kuna siku nmefanya research katika vitabu vya dini nikagundua shetani hajawahi kuua mtu, ila mungu kashaua wengi sana mpaka wasio na hatia sababu ya makosa ya wengine!
ah! niko around mazee!
Wewe umepotoka vibaya sana tena sana.
Anyways, sio kosa lako, kosa ni huna maarifa au ufahamu wa "NENO" la MUNGU.
Kwa kifupi sana nitakujulisha. Iko hivi:
MUNGU siyo "muuaji", kinachowaua Wanadamu ni "dhambi" na siyo MUNGU. Na aliyeleta dhambi duniani ni "shetani".
Kwa kuileta dhambi duniani shetani ndiye "muuaji" sababu pasipo dhambi hakuna kifo, kifo ni matokeo ya dhambi. Soma Yohana 8:44
Utaniambia mbona MUNGU alileta gharika ikaua mamilioni ya watu, au mbona MUNGU alishusha moto Sodoma na Gomora na kuua maelfu au utasema mbona MUNGU aliruhusu Waisraeli kuua mataifa yaliyokuwa nchi ya Kanaani.
Ndugu yangu unapaswa kufahamu kuwa MUNGU ni MKWELI na mwenye HAKI na kamwe hana UONEVU.
MUNGU amejiwekea laws and principles, sheria na taratibu zisizopindishwa wala kuyumbishwa na kitu chochote kile. Moja ya sheria hizo ni kwamba dhambi ikifanyika itazaa kifo. Hiyo iko hivyo na haibadiliki.
Ndiyo maana utaona kwamba kifo kilikuja baada ya dhambi kufanyika na aliyeleta dhambi ni Shetani hivyo automatically muuaji ni Shetani hata kama utekelezaji unafanywa na MUNGU. Ndiyo maana nikakwambia soma Yohana 8:44 imeandikwa, "Ibilisi ndiye muuaji tangia mwanzo".
MUNGU kwakuwa Yeye ni mwenye HAKI anasimamia sheria na taratibu zake sababu ndivyo impasavyo yeyote mwenye haki. Kwa kusimamia sheria na taratibu, watu wasiokuwa na "maarifa na ufahamu" wanamwona MUNGU kama muuaji.
Isitoshe, dunia na vyote viijazavyo wakiwemo viumbe wote, malaika na wanadamu, ni mali ya MUNGU. Ikiwa wewe una haki ya kusafisha nyumba yako na kutoa uchafu wote nje na kuuchoma moto na kuua panya na mende, viumbe usivyoviumba wewe, Je, MUNGU, hana HAKI ya kuisafisha dunia yake kwa kutumia sheria na taratibu alizoziweka??