Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,812
- 107,628
Well, previous I developed a topic for y’all lads centered on God’s omniscience-ness and I discussed a bit on how death can be affected by conscience. So this topicwill be serving as a tie-in spinoff and will be focusing on death and conscience respectively.
Imekua kama jambo la kawaida kwa watu karibia wote kila inapotokea kifo Fulani watu wanasema kwamba kifo chake kilikua kishapangwa na Mungu, unaweza kumwambia bodaboda kua endeshe pikipiki vizuri unaweza pata ajali ukafariki mara nyingi hua wanajibu kua Mungu ndio atakua kashaandika kifo chake afe hivyo. Bahati mbaya hata viongozi wetu weng wa dini zote hupendelea kufundisha/kusema kwamba Fulani kifo chake kilikua kishaandikwa atakufa hivi huo ni uongo mkubwa haiwezekani mtu wewe na akili zako uamue kujinyonga na kukatisha uhai wako kisa “My wako”hajibu text au kakupiga kibuti halafu watu waseme kwamba eti kifo chako kilikua kishaandikwa utajinyongo, never.
Hii ni dhana ya kumtupia lawama Mungu kwa mambo asiyohusika ni mbaya imekua ikiwafanya watu wasiwe makini katika mambo ya kujali uhai wao kwa kisingizio kwamba Mungu kapanga, pikipiki unaendesha kama upo ESPN na kuovateki magari hovyo ufe useme Mungu kapanga utakufa kwa ajali…..lakini inawezekana hii ni mbinu ya kuCope na maumivu ya uchungu wa kuondokewa na mtu wao waliyojitengenezeawatu bila wao wenyewe kujua. Ukweli ni kwamba Mungu hapangi vifo vyetu kamwe na hajui tutakufaje.
Theory of Everything….and Space-time Continuum
Kun mambo matatu duniani mwanadamu hana ujanja wa kuyakwepa lazima ayapitie ambayo ni Njaa,kusinzia na kufa. Hata uwe nani lazima usikie njaa, lazima pia usinzie fanya ufanyavyo ni lazima mwanadamu ulale masaa nane na usipolala hayo masaa nane lazima uyalipe hata ukilala masaa 7 na dakika 55 hizo dakika tano utazilipa tu hata ukiwa unatmbea au umekaa. Kwa kila kiumbe hai ni lazima kife labda nguvu inayotoa uhai iruhusu kisife (Mungu), Mungu alipotuumba alitupa pumzi yako yenye uhai wa milele usio na kikomo (Everlasting eternity) ndio maana wewe binafsi yaani yule unayejisikia ndani mwako kamwe hautakufa bali mwili wako huu wa nyama ndio utakaokufa..kama nilivyosema kwenye mada zilizopita kwamba mwanadamu ndio kiumbe pekee mwenye sifa ya Mortal and immortality yaani ana roho isiyokufa na mwili unaokufa hivyo anaweza kuishi ulimwengu wa roho au ulimwengu wa nyama. Nini kinatokea hadi tunakufa?
Time (muda) unanafasi kubwa katika uhai wa mwanadamu japo unaweza kuuchukulia kawaida ila wenyewe ndio unafanya maisha yawe hivi yalivyo leo hii, kwanza kabisa kila kitu kina Lifespan yaani muda wa kudumu wa kitu hicho kwa wanaofata vitabu vya dini vinasema lifespan ya mwanadamu ni miaka 70 tu na ikizidi hapo basi nai neema/favor umepata. Muda ndio unafanya ulivyokua mwaka 2015 sio ulivyo leo 2022. Kiuhalisia muda ndio unafanya mwanadamu tufe na kama tukiweza kuudhibiti muda basin a kifo tutakikwepa. Mtu unapokua mtoto wa 0yr mpaka 22yrs seli zinazozalishwa mwilini mwako zinakua ni nyingi zaidi ya zile zinazokufa (?)ndio maana mtu anakua(growth) ila akifika miaka 22 mpaka 50 tu basi mwili unaacha kukua maana anakua yupo kwenye hatua ya Stagnant amabapo seli zinazozalishwa na zinazokuafa zinakua kiwango kimoja ndio maana mtu akifika miaka 22 basi hata refuka tena kinachobakia ni mwili kwenda kwenye hatua ya Development….yaani kunenepa,mifupa kukomaa zaidi,sura kua ya kiutu uzima nk. Ukifika miaka 50 seli zinazozalishwa zinakua chache kuliko zile zinazokufa hapo mtu anaanza kuzeeka na kuchokakama yupo kwenye graph basi anakua anatembelea kwenye row ya utotoni baada ya hapo mtu unakua unasubiri kufa tu nothing more.
mwili wa binaadamu umewekewa Muda fulani ukifika tu basi roho yako haina budi kuuacha mwili, sasa hapo haijalishi Roho yako itauacha mwili kwa kutumia njia ipi na katika njia hizo hakuna njia aliyokupangia Mungu utakufa kwa njia hii, Never.
Mungu hajatupangia tufe kwa aina ipi ya kifo bali matendo yetu ya kila siku ndio yanaonyesha kifo chetu kitakua vipi na kadri unavyobadiri matendo na kifo chako kinabadilika. Chukulia kwamba kifo ni GPS na matendo ni Coordinates, ukiwa hapo ulipo GPS yako inasoma upo kwenye spherical au ellipsoidal coordinates zipi na pindi utahama kidogo hapo ulipo basi GPS yako itasoma coordinates tofauti na zile za mwanzo. Na kifo ni hivyo hivyo matendo yako,shughuli zako na tabia zako zinaonyesha kifo chako kitakua cha aina gani. Kama ni dereva,mwizi,fundi,mbea,muongo, mlevi, basi shughuli na tabia zako hizo zinaonyesha utafariki kifo cha aina gani na kama ukibadirisha matendo yako basi kifo chako kinabadirika pia. So aiana ya kifo cha mtu sio constant bali iko defined na matendo na tabia zako wewe.
Free will inaplay part kubwa sana kwenye hatima ya maisha yetu hapa duniani, jinsi maisha yako unavyoweza kuamua yawe vile unavyotaka kwa tabaia na matendo yako basi ndio pia matendo na tabia zako zinaweza kuamua kifo chako kiwe cha aina ipi. Nadahani ni muda sasa wa kuongozwa na imani pamoja na maarifa katika masuala ya dini.