Binafsi naamini kwenye familia, mmoja anaweza kuinuliwa ili aweze kuwainua wengine. Ndiyo maana kwenye maandiko Kitabu cha Mwanzo 42:25-28 unaona Yusufu alivyoinuliwa ili kuwasaidia ndugu zake. Kuna mtu anaweza kujiuliza kwani ni lazima kuwasaidia ndugu zako, Jibu sio lazima (Sijui kama kuna sheria inayolazimisha ndugu kusaidiwa hata Baba/Mama sio lazima) kuwasaidia lakini unajiuliza ni faida kiasi gani unapata kuona ndugu zako wakihangaika mitaani bila mafanikio wakati wewe ukiwa na nafuu?
Binafsi nimejaribu mara kadhaa kuwainua ndugu zangu (Tumbo moja) bila mafanikio mwisho wa siku najikuta napoteza mitaji tu. Natolea mfano, mwaka fulani nilimpa brother angu mtaji wa kumwezesha afanye biashara fulani iliyonigharimu kiasi. Bahati mbaya biashara akaiua/akala mtaji. Next time, nikampa mtaji mdogo wangu afanye biashara fulani aliyoitaka. Bahati mbaya naye akapoteza mtaji bila kufanikiwa. Simu za brother zikawa nyingi kuomba assistance huku akinishtakia kwa Wazee. Baada ya mivutano kidogo nikampa mtaji mwingine. Shida inakuja kwenye suala la kuikuza biashara na kuiendeleza, brother anafail, Kwahiyo baada ya muda mtaji huu pia ukafa.
Sasa nimempa mtaji wa mwisho wa biashara, akipoteza na huu Potelea mbali. Sitajali lawama za Walimwengu, hata Mungu anaona nilivyojitolea.
Swali, Je, kuna haja ya tunapowapa mitaji ndugu zetu(tuandikishiane) na tuanze kutoza riba ili kuongeza uwajibikaji (accountability)?? Jambo hili litakuwa na athari zozote kwa ustawi na mahusiano ya familia?
Kwanza kabisa hongera kwa moyo wa kusaidia.
DDC Mlimani Park walikuwa na wimbo wao mmoja, baadhi ya mashairi ya ule wimbo yanasema.
"Usitumie peeesa, kama fimbo baba
Mambo ya pesa hutaka makubaliano, hapo ndipo pesa huwa na thamani eee".
Pesa inataka makubaliano kwanza, si kutoa tu ukifikiri itamaliza kila tatizo.
Mimi nilimkopesha ndugu mmoja (a cousin) mtaji miaka mitatu iliyopita, akapotea hakulipa. Hilo halikuwa tatizo kwangu, kwani nilivyompa hela sikutegemea zirudi.
Ikafikia wakati akapatwa na msiba namtafuta simpati, mpaka nikajiuliza, huyu anashindwa kupokea simu zangu za rambirambi kwa sababu anafikiri nitamkumbushia kumdai zile pesa ama vipi? Nilihuzunika sana.
Mwaka huu kanirudia tena ana matatizo, kanisihi sana, najua ana matatizo. Tangu kipindi cha huo msiba hajakaa sawa.
Nimemsaidia tena. Kwa kuwa naelewa matatizo yake. Safari hii nimemwambia nampa tu msaada, asiwe na pressure ya kunilipa pengine hata kuogopa kupokea simu.
Kikubwa ni kutaka kuelewa tatizo na kusaidia zaidi ya pesa tu.
Pesa unatuma muamala tu umemaliza. Kwa hiyo kama unazo, ni kitu rahisi sana.
Kuna cousin wangu mmoja alikuwa anasema "kitu kinachotatuliwa na pesa si tatizo, hiyo ni gharama tu, expense. Matatizo halisi hata pesa haiwezi kuyatatua".
Kwa hiyo, elewa tatizo.
Kwa mfano. Inawezekana ndugu yako hana business plan, au haja target business nzuri, au ame target business nzuri lakini eneo si zuri.
Hapo hata ukimsaidia pesa atashindwa biashara tu na kurudi kutaka pesa zaidi.
Naelewa na wewe una maisha yako na labda huna muda wa kuchukua majukumu ya mtu mwingine kuhakiki mambo, lakini, hatua hii inaweza kukufanya uelewe tatizo vizuri zaidi, na uepuke matumizi mabaya ya pesa huku ukiwa unamsaidia ndugu yako vizuri zaidi.
Kitu kikubwa zaidi ni hiki, saidia kwa moyo, usisaidie kwa sababu mtu kakushitaki kwa wazazi.