Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
safi sana. hapo kwenye "si kwa fedha au dhahabu" hapo wengi wajue. hakuna pesa hata zingejaa dunia nzima zenye uwezo kusafisha dhambi. shetani huwa analeta kidogokidogo kafundisho, baadaye linakuwa fundisho kuu watu wanahama kwenye kazi ya msalabani nakuishi kwenye cults.Wewe hujaandika kwenye bandiko lako sadaka ya ukombozi ? Tunapiga kwenye hila kwingine hakuna tabu
Yaani hapo ndio adui kakaa ili kushusha thamani ya kazi ya msalaba
Tunafuta ujinga kwanza wengi wasipotezwe
Kula hiii afu tuendelee na swala la umuhimu wakushirikisha watumishi Wa Mungu hasa kwenye dhambi ainishwa
Au dhambi zinazokuzinga Kwa wepesi.
1 Petro 1:18 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
1 Petro 1:19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
kuna imani moja iliibuka mwaka 2003 hivi kama sikosei, ni ya mtu mmoja aliitwa Munuo, ndugu mmoja alikuwa kanisa la lutheran akahudhuria hiyo mikutano ya mwakasegee weee, akaanzisha kanis alake. yule mtu alikuja kuanzisha kanisa la Siloam, ambalo sasaivi wamebadili jina linaitwa Kanisa la Mungu Baba. wapi ndugu zangu wa karibu nawafahamu wanasali huko, na hata kipindi Munuo yupo hai niliwahi kwenda pale mbezi, nikaona uchafu mtupu nikakimbia mazima.
wale walichofikia kwa sasa, kutokana na hayohayo wanayaita mafunuo (amefunuliwa na Mungu ila kwenye Biblia hakipo), wanasema DAMU YA YESU IMEPUNGUA NGUVU, NA JINA LA YESU LIMEPUNGUA NGUVU, WANASEMA MASHETANI WAMELIZOEA SANA SIKIU HIZI HAYAKIMBII. KWAHIYO WAO HAWAOMBI KABISA KWA JINA LA YESU WALA DAMU YA YESU KWAO SI CHOCHOTE, WANAOMBA KWA JINA LA MUNGU BABA. yupi? wanamjua wenyewe. na Munuo alijiita yeye ni elitha Mungu mkuu. walimgeuza yule Munuo aliyejibadilisha na kujiita Eliya Mungu wa pili, wakamwita Eliya Mtishbi, yule aliyetabiriwa Malaki kwamba takuja (bila kujua huyo eliya ni Yohana Mbatizaji). Munuo alikuja kuugua tetenasi, akafia pale hospitali ya lugalo, hawakuzika siku kadhaa wakiamini atafufuka, wakaona ataoza tu wakaenda kuzika ile njia ya bagamoyo kule. wakati wa maziko kuna picha walipiga ni kama jini lilikuja kama kitu kinapanda wakasema amepaa, amepaaje wakati amezikwa hadi kaburi lake lipo na hajawi kufufuka?
hawa hawana tofauti na wengine wanaitwa the Branhamites, wafuasi wa mtumishi mmoja wa Mungu aliitwa William Branham wa Marekani, alikuwa na nguvu za MUngu mno hadi moto ulishuka waziwazi, ila sasa, ilifika kipindi akapotoka, akaanza kufundisha upotofu kwamba yeye ndiye Eliya, wasaidizi wake wakamwambia wewe usifundishe kwasababu alikuwa hajasoma shule kabisa na Biblia alikuwa haijui ili anajua tu kuweka mikono na kuponya magonjwa. akagoma. MUngu alimfunulia mtumishi wake mmoja aliitwa KENETH HAGIN kwamba Mungu amepanga kumwondoa aokoe roho yake kwasababu ameanza kufundisha mapotofu, akapata ajali akafa. cha kushukuru Mungu aliamua kumuondoa ili aponye roho yake. wafuasi wake pia hawakuzika wa siku nyingi wakidhani angefufuka, wakaishia kuwa na dhehebu la jina lake hadi leo.
Arusha kuna kanis akubwa kabisa la hawa watu wanaitwa the Branhamites, wanaweka hadi picha zake kwenye magari, Dodoma pia yupo jamaa anajitangaza kwenye mitandao, ni dhehebu kabisa la upotofu.
hivyo shetani huwa analeta kafundisho kamoja tu, halafu anatengeneza cult fulani itakayopotosha watu wengi ili aingie nao motoni. mafundisho mengi ya mwalimu kama ya mzaliwa wa kwanza, ukombozi kwa sadaka n.k, ni ya upotofu, hadi kina Benny HInn wamekuja kutubu hivi karibuni kwenye issue za kupanda mbegu, wamekiri walikuwa wanashurutishwa na walienda visivyo, kwasababu karama za Mungu hazinunuliki, hatuna uwezo huo kununua karama za Mungu au hata msamaha. Mungu asaidie kanisa lake linapotoshwa na hawa watu.