, ila sio wakati wa kutubu, kwasababu huwezi kununua msamaha.

umeandika hivi, au umesahau, nikuwekee tena hapa chini ulisema:

DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.

Kwa mfano mke au mume aliyezini naye yupo nchi za mbali au hata nchi moja lakini mbali inakuwaje? anyway to cut the story short, ukisema kwa pande zote mbili unamaanisha nini mkuu?
Ndugu,

Elewa jambo hili, ikiwa umezini na mke wa mtu, mumewe awe karibu au mbali, usiamze kwenda Kwa mume wa uliyezini naye tuomba msamaha,waeza poteza KICHWA chako na uhai.

Nenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli mwenye kifua, mshirikisha, atakupa njia za kulimaliza Hilo Kwa pande zote husika.

Upande wa Mungu, upande wa Muibiwa mke na upande wenu wazinifu.

Umeelewa mtumishi?
 
Yesu hakukataza watu Kutoa sadaka.

Halafu mada inaongelea kitu kingine, ninyi mmeshikilia sadaka pekee,

KAZI IPO!!
Wewe hujaandika kwenye bandiko lako sadaka ya ukombozi ? Tunapiga kwenye hila kwingine hakuna tabu

Yaani hapo ndio adui kakaa ili kushusha thamani ya kazi ya msalaba

Tunafuta ujinga kwanza wengi wasipotezwe

Kula hiii afu tuendelee na swala la umuhimu wakushirikisha watumishi Wa Mungu hasa kwenye dhambi ainishwa
Au dhambi zinazokuzinga Kwa wepesi.

1 Petro 1:18 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
1 Petro 1:19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
 
kwani sisi tunapinga watu kutoa sadaka? au kwenda na sadaka ya ukombozi kwa mtumishi akuombee unapotubu? sisi tunasema sadaka unatakiwa kutoa, ila sio wakati wa kutubu, kwasababu huwezi kununua msamaha.

umeandika hivi, au umesahau, nikuwekee tena hapa chini ulisema:

DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.

Nimekwambia sitakujibu, usilazimishe.
 
Ndugu,

Elewa jambo hili, ikiwa umezini na mke wa mtu, mumewe awe karibu au mbali, usiamze kwenda Kwa mume wa uliyezini naye tuomba msamaha,waeza poteza KICHWA chako na uhai.

Nenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli mwenye kifua, mshirikisha, atakupa njia za kulimaliza Hilo Kwa pande zote husika.

Upande wa Mungu, upande wa Muibiwa mke na upande wenu wazinifu.

Umeelewa mtumishi?
kwahiyo kuna dhambi zingine unasamehewa kawaida, na zingine unasamehewa kwa masharti? hahahaha huyu mwalimu wako aisee amekupotosha mno.
 
Salaam shalom.

INTRODUCTON.

Imeandikwa, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na haki, hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.( 1 Yoh 1:9).

Dhambi ni kutotii, kwenda kinyume na maelekezo ya Mungu. Na Roho mtakatifu yupo kutukumbusha dhambi zetu Ili tuzitibie Ili tuendelee kuwa WATAKATIFU.

DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

1. ZINAA NA UASHERATI.

UASHERATI ni kufanya Tendo la zinaa na mtu nje ya NDOA asiye mkeo au mumeo.

UZINZI ni kufanya tendo la uchafu, zinaa kabla ya Kuoa au Kuolewa.

Ukizini na mke wa mtu au mume wa Mtu, usijidanganye kuwa ukitubu sirini utasamehewa, HATIA itaendelea kuwepo Hadi uwatafute watumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi. Watumishi Wana BUSARA ya kusuluhisha dhambi hiyo pande zote mbili Ili ufunguliwe.

2. USHOGA.

Ikiwa uliwahi kuwa shoga, ukaamua kuacha, kamwe usitubu sirini na kuishiwa hapo, USHOGA huambatana na mapepo na kufungwa NAFSI, mfungwa kamwe hawezi jifunguanpingu mwenyewe, unawahutaji watumishi wa Kweli Ili UOMBEWE na kuwekwa huru, sadaka ni LAZIMA Ili itolewe huko.

3. USAGAJI.

Mwanamke pia aliyewa kufanya dhambi hiyo, huwezi kufunguliwa na Utumwa na HATIA hiyo pekeako Kwa kutubu sirini, nenda Kwa watumishi wa Kweli, Ukiwa na sadaka ya Ukombozi.

4. PUNYETO/ KUJICHUA.

Ikiwa uliwahi kujichua, ukaamua kuacha, unahitaji kwenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi Ili ufunguliwe, Mpiga PUNYETO ni mfungwa, ni mke au mume wa Roho chafu katika Ulimwengu wa Roho, hivyo kufunguliwa ni LAZIMA utoe sadaka, uvunje NDOA chafu hiyo ya kiroho na hati ya NDOA chafu ya kiroho iondolewe, usipofanya hivyo, unajidanganya. Mbinguni huingii ng'o!!
Neno Hilo hapo juu ni ROHO. Amen.

5.MWANAMKE KUOA MWANAMKE/MWANAUME KUOA MWANAUME MWENZIE.

Kutubu dhambi hii sirini bila watumishi wa Mungu ni kujidanganya. Chukua sadaka, nenda Kwa mtumishi, Sema Kweli Ili UOMBEWE na kufunguliwa, NDOA haramu ivunjwe na ufungwa wako kiroho uondolewe. Amen.

6. ORAL SEX.

Ikiwa uliwahi kushiriki oral sex, kunyonya au kuramba Kwa mdomo sehemu za Siri za mwanamke au Mwanaume na ukatambua ni DHAMBI, ukaacha, Bado u kifungoni.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli wa Mungu ufunguliwe na Mungu.

7. ABORTION./ UTOAJI MIMBA/ KUFUNGA UZAZI/ KUTUMIA VIDONGE VYA KUPANGA UZAZI.

Kimbia haraka Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli ,beba sadaka kulingana na uwezo wako, UOMBEWE ufunguliwe.

Ukipuuza Utakataliwa GETI la Mbinguni.

9. IKIWA ULIWAHI TUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME/ KIKE.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.

10. MAUAJI.

Ikiwa uliwahi kuua bila kukusudia ,ukahukumiwa JELA ukatoka, ikiwa uliua Kwa Siri na hukubainika, ikiwa ulishiriki kuua, usijidanganye kuwa unaweza kutubu sirini, HATIA Ili ikuondoke uwe na Amani, Tafuta kiongozi wa Mungu wa Kweli mwenye BUSARA za Mungu, akuongoze Cha kufanya, utoe pia sadaka ya Ukombozi.

11. IBADA ZA SANAMU, KUSHIRIKI IBADA ZA WAFU NA KUTOA SADAKA KWA MIZIMU KIMILA NK NK.

Kushiriki Ibada za KIMILA na Kutoa sadaka Kwa Roho za kishetani za Mababu, ni DHAMBI pia, ni kufungwa ni Utumwa ambao huwezi kujifungua pekeako.

Ukiamua kuacha na kuokoka, hatua inayofuata ni kushirikisha watumishi kukusaidia kukutenga na madhabahu hizo.

Sadaka ni LAZIMA, sababu, Ulimwengu wa Nuru na Giza sadaka ni inevitable. Amen

HITIMISHO.

Dhambi nilizotaja hapo juu, ni baadhi tu ya dhambi ambazo huwezi tubu pekeako, zimetajwa sawasawa na Ruhusa ya Roho mtakatifu Kwa mtumishi wake sawasawa na ufunuo wake apendavyo.

NB: Si DHAMBI zote zinahitaji kuona mtumishi wa Kweli kukusaidia kufunguliwa pingu za dhambi, ni baadhi ya dhambi ambazo Zina vifungo na attachment na maagano ya kipepo na kishetani.

Mungu awabariki.

Source: Nabii Justine Ibrahim.

Amen.
hiyo ni kwa mujibu wa biblia ipi au ni experience yako binafsi
 
Ndugu,

Elewa jambo hili, ikiwa umezini na mke wa mtu, mumewe awe karibu au mbali, usiamze kwenda Kwa mume wa uliyezini naye tuomba msamaha,waeza poteza KICHWA chako na uhai.

Nenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli mwenye kifua, mshirikisha, atakupa njia za kulimaliza Hilo Kwa pande zote husika.

Upande wa Mungu, upande wa Muibiwa mke na upande wenu wazinifu.

Umeelewa mtumishi?

Kwa upande wa muibiwa ndio sijakuelewa, hapo mtumishi anamalizaje, Kwa hapo ndio hujafafanua.
 
Wewe hujaandika kwenye bandiko lako sadaka ya ukombozi ? Tunapiga kwenye hila kwingine hakuna tabu

Yaani hapo ndio adui kakaa ili kushusha thamani ya kazi ya msalaba

Tunafuta ujinga kwanza wengi wasipotezwe

Kula hiii afu tuendelee na swala la umuhimu wakushirikisha watumishi Wa Mungu hasa kwenye dhambi ainishwa
Au dhambi zinazokuzinga Kwa wepesi.

1 Petro 1:18 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
1 Petro 1:19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
Ndo nasemaje,

Kwakuwa sinwewe hukunipa ujumbe huu, siwajibiki kwako, hivyo sitafuta Wala kuongeza chochote Hadi pale aliyenipa ujumbe kuniambia nifanye hivyo.

Sadaka ya Ukombozi IPO kimaandiko, sadaka ya ZAKA haijafitwa, tena AGANO jipya sadaka ya ZAKA ndo imeongezwa kabisa Kutoka 1/10 Hadi 10/10.

Ukiniomba maandiko nitakupa andiko la YESU alimwambia TAJIRI. Nenda UZA Mali zako zote, wapewe maskini ndipo unifuate.

Bahiri haingii Mbinguni.

Yesu anasema uza Kila ulicho nacho, wapewe maskini,

Anamalizia kusema, Ilipo hazina Yako, ndipo ulipo moyo wako.

Kwa maelezo uliyoweka hapa nimejua shida ni ufahamu wako na anayeweza kukusaidia ni Roho mtakatifu pekee

Ni swala la Muda nadhani mi sina neno maana nimeshajua tabu ipo wapi?
 
Back
Top Bottom