- Thread starter
- #501
Ungekuwa umeelewa, ungekubaliana na ufafanuzi nilotoa.Nimeelewa sana. Kwenye post yako umeweka orodha ya dhambi ambazo unasema mtu akizifanya hataweza kusamehewa mpaka amwone mtumishi wa Mungu, tena akiwa na sadaka ya ukombozi. Mimi nasema hivi, hiyo sio kweli. Mtu yeyote akiamua kumrudia Bwana Yesu, hata kama awe amefanya maovu ya namna gani, Bwana Yesu ATAMSAMEHE BURE, bila ya kuhitaji kuombewa na mtu mmoja. Neno la Mungu linafundisha kuwa, mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja tu, naye ni YESU. Kama mpatanishi ji Yesu tu, huyo mtumishi anayetaka watu wakamwone ni wa kazi gani?
Tunapokea msamaha wa dhambi bure kwa njia ya imani tu. Hiyo sadaka ya ukombozi ni ya kazi gani wakati Yesu alishajitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi za watu wote, pamoja na hizo ulizozitaja.
Kwa hiyo unataka kutuambia kuwa dhabihu ya Yesu haiwezi kumfanya mtu akasamehewa dhambi ya uzinzi au ushoga? Mwanadamu atatoa shilingi ngapi ili izidi thamani ya uhai wa Yesu?
Bado hujaelewa narudia. Soma tena na tena, maana uelewa inatofautiana.