Dhana nzima ya Futari na Daku

Dhana nzima ya Futari na Daku

vitu vizuri Duniani vipo vingi, ila vichache ni ivi.
1. Nidhamu_ kuwa sawa kiuhalisia na kuepuka makosa ya kawaida yanayokwepeka. mfano mtu kafunga yeye na wewe hupati madhara. kukaa kimya si dhambi.

2. Heshima_ kuwathamini wengine kwenye hisia zako. jichukulie wewe na yule au uyu.

3. Ujuzi_ utambuzi wa mambo na kufanya manbo kiufanisi.


# Mungu tubariki sana kizazi hiki.
Mambo ya ajabu lazima ku comments. Hii dunia iko hivyo, seeking knowledge in various fields
 
Kuamini bila sayansi ni upuuzi! Wwe ni NGUIN ndiyo maana huelewi kitu
Tayari wewe umeshaiamini Sayansi kwa hiyo waache na wengine waamini wanachoamini, kabla hiyo Sayansi haijaja Watu walikua hawaishi?
Wazazi wako wenyewe wanaamini Dini na wewe umezaliwa kwenye Dini ila kielimu uchwara kidogo tu tayari ushajikuta wewe ndio mvumbuzi wa Dunia,

Hao Wanasayansi walizikuta hizo Dini na Imani zingine mnachopaswa ni kuheshimu wengine.
 
Kuna post moja nimeiyona ingawa ilikuwa inazungumzia kwaresma lakini mwandishi wa post hiyo alikuwa na lengo la kukashifu dhana nzima ya Futari na Daku.

Kwake yeye Kwa mujibu wa Imani yao wanakula chakula chochote kile tofauti na watu wa Imani nyingine ambayo pasina kuficha na Imani hii ni Uislamu.

Kwa uelewa wa mwandishi anachoelewa yeye kuhusu Futari cha kwanza kinachomjia kichwani kwake ni uji, viazi au mihogo na tambi, kwake yeye hiyo ndio Futari.

Na Daku ni chakula ambacho kinaliwa usiku sana kama ugali, wali na ndizi na kadhalika, kwahiyo kana kwamba anaona fahari kwamba wao hawana mambo hayo kwahiyo mambo yao yapo super.

Ningependa nimpe elimu juu ya mambo haya ili ukungu umtoke katika ubongo wake na apate kujua usahihi wa dhana ya Futari na Daku ili kesho na kesho kutwa asirudie tena kuongea huo upuuzi.

Futari imetokana na neno kufuturu kwa Kiswahili chepesi ni mlo wa kwanza baada ya kufunga swaumu, kwahiyo kile chakula cha kwanza kukila baada ya kufungua ndio huitwa Futari, na yaweza kuwa tende au maji, ukipata kimoja kati ya hicho hapo tunasema umefuturu, na chakula kingine ni ziada tu kwa maana kinahesabika kama chakula kingine tu.

Tofauti na watu wa Imani nyingine, Futari au kufuturu ni ibada na ina utaratibu wake, miongoni mwa mambo muhimu ya kufanya kwa mwenye kufunga ni kutakiwa kufuturu mapema au haraka mara baada tu ya kuingia Magharibi baada ya jua kuzama.

Hapo hutakiwa kupata tende au maji kwani hivyo ndio vitu ambavyo ni Sunna kutoka kwa Mtume wetu, lakini hata hivyo hakuna aweza kufuturu Kwa biskuti, matunda, karanga au na chochote kile ambacho anaweza kuipata Kwa wakati huo, hapo ndio tunasema kufuturu.

Kwahiyo funga ya muislamu au mwezi wa Ramadhani unaweza kufungwa hata bila ya uwepo wa uji, au viazi, ndizi, magimbi na kadhalika, hivyo ni vyakula tu ambavyo vimezoeleka lakini sio kwamba bila hivyo haipatikani funga, mtu anaweza kufuturu kwa chai na mkate au chapati na hiyo ndo ikawa Futari yake.

Daku ni chakula ambacho huliwa usiku Sana na inashauriwa kuanzia saa nane, tisa mpaka saa kumi usiku, lakini hii nayo ni ibada pia, kwa maana ni bora zaidi kuchelewa kula Daku kama ambavyo ni bora zaidi kuwahi kufuturu, na unapata thawabu kwa kufanya haya.

Daku ni chakula kilicho barikiwa na ndio maana waislamu wanasisitizwa sana mwezi wa Ramadhani wajitahidi Kula Daku, lakini ifahamike kwamba Daku inaweza kuwa glasi moja ya maji au maziwa, au chai na andazi au chapati, ili mradi tu upate chochote kidogo cha kula usiku huo, na hiyo ndio Daku.

Kwa mfano unaweza kula wali wako au ugali saa tano usiku halafu usiku ukaamka kunywa chai tupu au juisi au maziwa ndio ikawa Daku yako, hapo unapata baraka.

Na haya mambo ya kudhani Futari ni viazi, mihogo, ndizi, magimbi na uji au chai huwa tatiza hata baadhi ya waislamu kwa kusema hawana hela ya Futari na hivyo kushindwa kufunga swaumu, huo ni uelewa mbaya sana na ni kukosa maarifa kabisa.

Tupende kujifunza na kupata elimu ili tufanye mambo sahihi kwa wakati sahihi kabisa.

Natumaini wale ambao walikuwa na uelewa mbaya kuhusu Futari na Daku walau kwa uchache watakuwa wamepata maarifa na kutoa ukungu katika vichwa vyao.

Ni hayo tu!

johnthebaptist
Numbisa
Mwendo ni uleule kula na kuvimbiwa

Mnakula Sana kipindi Cha mfungo wenu

Yani waislamu ukikutana nao kaa nae mbali akicheua ni mavimbizi tu
 
Kama unaweza kula chakula kizito mida hiyo ni vizuri ili ikupe nguvu/ stamina ya kufunga vizur mchana,
Inakupa kushiba mchana kutwa inamaana hujafunga

Waislamu hamfungi mnabadili mda wa Milo mchana usiku

Kuna ndugu zangu wailsamu mpaka wanaendaka kukopa wale Sana kipindi Cha mfungo , mfungo ukiisha wamenenepa
 
Inakupa kushiba mchana kutwa inamaana hujafunga

Waislamu hamfungi mnabadili mda wa Milo mchana usiku

Kuna ndugu zangu wailsamu mpaka wanaendaka kukopa wale Sana kipindi Cha mfungo , mfungo ukiisha wamenenepa

Wewe chizi kweli mtu wangu.

Aliekwambia kila anaekula Daku anashiba mchana kutwa ni Nani?
 
Mfano.

Wanafunzi waanze kwenda shule saa moja usiku Hadi saa kumi na moja Asubuhi.

Alafu waje watuambie eti wamefunga shule.
Imani ya DINI ya MAKOBAZI ni ya Hovyo sana.

Kila siku tunasema imetengenezwa Roma hamuelewi
Funga wewe usiku na mchana
 
Okay Kwa timetable hii INA maana watakuwa wamecheki Hali ya anga ikoje na kujua kuzama Kwa jua kunakuwaje
Imani ya waislamu inasema Jua linaenda kusujudu
Allah hawezi kufanya adjustment akaliruhusu lisujudu haraka na litoke chini ya maji yenye tope ?
 
Mwendo ni uleule kula na kuvimbiwa

Mnakula Sana kipindi Cha mfungo wenu

Yani waislamu ukikutana nao kaa nae mbali akicheua ni mavimbizi tu
Watu wanakula jasho lao we unaumia,una akili sawasawa!?..Sasa hivi Kuna wenzio wanakula bia na kitimoto baa huko lakini huoni ajabu
 
Watu wanakula jasho lao we unaumia,una akili sawasawa!?..Sasa hivi Kuna wenzio wanakula bia na kitimoto baa huko lakini huoni ajabu
Shida sio kula jasho lako , shida ni kula Sana usiku kucha na kuvimbiwa

Ofisini wakija wanatucheulia mavimbizi

Na mwezi wenu mnakopa Sana ili mle Sana
 
Shida sio kula jasho lako , shida ni kula Sana usiku kucha na kuvimbiwa

Ofisini wakija wanatucheulia mavimbizi

Na mwezi wenu mnakopa Sana ili mle Sana
Huwa unaugua kichaa!?..wanaokesha bar huwa hawakucheuliii mavimbizi ofisini!?
 
Back
Top Bottom