Dhana nzima ya Futari na Daku

Dhana nzima ya Futari na Daku

Daku inaambata na Vigoma siku hizi ukifika mwezi wa Ramadhan vile Vigoma vya Kula Kula Daku Mpemba na kinyago anaecheza Vigoma hakuna tena, sijui nani alieua vile Vigoma vya Daku siku hizi hakuna watu wanawaza kula tu na kula kwenyewe wanakula kiuchoyo zamani ukifika mda wa futari unachagua Baraza la kwenda kula na hufukuzwi na kingine utakuta umeletewa nyumbani ule,

Yaan zamani mwezi wa Ramadhani waislamu walikua wakalimu sana nazungumzia waislamu wote sio wahisani Ila siku hizi sijui njaa imezidi Ramadhan waislamu wanakula wenyewe ule utaratibu wa kula kibarazani umekufa hakuna kukaribisha mtu na hakuna kumpelekea mtu (jirani) chakula,
tatizo siku hizi waisilam waeiga tabia za kikirisito baada ya kuishi changanyikeni
 
common sense inanileta kuelewa kuwa daku ni kujiandaa masaa mengi kuhimili njaa! Unakula /inakunywa saa kumi hayo maji/uji ili ikusaidie kufika saa 12 , maana si rahisi/ni mateso kuhimili njaa,, kiu etc kwa saa zaisi ya 12 kesho yake.

Hivi tabu yote ya nini? Unatafuta nini? Bada? Kwani lazima ujitese? Ili iweje? Kuingia mbinguni? Who knows kama kuna Mungu? IMANI, IMANI IMANI
hako kaeimu kako kana kufanya kuwa zoba zezeta
 
Mkuu kule nilimuambia mdau aniletee ushahidi wa umiliki wa neno daku na futari kwa dini aliyokua anaishabikia. Maana povu lilimtoka kuwa kachokozwa.

Sasa kama mnakula daku mida hio ya usiku inamaanisha asubuh na mchana hamtakuwa na njaa iweje baadhi ya maeneo mnapiga marufuku watu kula na kufanya biashara ya chakula kuwa mtatamanishwa wakati mnakua mmeshiba?

Inakuaje mnamcharaza mtu viboko huku mkimuita kobe wakati ni maamuzi yake kula,kwann funga iwe lazima?
hakuna andiko la kumzuia mtu kula mchana mfano msafiri kikongwe watoto wadogo wajawaito wanao nyoyesha nk ukizuya kupika mchana watu hawa watapata wapi chakula? hata huko pemba ukijieleza mbona unalusiwa kula tu ila sio kwa wale waisilamu wenye uwezo wakufunga wale mchana
 
Swali zuri Sana madam Numbisa

Kama nilivyoeleza awali maana halisi ya Daku,pamoja na mambo mengine ni kumuwezesha mfungaji kuwa na stamina ili apate kuendelea na majukumu yake kama kawaida pasina kuwa na uchovu mwingi

Sasa,

Dhana nzima ya kuwazuia watu Kula chakula hadharani au kuuza vyakula ni Kwa Nia moja Tu kuheshimu mwezi mtukufu WA ramadhani na kuwahimiza watu wafunge au watekeleze ibada ya funga.

Na utaratibu huo hufanywa kwenye maeneo yenye waislamu wengi kama Zanzibar Kwa maana wengi wao ni waumini WA kiislamu hivyo hawana budi kufunga,na si rahisi kukuta huku bara kuna mambo kama hayo.

Lakini hata Kwa utashi WA kawaida Tu Kwa ibada kama ya mwezi wa ramadhani ambayo ni maarufu Sana na waislamu wengi wanafunga je si Busara basi kutokula hovyo hovyo hadharani?

Ebu chukulia wewe Numbisa let's say upo na wapangaji wenzako karibia wote wamefunga je itakuwa Busara ukiwa nao barazani mnabadilishana mawili matatu basi ukawa na msosi wako unakula mbele yao je ni Sawa?
wakiristo wanao ishi visiwani zanzibar ngazija komolo mambasa tanga mtwala kondoa uwa wanaheshimu sana mwezi wa ramadhani tena kuliko baadhi ya vijana wa kiisilamu
 
AKILI ZA HOVYO SANA.

YANI UNAKULA USIKU KUCHA MCHANA HULI UNASEMA UMEFUNGA.

UMEBADILISHA RATIBA. YA MSOSI UNAJIITA UMEFUNGA.

HOVYO SANA HII.

Biblia inasema.
OLE WAO WAUGEUZAO USIKU KUWA MCHANA.
Tuambie wewe maana ya kufungua tupate faida.

Tujuavyo sisi Waislamu kufungua ni kujizuia kula, kunywa, kufanya jimai na madhambi mengine kuanzia alfajiri ya kweli mpaka just linapo zama.

Type wewe maana ya fungal kwaujibu wa Biblia.
 
AKILI ZA HOVYO SANA.

YANI UNAKULA USIKU KUCHA MCHANA HULI UNASEMA UMEFUNGA.

UMEBADILISHA RATIBA. YA MSOSI UNAJIITA UMEFUNGA.

HOVYO SANA HII.

Biblia inasema.
OLE WAO WAUGEUZAO USIKU KUWA MCHANA.
Hawa jamaa wanabadilisha muda wa kula na sio kufunga.Mtu anaanza kula saa 12 hadi saa 11 usiku. Huku ni kufunga au kubadili ratiba?
 
Kuna post moja nimeiyona ingawa ilikuwa inazungumzia kwaresma lakini mwandishi wa post hiyo alikuwa na lengo la kukashifu dhana nzima ya Futari na Daku.

Kwake yeye Kwa mujibu wa Imani yao wanakula chakula chochote kile tofauti na watu wa Imani nyingine ambayo pasina kuficha na Imani hii ni Uislamu.

Kwa uelewa wa mwandishi anachoelewa yeye kuhusu Futari cha kwanza kinachomjia kichwani kwake ni uji, viazi au mihogo na tambi, kwake yeye hiyo ndio Futari.

Na Daku ni chakula ambacho kinaliwa usiku sana kama ugali, wali na ndizi na kadhalika, kwahiyo kana kwamba anaona fahari kwamba wao hawana mambo hayo kwahiyo mambo yao yapo super.

Ningependa nimpe elimu juu ya mambo haya ili ukungu umtoke katika ubongo wake na apate kujua usahihi wa dhana ya Futari na Daku ili kesho na kesho kutwa asirudie tena kuongea huo upuuzi.

Futari imetokana na neno kufuturu kwa Kiswahili chepesi ni mlo wa kwanza baada ya kufunga swaumu, kwahiyo kile chakula cha kwanza kukila baada ya kufungua ndio huitwa Futari, na yaweza kuwa tende au maji, ukipata kimoja kati ya hicho hapo tunasema umefuturu, na chakula kingine ni ziada tu kwa maana kinahesabika kama chakula kingine tu.

Tofauti na watu wa Imani nyingine, Futari au kufuturu ni ibada na ina utaratibu wake, miongoni mwa mambo muhimu ya kufanya kwa mwenye kufunga ni kutakiwa kufuturu mapema au haraka mara baada tu ya kuingia Magharibi baada ya jua kuzama.

Hapo hutakiwa kupata tende au maji kwani hivyo ndio vitu ambavyo ni Sunna kutoka kwa Mtume wetu, lakini hata hivyo hakuna aweza kufuturu Kwa biskuti, matunda, karanga au na chochote kile ambacho anaweza kuipata Kwa wakati huo, hapo ndio tunasema kufuturu.

Kwahiyo funga ya muislamu au mwezi wa Ramadhani unaweza kufungwa hata bila ya uwepo wa uji, au viazi, ndizi, magimbi na kadhalika, hivyo ni vyakula tu ambavyo vimezoeleka lakini sio kwamba bila hivyo haipatikani funga, mtu anaweza kufuturu kwa chai na mkate au chapati na hiyo ndo ikawa Futari yake.

Daku ni chakula ambacho huliwa usiku Sana na inashauriwa kuanzia saa nane, tisa mpaka saa kumi usiku, lakini hii nayo ni ibada pia, kwa maana ni bora zaidi kuchelewa kula Daku kama ambavyo ni bora zaidi kuwahi kufuturu, na unapata thawabu kwa kufanya haya.

Daku ni chakula kilicho barikiwa na ndio maana waislamu wanasisitizwa sana mwezi wa Ramadhani wajitahidi Kula Daku, lakini ifahamike kwamba Daku inaweza kuwa glasi moja ya maji au maziwa, au chai na andazi au chapati, ili mradi tu upate chochote kidogo cha kula usiku huo, na hiyo ndio Daku.

Kwa mfano unaweza kula wali wako au ugali saa tano usiku halafu usiku ukaamka kunywa chai tupu au juisi au maziwa ndio ikawa Daku yako, hapo unapata baraka.

Na haya mambo ya kudhani Futari ni viazi, mihogo, ndizi, magimbi na uji au chai huwa tatiza hata baadhi ya waislamu kwa kusema hawana hela ya Futari na hivyo kushindwa kufunga swaumu, huo ni uelewa mbaya sana na ni kukosa maarifa kabisa.

Tupende kujifunza na kupata elimu ili tufanye mambo sahihi kwa wakati sahihi kabisa.

Natumaini wale ambao walikuwa na uelewa mbaya kuhusu Futari na Daku walau kwa uchache watakuwa wamepata maarifa na kutoa ukungu katika vichwa vyao.

Ni hayo tu!

johnthebaptist
Numbisa
MashaaAllah
 
Daku ni lunch iliyochangamka.......... mabadiliko tu ya ulaji.........ivi kuna mtu anaweza kula msosi mzito saa 9 au 10 Usiku ashindwe kufika saa 1830pm?
 
common sense inanileta kuelewa kuwa daku ni kujiandaa masaa mengi kuhimili njaa! Unakula /inakunywa saa kumi hayo maji/uji ili ikusaidie kufika saa 12 , maana si rahisi/ni mateso kuhimili njaa,, kiu etc kwa saa zaisi ya 12 kesho yake.

Hivi tabu yote ya nini? Unatafuta nini? Bada? Kwani lazima ujitese? Ili iweje? Kuingia mbinguni? Who knows kama kuna Mungu? IMANI, IMANI IMANI
Na hio inatokana maana ya kufunga ,'nikujizuia kula ,kunywa.......katika mchana wa Ramadan '
 
tatizo siku hizi waisilam waeiga tabia za kikirisito baada ya kuishi changanyikeni
Zamani ilikua raha sana yaan muislam haangalii sijui wewe khafr au singasinga anakuletea vitafunwa km tende, sambusa, chapati, kababu, visheti, keki, zinasindikizwa na uji wa iliki na pilipili manga za kutosha au unakuta maharage yaliyotiwa sukari unakula bure barazani,

Na kingine ukifika nyumban unakuta umeletewa haijalishi umefunga km wao au haujafunga walikua wanagawa chakula kwa majirani zao wa karibu, nashangaa siku hizi ikifika mwezi wa Ramadhani futari biashara inauzwa wakati zamani ilikua bure
 
Mfano wako sio sahihi, kwa sababu unachanganya mambo ya dini na sayansi.
Pia napinga kuwa brainwash watoto katika dini wakiwa wadogo, waachwe wakuwe kama watoto wengine waamue wenyewe mambo ya dini wakiwa watu wazima.
Unamaanisha nini ukisema hivyo,kwamba wanafundishwa vitu vya uongo au
 
Back
Top Bottom